Wednesday, October 21, 2020

KUNDI LIPI NI GUMU AFCON 2017?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Makundi manne ya michuano ya fainali za Afcon mwaka huu yameshapangwa huku mashabiki wa soka wakishikwa na kigugumizi juu ya kundi gani gumu au la kifo miongoni mwa makundi hayo.

Mataifa 16 yamegawanywa katika kundi A-D huku kila kundi likiwa na timu nne zitakazochuana kuwania nafasi mbili za kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, ambayo imepangwa kuanza Januari 14 mwaka huu.

Kundi A, litakuwa na timu za Cameroon,  Burkina Faso, Guinea- Bissau na wenyeji Gabon, kwenye kundi hili ukiachilia mbali Cameroon ambao ni miamba wa soka Afrika, timu nyingine zinaweza kupigana vikumbo kuwania nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali. Wenyeji wanaweza kukabana koo vilivyo na timu yoyote, Burkina Faso nao wamekuwa si timu ya kubeza kabisa kwenye soka la Afrika kwa sasa.

Kundi B lina timu za Algeria, Tunisia, Senegal na Zimbabwe, wengi wanaidharau Zimbabwe kwenye kundi hili, lakini ukweli unabaki palepale kwamba Zimbabwe ya zamani ni tofauti na hii ya sasa, ilisheheni wachezaji wazuri wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya. Algeria watatamani kupata mafanikio zaidi ili kundelea kutawala soka la Afrika, lakini Tunisia wanahitaji kujenga upya heshima yao wakati Senegal nao wakitaka kuitingisha Afrika na dunia kwa mara nyingine.

Ivory Coast, DR Congo,  Morocco na Togo  zipo kwenye kundi C la michuano hiyo  japo Ivory Coast wanatajwa kuwa wakali kwa kuwa ni mabingwa watetezi, lakini DRC ni mabingwa wa CHAN huku Morocco na Togo zikiwa si timu za kubeza hata kidogo kwenye soka la Afrika.

Kundi D lina timu za Ghana, Mali, Egypt, Uganda, wengi hawaipi nafasi Uganda na wameacha nafasi kwa Ghana Misri na Mali, lakini Uganda imeonyesha si timu ya kubeza baada ya kutoka sare na Ghana kwenye makundi ya Kombe la Dunia. Kwa mtazamo wa harakaraka hili ndilo linaloonekana kuwa kundi la kifo kwenye michuano ya Afcon mwaka huu.

Lakini kwa kuwa soka la Afrika limebadilika sana, kundi lolote linaweza kuwa gumu kuliko ilivyotarajiwa. Timu ndogo zimeibuka na kufanya mambo makubwa kwenye soka la Afrika, vigogo wamekuwa wakiangushwa na mara kadhaa michuano hiyo imeshuhudiwa vigogogo wakitupwa nje ya michuano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -