Friday, November 27, 2020

KWA HILI LA REFA, TFF MMEJITEKENYA NA KUCHEKA WENYEWE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

PENGINE yule aliyesema kirefu cha ‘TFF’ ni ‘Tanzania Football Fitna’ alikuwa na maana bora zaidi kama tungeamua kumsikiliza kabla ya kumpuuza.

Kuna mambo ya ajabu sana pale TFF.

Tazama hili, kuelekea mchezo wa Simba vs Yanga, shirikisho lenye dhamana ya mpira Tanzania limeficha jina la mwamuzi.

Pengine hii ni rekodi nyingine tumeiweka duniani, baada ya zile ‘Twitti’ za Mheshimiwa. Ngoja niendelee kufuatilia kwanza!

Kupitia kwa msemaji wa Shirikisho, Ndugu Alfred Lucas, TFF wanasema kuwa wamechukua uamuzi huo ili kukwepa hujuma, vitisho na vitendo vyote vya ajabu ambavyo klabu za Simba na Yanga zingeweza kuvifanya kwa mwamuzi huyo.

Hapa ndipo mkubwa anapojitekenya na kucheka mwenyewe!

Sawa, mmezificha Simba na Yanga, lakini ni kwa asilimia ngapi TFF ina usawa, uadilifu na usiri kwenye utendaji wao?

Timu zikiripotiwa kupanga matokeo, ni lazima usikie jina la ‘Ofisa wa TFF’ kuhusika, uchafu wowote wa soka nchini, ni lazima uhusishe kwa namna moja au nyingine watendaji wa shirikisho, leo wanatuaminishaje kwamba wamefanikiwa kutunza siri hii?

Asilimia kubwa ya watendaji wa TFF, aidha walishawahi kuwa viongozi wa Simba na Yanga, au wako kwenye kamati za klabu hizi mpaka leo.

Ni maagizo gani hayo waliyompatia mwamuzi ambayo hayajafika kwenye kambi za Simba na Yanga?

Wako baadhi ya watendaji wa TFF wako na Yanga Kimbiji na wengine wako Zanzibar na Simba, ni kwamba hawakuwa na jina la Mathew Akrama mpaka jana usiku?

Rais wa TFF alishawahi kuwa Katibu wa Yanga, Katibu wa TFF alishakuwa Katibu wa Yanga, hao wenyeviti wa kamati mpaka leo wana majukumu yao makubwa tu, kwenye klabu za Simba na Yanga.

Na si majukumu tu, ni wanaharakati wa kuzisaidia timu zao kupata ushindi, eti leo na wao ndio wameficha siri!!???

Ebo!! Kuna siri ya kidole na mfuko kweli???

Kilichofanyika ni ujinga wa kumficha swala kwenye boma la chui, tusidanganyane kwa vichekesho hivi visivyochekesha.

Tunapoanza kutengeneza mazingira ya kulicheza pambano hili tunapoketi ofisini, tusitegemee kuona ubora tunaoutegemea kwa nyota wetu.

Utaonaje ubora wa Msuva ikiwa tayari presha ya mechi ilishaanza kuwekwa kwenye kichwa cha mwamuzi?

Kwa kumficha Akrama kwa sababu zilizotolewa ni kumtengenezea mazingira ya kuitia hofu taaluma yake na weledi wa kazi yake.

Kuna mawili yanaweza kufanyika, huenda akawa na maamuzi bora zaidi kwenye historia ya pambano la Simba na Yanga au akaweka rekodi ya kuwa refa mwenye maamuzi mabovu zaidi.

Wala tusishangae na wala hatutakuwa na sababu ya kushangaa lolote yatakapotokea hayo, tumeyatengeneza wenyewe kwa akili zetu hivyo tujue namna ya kulidhibiti kwa nguvu zetu pia.

Neno langu kwa Akrama, nenda kasimamie weledi wa kazi yako. Nenda kazitafsiri vyema Sheria 17 za soka zinavyosema. Achana na hizi siasa za soka letu.

Ni mchezo huu uliobeba taswira ya nani atabeba taji msimu huu, ni pambano kubwa zaidi ya siri iliyotunza jina lako, nenda kawape mashabiki wanachokitegemea kutoka kwako!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -