Monday, October 26, 2020

Kwanini kukosekana kwa Ibrahimovic ni habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MANCHESTER, England

MANCHESTER United watamkosa Zlatan Ibrahimovic watakapopambana na Arsenal, mchana wa leo, lakini hii inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wao.

Unajua ni kwanini? Kinda Marcos Rashford ataanza kwenye eneo la ushambuliaji akiwa straika wa kati.

Hii itakuwa kumbukumbu kwa kinda huyo, aliyeanza pambano lake la kwanza la Premier League dhidi ya Arsenal msimu uliopita na kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu, United wakipata ushindi wa 3-2.

Ni mchezo dhidi ya Arsenal uliomtambulisha Rashford kwenye ulimwengu wa soka, akimaliza msimu wa 2015-16 kwa kufunga mabao 8 kwenye michezo 18 aliyocheza.

Bila shaka atakumbukwa sana Louis van Gaal kwa kumuamini na kumpa nafasi Marcos.

Miezi tisa baada ya tukio lile, maisha ya Rashford yamekuwa tofauti pale Old Trafford, tangu Jose Mourinho alipokabidhiwa kibarua cha kuinoa Manchester United.

Awali kabisa wakati akiongea kwa mara ya kwanza na waandishi, Jose alijaribu kujisafisha kwa tuhuma yake ya kutowaamini chipukizi, lakini ujio wa Zlatan Ibrahimovic ukaleta majibu ya tabia yake.

Ibrahimovic akapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, huku Rashford akitupwa benchi.

Kwa kipindi chote Rashford alikuwa mkimya, japo mara chache alizokuwa akipewa nafasi, alizitumia vyema.

Mchezo wake wa kwanza chini ya Mourinho aliingia akitokea benchi na kufunga bao la ushindi dhidi ya Hull kwenye dakika za nyongeza.

Hapa akaanza kuaminiwa kidogo na Mourinho kiasi cha kupewa nafasi ya kucheza kwenye dakika 45 za kipindi cha pili kwenye pambano la ‘Manchester derby’.

Mchezo uliofuata dhidi ya Feyenoord, Rashford alipewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufanya vyema, United ikilala bao 1-0.

Tangu hapo, Mourinho akawa anamtumia Rashford kama winga wa pembeni, huku mkongwe Ibrahimovic akicheza nafasi ya straika wa kati.

Kimsingi, Rashford si winga kama ambavyo Mourinho anajaribu kuiaminisha dunia.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na mtandao wa Sky Sports, Septemba, Marcos Rashford aliweka wazi kuwa hajawahi kucheza kama winga tangu akiwa na miaka 12.

“Binafsi, kufunga mabao mengi zaidi ndilo jambo ninalolipa kipaumbele kwenye maisha yangu ya soka,” alisema Rashford.

Na kitendo chake cha kufunga mabao manne kwenye michezo sita kilitosha kabisa kwa binadamu yeyote anayependa soka kufahamu eneo sahihi analotakiwa kucheza Rashford.

Msimu huu akicheza pembeni ya uwanja, Rashford hajafunga bao kwenye michezo 10 aliyocheza akiwa na United na timu yake ya taifa. Hii ni takwimu mbovu zaidi kwenye maisha yake ya soka.

Nyakati fulani Rashford alisema kucheza pembeni kunamfanya apate uzoefu na kuzidi kukomaa kisoka na Mourinho amekuwa akinufaika na kasi yake linapokuja suala la kujilinda, lakini mabadiliko haya yanaonekana kumgharimu kwa sasa.

Kwa kulinganisha takwimu za msimu huu na msimu uliopita, ni wazi kuwa Rashford amepoteza makali yake tangu alipoanza kucheza pembeni.

Rashford ni mzuri kwa kusoma njia za mipira akiwa kwenye boksi, ndiyo maana shuti lake la kwanza alilopiga akiwa na jezi ya United lilikwenda kimiani.

Kumpanga pembeni ni kumrudisha nyuma kisoka, msimu huu wastani wake wa kutengeneza nafasi umeshuka, hata ukokotaji wake wa mpira ni tofauti akitokea pembeni.

Kasi yake na uwezo wake wa kumiliki mpira ni kitu hatari kwa mabeki wa timu pinzani na ni faida kwa wachezaji wenzake, dhidi ya Arsenal msimu uliopita, tuliona namna kina Laurent Koscielny walivyopata shida kupambana naye.

Hana nguvu ya kusukumana na mabeki kama alivyokuwa Ibrahimovic, lakini akili yake na wepesi ni kitu hatari zaidi akiwa kwenye boksi.

Kama Mourinho atachukua nafasi hii ya kumuamini Rashford na kumpanga eneo la straika kama alivyofanya Van Gaal msimu uliopita, huenda safu ya ulinzi ya Arsenal ikawa kwenye nyakati ngumu sana pale Old Trafford.

Kitu pekee kinachoweza kumfanya Mourinho abadili mawazo ni ufiti wa Wayne Rooney.

Kama Wayne atakuwa ‘fiti’ huenda Jose akatamani kuwa na mchezaji mzoefu zaidi kwenye eneo la mbele, hivyo Rashford anaweza kujikuta akipangwa tena pembeni.

Msimu uliopita Rashford alianza safari yake ya EPL dhidi ya Arsenal kwa kufunga mabao mawili na endapo Mourinho akimpa nafasi leo, huenda ikawa mwanzo wa safari yake ya pili pale Old Trafford.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -