Wednesday, October 28, 2020

KWA HALI ILIVYO HUU MJEZI WA AJIB INABIDI UFULIWE NA MAJI YA ULAYA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

DOMO LA MFUA JEZI

BASI iko hivi kama mlikuwa hamjui acha niwaambie, Shirikisho la Soka kule nchini Lesoto, wameanza kuhaha na kutafuta namna ya kumdhibiti Ibrahim Ajib, maana wameshapata taarifa kwamba atakuwepo kwenye kikosi cha Stars teh teh…….

Ajib amekuwa moto wa kuotea mbali kwa sasa katika Ligi Kuu Bara, huku akifunga mibao ya ajabu kwenye mechi za hivi karibuni na kuwashangaza watu.

Lakini hali imekuwa tofauti kwa wapinzani kule Lesoto, baada ya kusikia kwamba, nahodha wa Stazi, Mbwana Samatta ‘Samagol’, hatakuwepo kwenye mchezo dhidi yao lakini pia badala yake atakuwepo Ajib.

Ajib ambaye watu wanaendelea kulizungumzia lile bao kali la tiki taka alilofunga dhidi ya Mbao, lakini kiungo huyo mwishoni mwa wiki iliyopita aliifungia tena Yanga mgoli mkali huku akitoa asisti za mabao mawili.

Mgoli ule ulimfufua hata mzungu wa pale Msimbazi kwa majirani zao, huku akiwataka kuutumia kwa kulipia mishahara ya wachezaji wao na kuweka kambi za maana kutoka gesti hausi za vichochoroni mwe mwe mweee.

Kutokana na makali anayokuja nayo kiungo huyo na thamani yake kuzidi kupanda chati, mjezi wake sasa unafaa kufuliwa na mimaji ya Ulaya kwani si ya kawaida.

Bwana bwana bwana, watu sasa wanasubiri kwa hamu kuona mchezaji huyo akiitwa kwenye kikosi cha Stazi kinachotarajia kucheza mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Afcon dhidi ya Lesoto kati ya Novemba 16-18 mwaka huu.

Teh teh tehh….pengine tutashuhudia burudani na migoli mikali mingine kutoka kwake akiwa na kikosi cha Stazi iwapo kocha atamjumuisha nao.

Mjezi wa Ajib unaendelea kushika kasi ya ajabu mjini kwa sasa na kila nikiangalia namna ya kuufua naona maji ya Ulaya pekee ndiyo yanayofaa kuutakatisha.

Jamani jamani, Ajib amekuwa mcharo sana hivi sasa na kuwafanya mashabiki wa Wanajangwani kutuliza nyoyo zao kama hawana shida vile.

Zile kelele za kulia njaa mitaa ya Jangwani zinaonekana kusahaulika kwa sasa kutokana na matokeo mazuri wanayoendelea kupata timu yao.

Hata yule jamaa anayeongea zungu wa pale mitaa ya Msimbazi hana chakuwatania watani wake kwani kila akitafuta sababu ya kumwingia bwana Disman kumi, bado hapati.

Eti wajuzi wa mambo wanakwambia ndiyo kawaida yake bwana Migomba eti mkataba wake ukikaribia kueksipaya huwa anaonyesha kiwango cha juu ili tu kuwashawishi viongozi kutomwacha na pengine kujipandisha dau.

Lakini hilo tunamwachia mwenyewe, muhimu ni kwamba, anaisaidia timu kupata matokeo mazuri na kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.

Wakati mjezi wa Ajib ukiendelea kudiskasiwa na kila kona, nafikiria tena kuutafutia sabuni nzuri ule mjezi wa Klatusi Chama, maana ameanza kuzua zogo mjini.

Zahama zimemwangukia mchezaji huyo wa Simba, akifananishwa uwezo wake uwanjani na kiungo fundi wa kimataifa wa klabu hiyo, Haruna Niyonzima.

Lakini mjezi wake Chama utaendelea kusubiri foleni yake ifikie kwani kwa sasa mjezi uliojuu ni wa Ajib, inahitaji kufuliwa vizuri na kuuweka kwenye mazingira saafi kabisa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -