Friday, October 30, 2020

KWA NYONI NA WAWA… SIMBA WATAOKOTA SANA MIPIRA WAVUNI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

 

NA AYOUB HINJO


 

TANGU klabu ya Simba irejee kutoka nchini Uturuki walikoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya, wamekuwa gumzo kubwa kwa wadau wa soka.

Msimu uliopita walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukaa takribani misimu mitano bila taji hilo.

Kurejea kwao kumefanya kila mmoja achukue muda kuona ni kitu kipi kipya wamerudi nacho kutoka huko, tena wakiwa na kocha mpya, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji.

Kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza Septemba 22, Simba wamecheza michezo minne, wameshinda miwili na kutoa sare miwili, huku wakivutia zaidi kwa aina ya soka lao la pasi kuanzia nyuma.

Walianza kwa kutoa sare ya 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana, kisha walisafiri hadi mkoani Lindi kucheza na Namungo FC ambako walitoa suluhu.

Ushindi wa kwanza wa mabao 2-1 waliupata dhidi ya Arusha ya United katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kisha kundeleza dozi ya mabao 2-1 kwa Mtibwa Sugar, mchezo wa Ngao ya Jamii iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika michezo hiyo minne klabu hiyo imefanikiwa kufunga mabao matano na kuruhusu kuokota mipira mitatu kwenye nyavu zao.

Tangu katika mchezo wa Simba Day dhidi ya Asante Kotoko, mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara walionekana kukosa uwiano mzuri katika safu ya ulinzi.

Haikuwa na haja ya kupepesa macho juu ya hilo hasa pindi timu ya Simba ilipokuwa ikishambuliwa na Asante Kotoko ambao walionekana kuwa na watu hatari katika eneo la mwisho la tatu ‘final third’.

Mara kadhaa walinzi wa Simba walizidiwa maarifa na washambuliaji, lakini kubwa zaidi kasi yao kubwa ilikuwa sumu kwa mabeki hao walioongozwa na Erasto Nyoni na Paschal Wawa.

Huku kwa pande za pembeni wakiwa na Asante Kwasi na Nicolas Gyan aliyechukua nafasi ya Shomari Kapombe baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Asante Kotoko walikuwa na kasi kubwa pindi walipovuka kutoka eneo lao, walitumia pembeni kutengeneza mashambulizi yao kuelekea katika lango la Simba.

Nyoni na Wawa  ni mabeki mahiri sana lakini hawana kasi kubwa, mara kadhaa walikuwa wakikimbiza kivuli cha wapinzani wao na kupelekea kufungwa bao kwa makosa ya Nyoni baada ya kuzidiwa nguvu na mmoja wa wapinzani wake.

Kama wapinzani wa Simba waliuangalia mchezo huo naamini watajipanga zaidi kucheza dhidi ya mabeki hao kwa kuangalia udhaifu huo na kuiadhibu timu hiyo.

Mabeki hao wenye uzoefu mkubwa wamecheza pamoja katika michezo mitatu ambayo yote Simba waliokota mipira kwenye nyavu zao.

Kwa umakini zaidi ukiangalia utagundua kuwa licha ya uzoefu walionao bado kasi ya wapinzani imekuwa tatizo kubwa kwao, dhidi ya Asante Kotoko na Arusha United katika michezo ya kirafiki na ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Matibwa Sugar.

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliwahi kusema kuwa washambuliaji wanakufanya ushinde mchezo lakini mabeki wanakufanya ushinde ubingwa.

Msimu uliopita Simba waliruhusu kufungwa mabao 15 katika michezo 30 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, walikuwa na wastani mzuri lakini kwa hiki kilichotokea kwenye maandalizi ya msimu mpya wanaweza kujikuta katika wakati mgumu kwa wapinzani kutumia udhaifu huo.

Pia, msimu uliopita walitumia mfumo wa 3-5-2, uliowawezesha kutumia walinzi watatu huku Yusuph Mlipili akiwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo kwa kucheza vizuri naamini huu ulikuwa msimu wa muendelezo wa kile alichokianza msimu uliopita licha ya uwepo wa kocha mpya.

Nyoni na Wawa wanaonekana kutoendana kwa kiasi fulani, hivyo Simba watumie udhaifu wao licha ya kuwa mabeki wazuri kutoa nafasi kwa akina Mlipili na Paul Bukaba ambao walifanya vizuri mzimu uliopita.

Msimu uliopita Nyoni alicheza sana na Mlipili aliyeonekana kufuata maelekezo vizuri kutoka kwa mkongwe huyo, hata Bukaba alicheza vizuri alipokuwa na Wawa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki, Cecafa Kagame.

Kwa muda mfupi wanaonekana kama mwili wa baunsa, wakiwa na safu kali ya kiungo na ushambuliaji huku wakiwa na udhaifu katika idara ya ulinzi.

Ni mapema kuweza kuwatabiria kama watafanya vibaya lakini kwa dalili hizi zilizoonekana mapema wanao muda wa kurekebisha makosa yaliyotokea katika kikosi chao kabla ya wapinzani kuutumia udhaifu huo kama faida kwao.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -