Monday, November 30, 2020

KWA VIGEZO HIVI SANCHEZ ATUE CHELSEA, MSN WATAZIMA SIGARA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

Alexis Sanchez anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Arsenal mwishoni mwa amsimu huu na wakati anasubiri kuongeza mkataba, klabu mbalimbali za wapinzani zitakuwa zikipigana vikumbo ili kumnasua kutoka Emirates.

Juventus, Paris Saint-Germain, Sevilla na klabu za China (Chinese Super League) wamekuwa wakihusishwa na Sanchez katika wiki kadhaa, wakati Chelsea wanafuatilia kwa karibu kujua hatima ya mchezaji huyo na timu yake ya Arsenal.

Mtandao wa ESPN umejaribu kuorodhesha sababu tano kwanini Sanchez atafiti kuichezea Chelsea.

  1. Anacheza soka la Conte

Chelsea wamefunga mabao 45 kwenye mechi 20 za Ligi kuu England tangu kocha wao, Antonio Conte aamue kubadilisha mfumo na kucheza 3-4-3 mwishoni mwa Septemba mwaka jana, akizipasua safu za ulinzi za timu pinzani kwa kasi, wakiteleza kwa pasi za kufungia uwanja na soka la kushambulia moja kwa moja.

Sanchez anashika nafasi ya sita kwa wachezaji wa Ligi Kuu England hatari kwa kukokota mipira. Kwa mechi moja ana wastani wa (2.9) na pasi muhimu ana wastani wa (2.5). Kiu yake ya kucheza soka la kushambulia imemfanya afanikiwe kupachika mabao 17 na kupika nane katika mechi 25 za Ligi Kuu England, uwezo wake wa kujituma kila mechi utamfanya awe mchezaji muhimu kwa Conte.

  1. Anaweza kucheza nafasi yoyote kwenye safu ya ushambuliaji Chelsea

Kwa miaka yake miwili ya kwanza akiwa Arsenal, Sanchez alikuwa akicheza kwenye nafasi moja ambayo anacheza Eden Hazard ndani ya Chelsea, akiingia golini kutokea upande wa kushoto wakati wa kushambulia. Msimu huu, nyota huyo wa Chile amewatesa mabeki Ligi Kuu England, akicheza kama namba tisa bandia.

Hembu jaribu kufikiria Sanchez awe mmoja wa mawinga wawili wa Chelsea wakicheza na Diego Costa kwa mfumo wa 3-4-3 wa Chelsea, pia ameonyesha kwa miezi kadhaa sasa kwamba anaweza kuwa mchezaji muhimu kama Costa akikosekana kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

  1. Ni zaidi ya Pedro

Pedro amekuwa kwenye kiwango cha juu msimu huu na kuifanya Chelsea kuwa kwenye kiwango kingine cha ushambuliaji tangu Oktoba, mwaka jana.

Nyota huyo wa Hispania amefunga mabao saba na kupika sita Ligi Kuu England, huku uwezo wake wa kukimbia na mpira ukichanganya na kipaji cha Hazard na Costa.

Kwa ubora alionao Pedro, halafu umchezeshe na Sanchez na wachezaji wengine wazuri, kutaifanya Chelsea kuwa hatari zaidi ya washambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar (MSN). Kama dili la  Sanchez kutua Chelsea litatokea na akafanikiwa kujiunga na klabu hiyo, basi itakuwa hatari. Kwa sasa Sanchez amefunga jumla ya mabao 20.

  1. Anachukia kupoteza kama Conte

Kama Conte alivyosema mara kadhaa msimu huu kwamba anasumbuliwa na vipigo alivyochapwa nyuma katika mechi za Ligi Kuu England, ambapo wiki iliyopita aliweka wazi kwamba hakuweza kulala siku sita baada ya timu aliyokuwa akiiongoza kama nahodha, Juventus kupoteza taji kwa Lazio dakika za majeruhi baada ya kuwazidi kwa tofauti ya pointi sita, ambapo zilikuwa zimebakia mechi saba kama msimu wa Serie A wa 1999-00 kumalizika.

Ukiangalia mwonekano wa Sanchez uwanjani, iko wazi kwamba kufungwa kwa Arsenal mara kwa mara kunamwathiri sana, tofauti na ilivyo kwa wachezaji wenzake. Kuchukia kwake kufungwa kunaweza kukawa chanzo cha kuondoka Gunners mwisho wa msimu huu, hilo pia ndilo jambo linalomfanya Conte ampende.

  1. Si wa kubahatisha

Wachezaji wengi wanaofukuziwa na Chelsea kwa ajili ya dirisha kubwa la usajili ni akina Alvaro Morata, Moussa Dembele, Andrea Belotti, wachezaji ambao huna uhakika nao kama watakuja kucheza vizuri Ligi Kuu England.

Sanchez si wa kubahatisha. Mwisho wa msimu huu atakuwa ni mmoja wa washambuliaji bora Ligi Kuu England. Kama Chelsea watafanikiwa kumnasa, wanajua kile watakachokipata.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -