Friday, November 27, 2020

KUNA SIKU MZEE BAKHRESA ATAUCHUKIA MPIRA!

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA OSCAR OSCAR

HAKUNA jambo baya katika maisha ya mwanadamu kama kukata tamaa. Hatua hii hufikiwa pale mwanadamu anapojaribu kila njia kufanikisha jambo lakini matokeo yanakuwa kinyume na matarajio. Inasikitisha sana kuona miaka nane ya Azam FC kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara wakitwaa ubingwa mara moja.

Inasikitisha kuona nguvu anazotumia mmiliki wa klabu hiyo, mzee Said Bakhresa, katika uwekezaji hazizai matunda. Wasiwasi wangu isijefikia wakati mzee akaona ni bora aendelee kuzalisha ice cream kuliko kuendelea kuwekeza kwenye soka.

Timu yoyote yenye uwekezaji mkubwa duniani hutegemea pia kupata mrejesho unaoendana na uwekezaji na ndiyo maana kuna kazi kubwa kufundisha klabu kubwa kama Real Madrid, Bayern Munich, Manchester United na vingine vingi barani Ulaya, kama kocha atashindwa kuleta mafanikio ndani ya klabu. Azam FC imefanya uwekezaji mkubwa sana lakini mrejesho wake ni hasara tupu!

Hivi karibuni Azam FC wametoka kutimua benchi lao lote la ufundi likiongozwa na kocha mkuu, Zeben Hernandez. Mimi sina tatizo na maamuzi haya kwa sababu namba hazidanganyi. Mhispania amechemsha katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ushindi mara saba, sare mara sita na vichapo mara nne si matokeo yanayoweza kuipeleka Azam FC mbele.

Lakini cha kujiuliza, uongozi wa Azam ulitumia vigezo gani wakati wa kumwajiri huyo “Pep Guardiola” wao? Nafikiri hapa ndiyo kuna shida kubwa sana katika uongozi wa Azam. Nafikiri kuna watu wananufaika na mwendelezo huu wa kuingia na kutoka kwa makocha na wachezaji.

Hakuna mwenye uchungu wa kuvunja mikataba ya makocha na wachezaji kila kukicha isipokuwa mzee Bakhresa. Kwa mtindo huu, kuna siku mzee atauchukia mpira kabisa. Kuna siku mzee ataona ni bora aendelee kuzalisha tu ice cream kuliko kuihudumia timu!

Azam FC imekosa watu wenye nia ya dhati ya kuipeleka mbele timu hiyo. Wengi wanaoajiriwa, wanakwenda kama watu waliopata fursa ya kutengeneza maisha  yao ya baadaye. Kila mmoja anapambana kuhakikisha anajijenga akiwa Azam na anakuwa karibu na watoto wa bosi.

Wachache sana wana mtazamo wa kuifanya Azam FC iwe timu inayoweza kujiendesha yenyewe. Kwa bahati mbaya sana wengi wanadhani Azam FC ni klabu tajiri Tanzania. Ndugu zangu si kweli, Azam FC ni klabu masikini isipokuwa mmiliki wake ndio tajiri. Azam FC inapaswa kuwa klabu inayotengeneza mapato yake.

Inapaswa kuwa klabu inayoweza kuajiri kocha na kusaini wachezaji kwa fedha za klabu na si za mzee Bakhresa. Hiki ndicho kinachokosekana ndani ya klabu ya Azam. Wafanyakazi wote wanapaswa kulipwa kutokana na kile walichozalisha ndani ya klabu, lakini kitendo cha kuendelea kutoa fedha kwenye ice cream na kuwalipa mishahara wachezaji, siku zote kitaifanya Azam FC iendelee kuwa fursa ya watu kujipigia fedha tu.

Mwaka 2017 unapaswa kuwa mpya kwa Azam FC kabla mzee Bakhresa hajauchukia mpira. Mtendaji mkuu anapaswa kuhakikisha timu inajiendesha yenyewe angalau kwa asilimia 50. Kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha ndani ya klabu kwa sababu tu hakuna mwenye uchungu na fedha hizo.

Kama watu wangekuwa na uchungu na fedha zinazotumika, isingekuwa rahisi kuingia mikataba na wachezaji wa kubahatisha. Wala hakuna ubishi Azam FC wanasajili kwa kiasi kikubwa kwa kubahatisha na ndiyo maana kutwa hawaishi kuvunja mikataba.

Azam FC si klabu tajiri kama wengi wanavyodhani, isipokuwa mmiliki wake ndiye mwenye utajiri. Ukitaka kulijua hilo, chukua kiasi cha fedha wanachoingiza Azam FC kwa mwaka kisha toa matumizi yao kwa mwaka mzima.

Ukipata jibu, kaa nalo usimwambie mtu. Kama kila mchezaji, kocha au kiongozi ataajiriwa Azam FC akiwa na mtazamo kuwa Azam FC, ni klabu changa isiyo hata na miaka 10 kwenye ligi, klabu masikini kiuchumi kutokana na vyanzo vyake vichache vya mapato, klabu ambayo ina ubingwa mmoja tu wa Ligi Kuu Tanzania, kuna uwezekano mkubwa wakapiga hatua mbele.

Lakini kama wataendelea kuajiri watu wenye mtazamo wa Azam FC ni timu tajiri zaidi Afrika Mashariki, timu ya fursa, timu ya kupata kiinua mgongo, kuna siku mzee Bakhresa atauchukia kabisa mpira. Ataona ni bora kuzalisha ice cream kuliko kuihudumia Azam’ FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -