Thursday, December 3, 2020

KWAHERI HAYATOU LAKINI UTAKUMBUKWA KWA HAYA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ADDIS ABABA, Ethiopia

HATIMAYE baada ya kipindi cha miaka  29, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeingia katika utawala mpya baada ya kiongozi wake wa muda mrefu, Issa Hayatou, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka  la Cameroon, kuangushwa na mwenzake kutoka  Madagascar (FA),  Ahmad Ahmad katika  Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Katika uchaguzi huo, Ahmad, mwenye umri wa miaka 57, ambaye ameliongoza Shirikisho la Soka la Madagascar tangu mwaka 2003, alipata kura 34 kati ya 54  zilizopigwa na wakuu wa mashirikisho na vyama wanachama wa umoja huo.

Kushindwa kwa Hayatou, ambaye alikuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika, kunaonekana kuwashtua wapenda soka wengi na kuna wanaoonekana kuwa huenda soka katika bara hili likarudi nyuma.

Wasiwasi huo kwa wapenda maendeleo ya soka huenda unatokana na mchango mkubwa ambao kigogo huyo amekuwa akiutoa katika kuhakikisha soka la Afrika linasonga mbele.

Katika Makala haya, BINGWA imejaribu kuangalia mambo kadha wa kadha ambayo rais huyo wa zamani aliyafanya katika kipindi cha miaka 29 ambayo anaendelea kukumbukwa pamoja na misukosuko ambayo alikumbana nayo.

 *Ya kukumbukwa

Kabla ya kushindwa juzi, Hayatou, mwenye umri wa miaka 70, ni mara mbili tu alipopata upinzani na mara zote hizo alishinda kwa kishindo.

Akiwa madarakani tangu mwaka 1988, Hayatou aliweza kuleta ushawishi mkubwa wa  kisiasa katika soka la kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuchukua nafasi katika Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA, ambayo  sasa itabidi kuondoka  baada ya kushindwa.

*Alivyoipaisha CAF

Akiwa rais wa CAF kwa zaidi ya miongo hiyo miwili, Hayatou  alipata mafanikio katika fainali za Kombe la Dunia kwa nchi za Senegal, Nigeria na Cameroon kufanya vizuri na huku akiongeza msukumo kwa bara hili kuongezwa nchi kutoka mbili hadi tano na huku akiiwezesha Afrika kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2010 likiwa na timu sita, ambapo mwenyeji Afrika Kusini aliingia moja kwa moja kama mwandaaji.

Katika kuhakikisha michuano hiyo inafanyika Afrika, Hayatou alikuwa mstari wa mbele katika mchakato mzima wa kuwania nafasi hiyo pamoja na kushiriki katika Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza Afrika mwaka huo wa 2010.

Mbali  na Kombe la Dunia, kiongozi huyo ndiye aliyefanikisha kuongezwa timu zinazoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kutoka nane hadi 16 kutoka katika mataifa  50 yaliyopo katika kanda na mashirikisho matano.

Mbali na Mataifa ya Afrika, kigogo huyo pia ndiye aliyeleta mabadiliko kwa klabu ambapo kumekuwapo na idadi kubwa zinazoshiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Shirikisho ambayo ilianza mwaka  2004 kwa timu ambazo ni washindi katika mataifa yao, Kombe la  CAF na  CAF Super Cup kama ilivyo kwa nchi za Ulaya.

Vilevile katika utawala wake, Hayatou ndiye aliyeondoa utamaduni wa kuangalia soka la wanaume tu ambapo  CAF ilianzisha mashindano ya timu za vijana, wanawake, soka  la kuchezea kwenye sakafu (Fustal) na la ufukweni

*Uhusiano wake na UEFA, FIFA

Moja ya malengo makuu ya urais wa Hayatou katika miaka ya 1990 lilikuwa ni kutoa motisha kwa klabu za  soka Afrika ambayo itaweza  kuzuia upatikanaji wa wachezaji wa Afrika kwenda Ulaya; mpango ambao  hata hivyo alikutana na mafanikio kidogo.

Katika mpango huo, Hayatou alikuwa akilalama kuona rasilimali ya soka inarejeshwa katika mfumo wa kikoloni,  akisema kuwa: “nchi tajiri  zimekuwa zikiagiza malighafi ya vipaji na kisha kuwatumia kwa ujira mdogo na huku zikileta wataalamu wenye ujuzi duni ili waweze kuajiriwa kwa bei kubwa katika mataifa ya  Afrika.”

Kutokana na msimamo huo, Septemba, 1997 ndipo ikashuhudiwa yanakuwapo majadiliano kati ya Hayatou  na UEFA kuhusu ada za uhamisho kwa wachezaji kutoka Afrika, zitakazokuwa zikilipwa katika bodi hiyo ya soka Afrika na klabu zitakazouza wachezaji wazaliwa wa bara hili.

Majadiliano hayo ndiyo yalisaidia kusainiwa kwa mradi wa Meridian Project, Desemba  1997, baina ya CAF  na  UEFA, ambao uliwezesha vyama vya soka Afrika kuwa vinapewa fedha kila mwaka na huku yakianzishwa mashindano yaliyopewa jina la  UEFA-CAF Meridian Cup.

Katika mradi mwingine wa 1999 Goal Project  ulioanzishwa na FIFA, uliyawezesha mashirikisho ya soka 46 ya Afrika kupata msaada wa takribani dola milioni moja kwa zaidi ya miaka minne.

Katika mazungumzo hayo, bila kujali athari zake kwa klabu za soka Afrika, kughushi na uhusiano wa karibu kati ya viongozi wa UEFA na Hayatou, ndicho kilichowezesha  kuungwa mkono na UEFA katika  uteuzi wa Hayatou wa kuchukua nafasi ya Sepp Blatter kuwa kiongozi wa FIFA mwaka 2002.

Hata hivyo, Blatter, ambaye alikuwa akiungwa mkono na mashirikisho ya soka kutoka Amerika na Asia, aliweza kumshinda  Hayatou kwa kura 139 dhidi ya 56 alizozipata kiongozi huyo.

*Kashifa ya rushwa

Pamoja na  kupigania soka la  Afrika kama ilivyo kwa viongozi wengi kukumbwa na kashifa, Novemba  2010  mwandishi wa habari za uchunguzi  nchini Uingereza, Andrew Jennings, alifichua siri ya uchafu ambao ulikuwa ndani ya  FIFA, akidai kuwa,  Hayatou katika kipindi cha miaka  1990 alikula rushwa katika utoaji wa mikataba kwa vituo vya televisheni  ya kuuza hati miliki ya kurusha matangazo ya michuano ya fainali za Kombe la Dunia.

Kupitia katika kipindi hicho cha Panorama kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mwandishi huyo alieleza kunasa nyaraka kutoka katika kampuni inayoitwa ISL zinazoonesha kwamba,  Hayatou  alilipwa faranga  za Ufaransa  100,000 na kampuni hiyo ambayo ilipata hatimiliki hiyo.

Hata hivyo, Hayatou alikana shutuma hizo, akisema kuwa, fedha hizo hazikwenda mfukoni mwake, bali ziliingia CAF.

Mbali na kashifa hiyo Mei,  2011, gazeti la  Sunday Times liliandika kuwa  Hayatou na mjumbe mwenzake wa muda mrefu katika Kamati Kuu ya FIFA,  Jacques Anouma, walikuwa mlungula wa dola milioni 1.5  kutoka  Qatar  ili waweze kuiunga mkono ipate nafasi ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia  2022.

*2010 kufungiwa Togo

Ikiwa ni siku moja kabla ya kumalizika fainali za Mataifa ya Afrika 2010, zilizofanyika nchini Angola, akiwa kiongozi wa CAF, alitangaza kuifungia nchi ya Togo kushiriki katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa kipindi cha miaka miwili, kwa kile alichodai ni kutofurahishwa na hatua ya serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka baada ya Waziri wa Michezo, Gilbert Huongbo, kuamua timu hiyo ijitoe kwenye mashindano hayo.

Hatua ya waziri huyo ilikuja baada ya timu ya taifa kushambuliwa na kundi la waasi katika Jimbo la Cabinda, wakati ikiwa njiani kwenda Angola kwa ajili ya fainali hizo ambapo watu wawili walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Kutokana na uamuzi huo, nahodha wa Togo, Emmanuel Adebayor na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hubert Velud, waliushutumu vikali uamuzi huo wa  Hayatou na CAF, huku wakimtaka ajiuzulu.

*Utata uteuzi wake OIC

Septemba  21, 2011, ni siku ambayo FIFA ilimtangaza  Hayatou  kuwa Rais wa Kamati  ya Olimpiki katika shirikisho hilo na huku ikiidhinisha wadhifa wake wa kuwa Mwenyekiti wa mradi wa  Goal Bureau.

Baada ya kukabidhwa wadhifa huo wa Kamati ya Olimpiki, Hayatou  aliutumikia kuanzia mwaka 1992 hadi 2006 na huku kipindi hicho akiwa chini ya uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa.

Hata hivyo, baadaye FIFA ilikana kumteua  Hayatou kuwa rais wa kamati hiyo ya Olimpiki kwa kile ilichodai uteuzi huo yalikuwa ni makosa ya kiufundi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -