Monday, November 30, 2020

KWA AUBAMEYANG MAN CITY HAIMHITAJI AGUERO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

KUELEKEA dirisha dogo la usajili la Januari, tetesi ni nyingi zinzowahusisha wachezaji mbalimbali kuhama timu moja kwenda nyingine.

Hata hivyo, inayoonekana kuteka vichwa vya habari zaidi ni ile inayomhusisha mpachikaji mabao hatari wa Ligi Kuu nchini Ujerumani (Bunderlsliga), Pierre-Emerick Aubameyang, kutua England na kujiunga na Manchester City.

Inaelezwa kuwa, kichwa cha kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, hakijatulia hata kidogo na huenda akapumua ikiwa atafanikiwa kuinasa saini ya straika huyo wa kimataifa wa Gabon anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund.

Hata hivyo, si Guardiola pekee anayetolewa udenda na makali ya Mwafrika huyo, kwani amekuwa akiwindwa vikali na matajiri wa La Liga, Real Madrid.

Lakini, wachambuzi wengi wa soka wametabiri kuwa, kama Guardiola atafanikiwa kwenye vita hiyo, fowadi wake wa sasa, Sergio Aguero, atakuwa hana chake.

Hiyo ni kutokana na makali ya Aubameyang  linapokuja suala la kuwazidi akili mabeki wa timu pinzani na kuwatungua walinda mlango.

Lakini je, ni kweli Aubameyang atammaliza kabisa Aguero, ambaye amekuwa mtambo wa mabao wa Etihad kwa miaka mingi?

Mwanzoni mwa msimu huu, Man City walionekana kuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Katika siku za hivi karibuni, hasa baada ya kuchapwa mabaio 3-1 nas Chelsea, kikosi hicho kimeanza kuyumba.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kikosi hicho kilishangaza wengi baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Leicester.

Man Cit, ilicheza bila mastaa wake, Aguero na Fernandinho, ambao wanatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Imeelezwa kuwa, Guardiola hana mpango wa kuendelea kubaki na Aguero ifikapo Januari, licha ya uwezo mkubwa alionao katika kupasia nyavu.

Aubameyang anaongoza kwenye orodha ya mastraika wanaotajwa kutua Etihad kuvaa viatu vya Maurgentina huyo.

Wachambuzi wanaamini mkali huyo mwenye umri wa muiaka 27 ana sifa zote za kumrithi Aguero, hasa baada ya hivi karibuni kufikisha mabao 15 na kuwa kinara wa mabao katika orodha ya wafungaji wa ligi zote kubwa barani Ulaya.

Kwa Guardiola, kumpiga bei Aguero ni jambo linalowezekana kabisa, hasa ikizingatiwa kuwa huwa hababaishwi na wachezaji wenye majina makubwa.

Kwa vipindi tofauti, aliwahi kuwauza mastraika hatari, Samuel Eto’o, Zlatan Ibrahimovic, Mario Gomez na Mario Mandzukic.

Haina maana kuwa Aguero si mchezaji mzuri, ila ni ngumu kumfananisha na Aubameyang wa sasa.

Takwimu zinaonyesha kuwa, Aubameyang ni hatari zaidi mbele ya lango kuliko staa huyo wa zamani wa Atletico Madrid.

Aubameyang anapopata nafasi ya kufunga, huwa na asilimia 35 ya kukwamisha mpira kimiani.

Hiyo ni tofauti na Aguero, ambaye huwa na asilimia 16 pekee ya kufunga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -