Sunday, November 29, 2020

KWANINI UMRI SI KIGEZO KATIKA NDOA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NI kawaida mume kuwa na umri mkubwa na mke wake kuwa na umri mdogo. Ni kawaida ambayo kwa namna fulani imegeuka kuwa kama sheria.

Utofauti wa maumbile baina ya mwanamume na mwanamke unafanya mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kuwa sawa na mwanamume wa miaka 26. Si vibaya kawaida hii kuwa sheria. Si kawaida mbaya, bali huleta hali fulani ya uwiano wa kimwili baina ya wanandoa.

Ni dhahiri mwili wa mwanamke huwa unamfanya aonekane mkubwa zaidi hata kama ana umri sawa na mwanamume. Mwanamke wa umri wa miaka 18 anaweza kumuona mvulana wa umri huo kama mdogo wake. Katika hili hakuna ajabu hata kidogo.

Mwanamke huyu kwanza anaweza kuwa na mwanamume mkubwa zaidi ya umri wake, na jamii ikaona kawaida, ila mwanamume wa umri huo ni ngumu kuwa na mwanamke wa umri mkubwa zaidi.

Na hata ikitokea kwa wengi huwa na hali fulani ya kujishtukia na kuona kama wamefanya jambo ambalo si sahihi sana. Je, ni halali mwanamke kuwa na mwanamume mwenye umri mdogo?

Hakuna dhambi kuwa na mwanamume mwenye umri mdogo katika uhusiano au ndoa. Suala ni kwanini unakuwa naye. Kama ni upendo ndio unaosukuma kuzaliwa kwa uhusiano wenu, hatari iko wapi?

Ndiyo, kunaleta hali fulani ya kupendeza kwa mwanamume kumzidi mwanamke umri katika ndoa. Ila si sheria kamili. Kuna kupendeza zaidi kama kuwa na mtu unayempenda? Umri nini kwani? Marehemu Aaliyah aliwahi kusema ni namba tu.

Ikiwa unayemzidi umri huna hisia naye utalazimisha? Ikiwa ambaye kakuzidi umri unampenda na yeye ana hisia kama hizo kwako suala ni kumkimbia? Hapana!

Mapenzi hujenga daraja katika maisha yetu. Kuwa na mwanamke mwenye umri mkubwa haina maana heshima na thamani yako katika nyumba itatoweka. Heshima haijengwi kwa kuwa na mwanamke mwenye umri mdogo au mwanamume mwenye umri mkubwa. Heshima huwa na mizizi yake mingine.

Kama anakupenda kwa dhati haiepukiki kukupa heshima. Kama kweli anakuhitaji katika maisha yake ni lazima ataiona thamani na hadhi yako katika maisha yake. Katika umri hakuna heshima kama hakuna upendo. Katika umri kuna woga kama hakuna upendo. Suala kwanza ni upendo. Halafu tutaangalia nani mkubwa na nani mdogo.

Usimuache kwa sababu eti umemzidi umri na wala usitake kuwa naye eti kwa sababu umemzidi umri. Umri ni kitu cha kawaida sana baina yenu. Ni kitu ambacho hakiwezi kuleta amani na thamani baina yenu ikiwa hakuna upendo wa kweli. Chanzo cha heshima katika uhusiano si umri. Chanzo cha masikilizano baina ya wanandoa si umri, bali ni upendo.

Katika upendo kuna masikilizano na kuona thamani ya mwingine. Katika upendo kuna kuambiwa na kuelewa na kufuata yaliyo mema. Usimezwe na hoja ya umri na kujikuta ukiingia kwa mtu usiyemkubali katika nafsi yako.

Mapenzi kwa mtu usiyempenda ni kheri kubaki bila mtu. Ni mateso na hakuna amani timilifu. Ni huzuni na hakuna muda wa kufurahi kwa dhati na mwenzako.

Ndiyo, mwanamke anawahi kukua kuliko mwanamume.

Tofauti zenu za kibaolojia zinafanya umbile la mwanamke liukimbilie uzee kabla ya umbile la mwanamume. Wengi hapa mnaogopa. Mnajua baada ya kuwa na Ally hali umemzidi umri basi ukizeeka atakuwa busy na vimada. Kuna kitu mnakataa kukiona angali kinaonekana. Wangapi japo bado wote vijana wanasalitiana katika uhusiano wao?

Hawezi kukusaliti kwa sababu una umri mkubwa. Anaweza kukusaliti kwa sababu kadha wa kadha, zikiwamo za kutojielewa vizuri.

Baada ya kuwa katika umri stahili wa kuoa au kuolewa, suala la kukufanya uoe lisiwe tena umri wa Fulani, bali uhalali na haki ya moyo wako kwake. Je, unampenda? Anakupenda kwa dhati? Basi ndoa ifungwe.

    ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -