Tuesday, October 20, 2020

KWANINI MADRID WALIVAA JEZI ZA PLASTIKI?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MADRID, Hispania


MABINGWA mara 11 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, mapema wikiendi iliyopita waliwaacha watu na maswali juu ya jezi walizotumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Sporting Gijon.

Mtanange huo uliomalizika kwa Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ulikuwa na kitu kigeni machoni mwa wadau wa timu hiyo ambapo jezi zilionekana kuwa ni nyepesi mno hasa baada ya kuloweshwa na mvua kubwa iliyonyesha kwenye dimba la Santiago Bernabeu.

Jezi hizo zilitengenezwa kwa kutumia makopo ya plastiki na kitendo hicho ni cha thamani, kwani ni kampeni dhidi ya uharibifu wa mazingira hasa katika Bahari ya Hindi na kampuni ya Adidas ndio iliyochukua jukumu la kutengeneza jezi hizo.

Kila jezi ilitengenezwa kwa kutumia chupa 28 za plastiki zilizotumika ambapo kwenye kola zake kulikuwa na neno ‘For the Ocean’ (kwa ajili ya bahari).

Kampuni ya Adidas inafanya kazi sambamba na taasisi ya ‘Parley for the Ocean’ ambayo ina nia ya kuikumbusha dunia juu ya utunzaji wa maeneo ya bahari yanayosumbuliwa na uharibifu unaotokana na kazi za binadamu.

Hapo awali, Adidas ilitengeneza jezi za plastiki kwa klabu ya Bayern Munich, ingawa ilidaiwa kwamba jezi nyeusi za ugenini zinazotumika na klabu hiyo zisingependeza kama ilivyo kwa jezi nyeupe za Madrid.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -