Sunday, January 17, 2021

KWANINI AMEBADILIKA, JIULIZE KUANZIA HAPA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

ALIKUWA anapenda kuzungumzia kuhusiana na ndoa, ila sasa hataki hata kuligusia. Sasa ukilizungumzia yeye anakuwa msikilizaji zaidi badala ya mchangaji kama ilivyokuwa awali.

Kwa siku ulikuwa unawasiliana naye zaidi ya mara tatu, ila sasa kupita wiki bila mawasiliano inaanza kuwa kawaida.

Ukikutana naye si yule wa zamani. Lile tabasamu na maneno matamu yamepita kama muda ulivyopita. Ukitaka mwende ufukweni kama ulivyozoea, hayuko tayari tena. Yuko radhi akupe pesa uende na marafiki zako ila yeye abaki nyumbani. Kila ukimtafakari unagundua sura na umbile tu ndiyo yako vile vile, ila tabia na mwenendo wake uko tofauti na yule uliyemzoea.

Ukijaribu kuumuliza hajibu kama zamani.  Wakati zamani alikuwa akikujibu kwa bashasha na shauku, siku hizi ni kama anaringa hivi. Ni kama hajisikii hivi! Hapa kuna tatizo. Unaongea kwa maneno marefu yenye kila ashirio la mapenzi na kumhitaji, yeye anajibu kifupi. Kwa maneno ya hovyo yasiyo na raha ila karaha na visa. Kila ukijiuliza nini tatizo, hupati jibu. Kila ukimuuliza anakwambia hamna kitu. Unajikuta njia panda.

Katika mabadiliko haya kuna kitu kimefanyika, kinafanyika au kinataka kufanyika. Ukituliza akili na kujiuliza maswali kadhaa utajua kwanini amekuwa hivi.

Mtu aliyekuwa anakutafuta karibu kila siku iweje sasa imekuwa mpaka umtafute wewe tu. Ukikaa kimya na yeye kimya, hata mwezi. Hapa kuna namna. Jaribu kuwa makini na matendo yake. Huenda ikawa hutakiwi kuamini kuwa ni mpenzi wako tena, maana kwanini baada ya mwezi jana kukubali kumvulia nguo awe ‘busy’ hivi?

Hapo kabla alikuwa karibu kila muda anakuita baby, ila sasa ukituma ‘meseji’ anakwambia nitakucheki baadaye, na asifanye hivyo. Kwanini? Kwanini mabadiliko haya hayakufanyika kabla hujafanya tendo lile? Huenda atakuwa alikuchukulia wewe ni wa muda tu. Kuwa makini.

Katika akili ya kawaida haiwezekani mtu aliyekuwa anakesha akiongea  na wewe, leo awe wa kutokupigia simu wiki nzima.

Ndiyo, kunaweza kuwa na sababu nyingine, ila zitafute sasa. Maana wakati mwingine unaweza kuwa ni wewe umekuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia yake. Kila siku ni yeye wa kukutafuta, kila muda unataka wewe ndiyo uambiwe umekumbukwa. Labda mwenzako kachoka.

Hupaswi kulalamika kwanini kabadilika ikiwa hutaki kuchunguza ni wapi umekosea ama ni kwanini amekuwa hivyo. Watu wengine zao ni kuwa na mpenzi karibu kila mwezi, sasa kama hakupigii jua mkataba wenu uliisha siku ile pale ‘Gesti’.

Kabla hujaanza kufikiria tofauti juu ya mabadiliko yake, tafakari mangapi mazuri alikuwa akifanya kwako, halafu pima ulikuwa ukiyalipa vipi. Wengine kila siku wanafanyiwa wao mazuri na bado viburi wanakuwa wao. Wanapigiwa simu wao, na bado wao ndio wakujibu vibaya. Sasa kwanini unashangaa haya mabadiliko? Wakati mwingine vyanzo vya mabadiliko huwa vitatu.

Matendo yako kwake, dhamira yake kwako pamoja na mazingira yanayomzunguka. Kama mwenzako anakuwa mwema kwako halafu unamlipa ufedhuli na dharau, usishangae kubadilika.

Kila siku anakwambia tabia fulani hapendi, we ndio kwanza unazidisha. Sasa hapa unategemea kwa vipi aendelee kugusia suala la ndoa? Kama wewe umeamua kuwa hivi, yeye atamtafuta wa kuwa vile anavyotaka yeye.  Akianza kupunguza mawasiliano kwako usishangae, bali jua yuko mbioni kukutema.

Pia mwenzako anaweza kubadilika ikiwa dhamira yake kwako haikuwa hiyo unayodhani. Ndiyo, alikwambia anakupenda ila hakumaanisaha hivyo. Japo maneno yake yako hivyo, ila alichokitaka kwako ni kile ulichompa wiki iliyopita. Ndiyo maana baada ya hapo hajakupigia tena simu.

Huna haja ya kulalama, ila cha kufanya ni kuzidisha umakini kuweza kumtambua yupi mkweli na nani tapeli.

Ila pia si vyema kila muda kuwa na mawazo hasi, wakati mwingine mwenzako hakupigii simu kutokana na mazingira aliyopo. Mwanzo mlikuwa mnaongea usiku kucha, ila sasa sheria ya kazini inamtaka usiku afanye kazi na sio kuwa ‘busy’ na simu. Kuwa na makini katika mabadiliko ya mwenzako. Wapendwa tuishie hapa, nafasi inanihukumu!

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -