Monday, October 26, 2020

Kwa tabia hii ni kwanini ufurahie mapenzi?

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

KILA anayekwambia nakupenda unamwona wa maana. Kwa sauti yake na kwa fedha zake tu, inatosha kukufanya uamini kuwa ni  kweli anakufaa katika maisha yako. Kwa namna hii, ni kwa namna gani utaona mapenzi kwako mazuri?

Kila anayekwambia u-mzuri na kusema anakuhitaji katika maisha yake unaona umepata bahati. Siku ya pili unamwita mpenzi, anakuita baby, eti tayari mnajipanga kuishi pamoja siku moja. Haya ni mapenzi ya namna gani?

Mapenzi si suala jepesi kama unavyoweza kujidanganya. Unahitajika kuwa makini na mwenye kutuliza akili ili uwe salama katika mapenzi.

Ni kweli anakwambia anakupenda. Kila siku anakupa zawadi na kukuahidi kukufanyia mengi na ya msingi, ila mapenzi si suala la namna hii. Ni suala muhimu linalokuhitaji utulize akili ili uweze kumtambua ni nani wa dhati na nani anajifanya kuwa.

Matapeli wa mapenzi ni wengi. Wengi wapo radhi kukuambia kila neno zuri unalotamani kuambiwa. Wapo tayari kukupa kila zawadi hata za kukopa ili waweze kukuteka kiakili.

Baadhi hawaoni shida kuapa na kujiaminisha kwako kitapeli ili waweze kukupata. Bila kuwa makini kila siku utajikuta ukiangukia katika mikono yao na kuumia. Katika dhana ya mapenzi halisi umakini ni suala unalopaswa kuliweka akilini.

Japo anakwambia anakupenda na hata kuonesha kama anakujali. Suala si kuingia kichwa kichwa. Simba mwenda pole ndiyo hupata windo lake. Jipe muda wa kumsoma vizuri, kuwa makini katika maneno yake, jitahidi kadiri inavyowezekana kuyasoma matendo yake kwa upana na maana inayofaa.

Wapo wanaoweza kuigiza na kufanana na wale wa kweli, sasa kama hauko makini na mjanja unaweza kuamini umepata kumbe umepatikana.

Ingawa anakuonesha kuwa wewe ni mtu wa kipekee katika maisha yake, suala si kusema ndiyo, panga mipango ya kumwona katika maana halisi. Chunguza kauli zake na pima matendo yake. Je, ni kweli anamaanisha au anataka kuingia katika maisha yako na kutimiza tu lengo lake? Kuwa makini sana.

Katika hali ya kumchunguza kiufasaha unaweza kuwa naye karibu. Ukaribu huu uwe tofauti na ule wa mapenzi. Dhumuni la kufanya hivi ni katika kuweza kumwona kwa ukaribu na kujaribu kupima matendo na kauli zake katika mizani ya ukweli. Ukaribu huu usikufanye uamini eti tayari umekuwa wake. Hapana!

Hapa ni katika uchunguzi ila ni vyema yeye ukamwaminisha kuwa tayari umekuwa wake katika namna fulani. Maana ya kufanya hivi ni kuona upande wake wa pili.

Wengi wa matapeli wanaotongoza kwa lengo au nia fulani hujisahau baada ya kuona wameingia na kina fulani katika uhusiano. Hapa hutaka sana ngono au hujionesha namna walivyo watawala katika maisha ya wahusika.

Ukiwa makini hapa unaweza kumsoma mwenzako vizuri na kuona nia yake halisi ya kuja kwako. Unahitajika kuwa makini ili usiweze kuingia katika mfereji wa mateso na manyanyaso.

Acha kumwangalia na kuhukumu kwa namna anavyoonekana. Wengi wako tayari kuwa katika aina fulani ya tabia kwa ajili ya maazimio yao fulani. Ukiacha kuwa makini na mjanja unaweza kuzama.

Katika kila hatua unayoenda naye jaribu kumsoma kwa makini. Jionye usije ukatekwa na maneno na matendo yake na kujisahau, matokeo yake akatimiza lengo lake. Matapeli wa mapenzi wako wengi sana.

Wengi wamekutana nao na wameachiwa maumivu yasiomithilika. Kila siku wanalia na mapenzi. Kila mtu wanamwona mbaya na wengine wamefikia hata kuyaona mapenzi yenyewe kama hayana maana. Kama usipokuwa mjanja na makini unaweza kujikuta na wewe katika aina hiyo ya maisha.

Suala ni kujitambua na kuwatambua kisha kukaa nao mbali. Si kila anayekwambia anakupenda anamaanisha. Neno hili huwa mtego wa kukuweka katika himaya yao. Kuwa makini!

Ni kweli anasifa za mtu unayemtaka. Anaweza kuwa na kila kitu unachotaka mwanamke au mwanaume wako awe nacho, ila kabla hujaamua aingie katika maisha yako unahitajika kumsoma vizuri na kumwelewa mapema.

Wengi ni matapeli! Wanakuwa wema mwanzo na mwisho  wanabadilika kabisa. Bila kuwa makini, mbunifu katika kuwasoma huwezi kuwatambua kirahisi.

Usisukumwe kirahisi na hisia ukawa naye. Jionye na ruhusu akili yako izipe subira hisia zako. Bila subira, umakini, utajikuta unalia. Usibabaike na mwonekano wake wala na kipato chake; katika mapenzi suala muhimu ni furaha na amani. Ukimbabaikia bila kuwa makini, mbali na mali au mwonekano wake atakuacha na majonzi na ukajikuta unalaumu mapenzi bure. Siku njema!

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -