Sunday, November 29, 2020

KWA MECHI ILE YA AZAM, YANGA…….SIMBA HAINA MPINZANI 2016

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA

UKIAMUA kusema Simba mabingwa wa msimu wa 2016/17, bila shaka utakuwa hujakosea sana hasa iwapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga pamoja na Azam FC wataendelea kuonyesha kiwango duni kama ilivyokuwa katika mchezo baina yao mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Dalili za ubingwa kuelekea kwa Wekundu wa Msimbazi hao zimezidi kujionyesha kutokana na soka bovu lililoonyeshwa na Yanga na Azam Jumapili iliyopita ambapo zilitoka suluhu.

Matokeo hayo yameifanya Simba kuendelea kujinafasi kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa, huku Yanga iliyoshuka dimbani mara nane ikiwa nafasi ya tatu na Azam ikiwa ya saba na pointi zake 12.

Katika mchezo baina ya Yanga na Azam, timu hizo zilishindwa kucheza kandanda la kuvutia kama ilivyokuwa ikitarajiwa hali ambayo ilileta maswali mengi kwa mashabiki hasa baada ya mtanange huo kumalizika.

Kasi ya timu hizo ni tofauti na ile ya msimu uliopita ambapo kila timu iliyokuwa ikipangwa kucheza nazo ilikuwa inajipanga kisawasawa lakini msimu huu wanaonekana kuchoka tofauti na Simba wenye kasi ya ajabu.

Katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, Yanga walionekana kuchoka hasa kipindi cha pili, huku Azam nao wakishindwa kutumia nafasi walizokuwa wakizipata.

Katika safu ya ulinzi, Kelvin Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’, angalau walionekana kuelewana, lakini Thaban Kamusoko na Juma Said Makapu kuna kipindi walikuwa wanapoteana na kumpa nafasi Abubakar Salum ‘Sure Boy’ na Himid Mao wa Azam FC kujinafasi.

Kwa upande wa mawinga, Simon Msuva, alianza vizuri kwa kasi kubwa lakini kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo alivyokuwa akianza kuporomoka na mara kadhaa akipiga krosi feki huku Deus Kaseke naye akishindwa kufanya kile alichotumwa.

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma ambaye amezoeleka kuwakimbiza mabeki wa timu pinzani, alipoteza ubora wake na kuonekana si chochote mbele ya akina Aggrey Morris.

Kwa upande wake, Obrey Chirwa, licha ya kwamba alijaribu kufurukuta bado mambo yalikuwa magumu mbele ya mabeki wa Azam FC, lakini hata hivyo alipata nafasi mbili za kupiga vichwa kutokana na krosi za Juma Abdul na kama angekuwa makini angalau angefunga hata bao moja.

Kama mipira hiyo miwili ya vichwa ingekuwa imemkuta Amissi Tambwe ambaye hakuwepo kutokana na majeraha, ni wazi angeweza kutumia vizuri nafasi moja.

Kwa ujumla, kiwango walichokionyesha Yanga hakikuwa vizuri na ilifika hatua wakaanza kubutua mipira kitu ambacho si kawaida yao.

Kwa upande wao Azam FC kitu kikubwa ambacho kama wasipokuwa makini kinaweza kikawagharimu ni kutokana na kucheza rafu nyingi hasa beki wao, Aggrey Morris, ambaye kwa sasa jina lake linatajwa vibaya mitaani.

Rafu mbaya aliyomchezea Abasirim Chidiebere wa Stand United, akakumbushia jinsi alivyomzimisha Emmanuel Okwi kipindi cha nyuma na katika mchezo wa juzi nusura amuumize Chirwa hivyo anatakiwa kujirekebisha mapema.

Mbali ya mapungufu hayo, lakini safu hiyo ya ulinzi ya Azam FC angalau ilijitahidi kuwazuia akina Ngoma na Chirwa na kama watamtumia vizuri Daniel Amoah, anaweza akawasaidia zaidi mbele ya safari.

Katika safu ya ushambuliaji ya Azam FC pengo la Kipre Tchetche linaonekana wazi kwani hakuna ambaye anaweza kumsaidia kwa ukaribu John Bocco na angalau kama Didier Kavumbagu angekuwepo huenda wangetengeneza kombinesheni nzuri.

Bocco alikuwa akifanya kazi kubwa lakini hakuwa na mtu wa kumsaidia hali iliyosababisha akina Yondani na Dante kuwa na kazi rahisi ya kuokoa hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni kwao.

Sehemu pekee ambayo haikuwa na maswali mengi ni upande wa kipa ambapo Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Aishi Manula wa Azam FC, waliendelea kuonyesha uwezo kama kawaida yao huku wakiondosha hatari nyingi.

Kutokana na mapungufu waliyoyaonyesha Yanga na Azam, ni wazi wasipojiangalia wataiona Simba ikitwaa ubingwa mchana kweupe kutokana na kasi waliyonayo wakiwa hawajapoteza mchezo wowote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -