Saturday, October 31, 2020

KUULI AITUNISHIA MISULI TFF

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

SIKU chache baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumpa siku tatu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli, kujieleza kwanini ameusimamisha uchaguzi wa Simba, Wakili huyo msomi ameibuka na kusema kuwa hakuna sheria inayomzuia kuzungumza na vyombo vya habari.

Katika barua iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, Kuuli alitakiwa kujieleza kama uamuzi wake huo wa kuusimamisha uchaguzi wa Simba SC umetokana na kikao cha Kamati yake cha Dodoma.

Akizungumza na BINGWA, Kuuli alisema nafasi yake ya Mwenyekiti anaruhusiwa kuzungumza chochote na vyombo vya habari, kwa kuwa kamati yake inahusu masuala ya kisheria ambayo hayaruhusiwi kuingiliwa na yeyote.

“Sijaipata hiyo barua yao na hata nikiipata nitaangalia kama inanilazimu kufanya hivyo, maana kuna vitu vingine ukiona havina maana unavitupa kwenye ‘dustbin’ tu.

“Sihitaji mabishano, watu wa mjini wanasema bifu mimi nimeshakuwa mtu mzima nina mambo mengi sana, ukipanda basi ukiona halifai unashuka tu.

“Namshangaa Katibu Mkuu, Wilfred Kidau, kuthubutu kuniandikia barua wakati Katiba haimruhusu kufanya hivyo.

“Yeye Katibu mimi ni Mwenyekiti, Katibu hata awe nani yeye anakuwa chini yangu, labda angesema kama kikao cha Kamati ya Utendaji kimemtuma kufanya hivyo,” alisema.

Alisema atakapoipata barua atajibu hoja zao kimaandishi, kama ataona kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Kuuli alitakiwa kujieleza kuanzia Septemba 19 mwaka huu, juu ya kuusimamisha uchaguzi wa klabu ya Simba SC uliopangwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.

Ikumbukwe, Septemba 17, mwaka huu, Kuuli alisitisha uchaguzi wa Simba kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za msingi.

Lakini siku mbili baadaye ikaripotiwa ameruhusu uchaguzi huo uendelee baada ya dosari zilizojitokeza kufanyiwa marekebisho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -