Monday, November 23, 2020

KWANINI MASHABIKI WA CHELSEA WALIMZOMEA MOURINHO?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

WAKATI ratiba ya robo fainali ilipopangwa na Chelsea kupangiwa kuchuana na Manchester United, ulikuwapo uwezekano mkubwa bila kujali chochote Meneja wa United, Jose Mourinho, kujikuta katikati ya changamoto kubwa ya kutoelewana na mashabiki wake wa zamani wa Chelsea.

Historia ya maisha ya Mourinho na Chelsea inavutia mno.

Mreno huyo alitwaa mataji saba makubwa na Chelsea yakiwamo matatu ya Ligi Kuu England ndani ya misimu miwili.

Kwa takwimu hiyo, Mourinho ni kocha bora zaidi kuwahi kuinoa Chelsea, hakuna ubishi juu ya hilo.

Hicho ndicho kilichomfanya Mourinho akawajibu mashabiki waliokuwa wakimzomea usiku ule ambao N’Golo Kante kwa mara ya pili aliifunga United na kuiondoa kwenye Kombe la FA.

Kwanini aliwajibu? Walimzomea. Walimwita ‘Juda’ na yeye akawaonesha ishara ya vidole vitatu akimaanisha bila yeye wasingeweza kunyanyua makombe matatu ya ligi.

Hawakuwa mashabiki wengi, bali ni wachache ambao hawakuridhishwa kusikia Mourinho ametua Manchester United.

Kwa dakika 90 walikuwa wakimpigia kelele, ni kwa sababu tu alikuwa karibu nao kwenye benchi la ufundi.

Zaidi ya kuwaonesha ishara hiyo ya vidole vitatu, aidha alikaririwa akisema mbele ya waandishi wa habari baada ya mchezo kuwa kuitwa Juda si jambo la ajabu kwake, kwani bado anajijua kuwa yeye ni namba moja ndani ya Stamford Bridge na hadi takwimu zake zitakapokuja kuzimwa na kocha mwingine ndio waanze kumzomea.

Licha ya Mourinho kutamba hivyo, ni yeye mwenyewe aliyesababisha hadhi yake kupungua alipotimuliwa katikati ya msimu uliopita, lakini hata alipoondoka bado aliipenda klabu, aliiheshimu.

Na ndio maana hakuna ambaye alifikiri kwamba Antonio Conte angekuwa na faida kubwa ndani ya Chelsea kwa msimu huu tu wa mwanzo, hata Mourinho hakuwahi kudhania.

Nani alichukua hata dakika chache kuunda taswira ya mabadiliko makubwa ambayo yametokea hivi sasa chini ya Conte? Hakuna. Hizo ndizo baadhi ya sababu za mashabiki kumpenda Conte.

Ule mchezo wa kwanza wa ligi baina ya Chelsea na United, mchezo wa kwanza kwa Conte na Mourinho kuvaana, Uwanja wa Stamford Bridge ulikuwa mzuri kwa Mourinho. Mashabiki walimkaribisha vizuri tu, kilichobaki ni nini ambacho kingetokea ndani ya uwanja.

Huo ndio mchezo uliodhihirisha Conte anaunda himaya yake, anautaka ufalme wake pale. Akamchapa Mourinho bao 4-0.

Akashangilia sana, mashabiki wakampenda, upendo wa mashabiki na Conte kuanzia hapo ukawa hauelezeki.

Kadiri mchezo ulivyokuwa ukiendelea, jina la Antonio lilisikika likiimbwa mno. Kulikuwa na asilimia chache ya furaha moyoni mwa Mourinho aliposikia na kuona kilichokuwa kikiendelea, kumwona Conte akishangilia hadi kupitiliza kikomo mbele ya mashabiki waliokuwa wakimhusudu hapo kabla lilikuwa ni jambo gumu kukubaliana nalo.

Mourinho hakuwa na utulivu moyoni. Alianza kusikika akizungumza vitu visivyo na ulazima zaidi ya kuifanya kazi iliyompeleka Manchester United. Tangu alipotandikwa na Conte, vijembe kuhusu Chelsea vikaanza kutoka kinywani mwake.

Kama si kuzungumzia aina ya soka la ‘kujilinda’ la Conte, basi angezungumzia wepesi wa ratiba waliyonayo Chelsea au aina ya mashabiki waliopo Stamford Bridge.

Ule upendo aliokuwa akiupata Mourinho kutoka kwenye mitaa ya SW6 Fulham na kando ya Mto Thames jijini London, umepungua kwa kiasi kikubwa, dalili zinaonesha heshima yake itashuka zaidi miaka michache ijayo.

Nini kitakachochangia kupunguza heshima ya Mourinho na nini ambacho hakitawazuia mashabiki wa Chelsea kumzomea? Ni hadi pale Mourinho atakapoanzisha upinzani wa kweli dhidi ya Conte. Lakini kwa sasa anaonekana kama mpumbavu kwa kujibizana na mashabiki.

Hadi pale atakapomalizana naye kwenye mechi ya mwisho ya ligi msimu huu, atapata nafasi ya kujipanga upya.

Heshima pekee ya Mourinho msimu huu ni Kombe la EFL na hana budi kutwaa mengine zaidi, Conte hajatwaa lolote lakini anao uwezo wa kupiku mafanikio aliyoyapata Mourinho pale Chelsea.

Hata hivyo, kawaida ya mapenzi yaliyokuwa matamu pia kuna kipindi yana uwezo wa kupungua na kugeuka machungu kama shubiri. Mashabiki wa Chelsea kwa sasa wana upendo kwa Conte, si Mourinho wanayemwona United.

Unahisi ni lini watajitokeza na kuzungumzia kwa uzuri mafanikio aliyowapa? Labda ni pale atakapoondoka England.

Lakini kwa sasa mapenzi yao ya kweli yapo kwa Conte, wanavutiwa naye. Na ndio maana upendo wao kwa Mwitaliano huyo umewafanya kufikia hapo na kuangusha vikwazo vyote, akiwemo Mourinho na Manchester United yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -