Wednesday, November 25, 2020

KWANINI UNAKUWA NA MTU WA AINA HII?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MPAKA kwa Mungu anakuapia kuwa anakupenda. Unamsikiliza, kisha unamkubalia. Katika maelezo yake anasema anakupenda sana japo yuko na mtu mwingine katika uhusiano na wewe unakubali kuwa naye.

Huwa unafikiria nini kumkubali mtu katika hali kama hii? Unadhani uhusiano wenu unakuwa katika picha gani?

Mapenzi ni suala la kipekee sana. Mtu anayekupenda kwa dhati anahitaji uwe wa pekee sana katika maisha yake. Anahitaji akujali sana yeye, akuthamini zaidi yeye na umtazame sana yeye. Ni vipi huyu awe na mtu mwingine na bado aseme anakupenda wewe? Mapenzi si hayo. Ni tofauti sana na ngonjera za mtaani na wala hazifanani na sinema za ndotoni.

Mapenzi ni hisia za ndani zenye kujali na kuthamini na kuona dhati ya nafsi ya mtu. Hata siku moja mtu mwenye hisia kamili na wewe hawezi kuwa na mtu mwingine.

Ndiyo, kuna suala la tamaa katika maisha. Ila ili uwe katika uhusiano kamili unahitajika kuwa na mtu makini na thabiti juu yako. Mtu mwenye kujitoa kwa ajili yako. Atakayekuwa tayari kupambana na kila changamoto za kimaisha kwa ajili ya kupata faraja ya penzi lako.

Anayekwambia nakupenda na kisha akawa na mtu mwingine, mwangalie vizuri. Nini maana ya upendo basi ikiwa anaweza kuwa na wewe na akampenda mwingine? Mapenzi yanajengwa na hali fulani ya wivu. Hali hii hufanya mhusika atake mwenzake kwake awe na maana nyingi zaidi kuliko kwa mtu mwingine. Atake amguse yeye, ampapase yeye na amfanyie kila jambo maalumu yeye tu. Sasa vipi awe na mtu mwingine na bado aseme anakupenda? Haya si mapenzi.

Hapana! Anayekupenda atahitaji kuwa na wewe. Akujali na akuthamini wewe tu. Vipi anayekupenda kimapenzi awe na wewe na awe na mwingine? Hapana! Hapo kuna usanii. Mapenzi si katika namna hiyo. Anayetaka kuwa na wewe na pia yuko na mwingine, jua si mapenzi yanamsukuma kufanya hivyo. Aidha ni tamaa au kuna jambo jingine usilolijua analihitaji kutoka kwako.

Kuna wengi wamejuta kwa kuingia katika uhusiano wa namna hii. Bila kujiuliza mara mbili wakakubali kuingia katika uhusiano na watu wenye wapenzi. Sasa kila kitu kwao kibaya. Mapenzi mabaya na pia maisha kwao mabaya.

Hata siku moja huwezi kufurahia maisha kama mapenzi yaliyoingia katika nafsi yako hayako katika hali nzuri. Kabla hujakubali kuwa na mtu katika uhusiano itazame kwanza furaha yako.

Furaha yako inathamani sana katika maisha yako kuliko mwili wake wala ufundi wake kitandani. Ijali na ithamini sana. Kama ana mtu mwingine, una mambo mawili tu ya kuamua. Kama anakuhitaji basi awe na wewe na aachane na mwingine, ila kama anaona hawezi kuachana na mwingine bora wewe uachane naye. Siku njema!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -