Tuesday, November 24, 2020

KWA REKODI HIZI TAMBWE ANAKUACHAJE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

HAKUNA ubishi kuwa Amissi Tambwe anajua kufunga! Kama unabisha tafuta rekodi zake za kucheka na nyavu tangu atue nchini akitokea kwao Burundi, lazima utakubali tu. Jamaa ameweka rekodi ya ufungaji bora katika misimu tofauti akiwa na Simba na Yanga.

Tambwe amekuwa mfano bora zaidi kwa wachezaji wa kulipwa kwa jinsi alivyo stadi, fundi, mtulivu mbele ya lango. Ufuatiliaji wake wa ‘move’ za mchezo, uwezo wake wa kujipanga kutumia nafasi na mambo mengine kumemfanya kuwa mmoja wa washambuliaji tishio sana hapa nchini.

Katika mechi ya Watani wa Jadi, Simba na Yanga keshokutwa, Tambwe anazungumzwa sana, ndiye aliyeleta zahama katika mechi iliyopita kutokana na bao lake, lakini si hilo tu gumzo kubwa ni jinsi anavyoifunga Simba mara kwa mara tangu alipoihama.

Mechi hiyo ambayo joto lake kwa sasa limepanda kwa wale wapenzi wa Simba na Yanga, haiwezi kuzungumziwa kama hajatajwa Tambwe, pande zote mbili wanamtaja mshambuliaji huyu raia wa Burundi kwa namna tofauti.

Anatajwa kwa sababu amekuwa mchezaji wa pekee mwenye rekodi ya aina yake katika pambano la timu hizi mbili, ameshafunga mabao matano katika mipambano saba ya mahasimu hao wa kandanda Tanzania tangu yeye alipotua nchini.

Ni rekodi ya aina yake ambayo sasa imemfanya kusimama na Watanzania, Emmanuel Gabriel na Jerryson Tegete ambao pia wamefunga mara tano katika ‘derby’ hiyo yenye kuvutia wapenzi wengi wa kandanda Tanzania na Afrika Mashariki.

Wakati Gabriel alifunga mabao yote Yanga na Tegete akifanya hivyo kwa kuifunga Simba, Tambwe amefunga kila upande na kuna washambuliaji wengi waliopita katika timu zote lakini tangu mwaka 1935, hakuna aliyeweza kufanya kama alichokifanya Tambwe katika mechi ya watani wa jadi.

Tambwe ni kiboko katika mabao hayo, aliifunga Yanga mara mbili wakati alipokuwa mchezaji wa Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 2013 katika ushindi wa mabao 3-1.

Mtaalamu huyo wa mabao ya kichwa, akaifunga Simba mara mbili katika mechi za VPL akiwa na kikosi cha Yanga msimu wa 2014/15 (Yanga 2-Simba 0) Oktoba 2015, Febuari 2016 (Simba 0-Yanga 2) na mechi ya Oktoba mosi 2016 alipofunga bao lake la tatu kwenye mechi iliyomalizika kwa sare ya bao (1-1).

Tambwe utamchukia wewe, lakini sifa yake itapendwa na wapenzi wengi wa kandanda nchini hasa wale wanaovaa jezi za rangi ya kijani na njano kwa sasa, huku wale wa Msimbazi wakimchukia kutokana na rekodi zake alizonazo kwa sasa.

Huyu ndiye ‘Mr Hat-trick’ ambaye aliweka rekodi ya kufunga hat-trick nyingi kwenye ligi kuu tangu ajiunge kuliko mshambuliaji yoyote wa kigeni aliyesajiliwa hapa nchini.

Mechi ya kwanza kufunga hat-trick ilikuwa ni Febuari mosi mwaka 2014 dhidi ya JKT Oljoro akiwa na Simba ambayo ilishinda 4-0. Mechi ya pili ni Septemba mwaka 2014 wakati Simba ikimenyana na Mgambo JKT na Wekundu wa Msimbazi kuibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Mechi ya mwaka 2015 akiwa na Yanga, Tambwe alipiga hat-trick wakati timu yake ikicheza na Coastal Union na kushinda mabao 8-0, pambano lilopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ambapo idadi kubwa ya mabao amefunga kwa kichwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga.

Msimu wa 2015/16, alipiga hat-trick wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Taifa. Alifanya hivyo tena kwenye mchezo kati ya Yanga na Stand United na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye Uwanja huo wa Taifa katika msimu huo.

Lakini Tambwe pia anatambulika kwa ubora kutokana na kufanikiwa kuwa mfungaji bora msimu wa 2015/16, baada ya kufunga mabao 21 akifuatiwa na Hamis Kiiza ambaye alifunga mabao 19. Wakati akiwa na Msimbazi katika msimu wa 2013/14, aliibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 19.

Yote tisa, Tambwe pia amewahi kutwaa kiatu cha dhahabu akiwa kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Sudan kwa kufunga mabao saba yalioisaidia Vital O kutwaa ubingwa kipindi hicho.

Kwa rekodi hizo, je, Tambwe ataweza kupeleka shangwe Jangwani keshokutwa? Mechi inayosubiriwa kwa hamu na wadau wengi nchini huku ikitarajiwa kuwa na maamuzi ya nani atakuwa bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -