Thursday, November 26, 2020

KUNA WATU WATANUNA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

WINFRIDA MTOI

YANGA wametamba kuendelea kuwakera wapinzani wao, hasa Simba, kwa kuchukua pointi nyingine tatu leo watakapovaana na Gwambina katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), utakaochezwa kwenye Uwanja wa Gwambina Complex, uliopo Misungwi, Mwanza.

Mchezo huo utakuwa wa tatu mfululizo kwa Yanga wakiwa Kanda ya Ziwa baada ya kufanikiwa kushinda miwili iliyopita na kujizolea pointi sita.

Yanga ilikwenda jijini Mwanza wiki iliyopita na kuanza kucheza na KMC na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kabla ya kuelekea mkoani Mara kuvaana na Biashara United na kuifunga bao 1-0, Dimba la Karume, mjini Musoma.

Ushindi wa michezo hiyo miwili mfululizo ugenini, umeifanya Yanga kuzidi kuikalia kooni Azam iliyopo kileleni katika msimamo wa ligi hiyo,  timu zote hizo zikiwa na pointi 22, Wanajangwani wakishuka dimbani mara nane dhidi ya tisa kwa wapinzani wao hao wenye maskani yao Chamazi, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo wao wa leo, Yanga wametamba kushinda na kuishusha Azam kileleni kwani watafikisha pointi 25, huku wakiwa wanalingana mechi na Wanalambalamba hao.

Ikumbukwe kuwa wakati Yanga wanaelekea Mwanza, walitamba kuzoa pointi zote tisa katika mechi zao tatu Kanda ya Ziwa, kwa sasa wakiwa wameshatwaa sita.

Kutokana na kiwango cha wachezaji wa Yanga walichokionesha katika michezo miwili iliyopita kwa kuwa na hamu ya kushinda, wapenzi wengi wa timu hiyo wanaamini watashinda leo.

Hata hivyo, mchezo huo unatarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana na Gwambina kuongozwa na Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi, Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Wanajangwani hao.

Gwambina inakutana na Yanga ikiwa imetoka kuchapwa mabao 3-0 nyumbani na KMC, hivyo itakuwa na hasira za kutaka kulipa kisasi.

Pia, mchezo huo utatoa picha ya Yanga kuelekea katika mechi na watani wao wa jadi, Simba unaotarajiwa kupigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Matarajio ya Wanayanga wengi ni kuona Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Cedric Kaze, anaiboresha safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikishindwa kutumia vizuri nafasi zinazotengenezwa.

Akizungumzia mchezo huo, Kaze alisema anaendelea kufanyia kazi mambo mbalimbali ndani ya kikosi chaka na kwamba lengo la kwanza wanaloingia nalo uwanjani ni kupata pointi tatu.

“Michezo ya ugenini ni migumu siku zote, ukipata alama tatu ni jambo kubwa, wachezaji wangu wamefanya kazi nzuri katika mechi zilizopita, tunaamini hata mchezo na Gwambina tutashinda,” alisema.

Alisema aliifuatilia Gwambina katika mechi zake chache, anajua ni aina gani ya soka wanalocheza lakini ataingia na mbinu tofauti kwa sababu muda wowote timu inabadilika.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kuwa kwa upande wao kama viongozi, wamejiimarisha kila idara kuhakikisha wanashinda leo na hata Jumamosi dhidi ya Simba.

“Kama viongozi, tumejiimarisha kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ya kuchukua pointi zote tisa Kanda ya Ziwa, hivyo tuwaombe mashabiki na wanachama wa Yanga kuendelea kutoa sapoti kwa uongozi na hata wachezaji ili tuweze kushinda mchezo wetu wa kesho (leo) na hata ule wa Jumamosi dhidi ya watani wetu wa jadi, Simba,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -