Tuesday, November 24, 2020

KWANINI YANGA HAWAKUSONGA MBELE LIGI YA MABINGWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

TIMU ya Yanga juzi wakiwa ugenini walijikuta wakikubali kutolewa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, baada ya kutoka suluhu na wenyeji wao, Zanaco, mechi iliyochezwa Uwanja wa Mashujaa, Wanajangwani wakirejea rekodi yao ya mwaka jana kuangukia Kombe la Shirikisho.

Yanga imetolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Machi 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na wanapaswa kujilaumu zaidi kutokana na bao la kusawazishwa kwa Wazambia hao kufungwa dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame, wakati wenyewe walishajitengenezea mazingira mazuri dakika ya 38 baada ya Simon Msuva kuifungia timu yake bao la kuongoza.

Sare hizi mbili zinaipa nafasi Zanaco iendeleze rekodi ya kuitupa nje Yanga kwenye michuano ya Afrika, baada ya mwaka 2006 pia kuwatoa katika hatua kama hii ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakishinda 2-0 Lusaka, baada ya kufungwa 2-1 Dar es Salaam.
Yanga sasa itamenyana na timu iliyofuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, wakati Zanaco inakwenda moja kwa moja hatua ya makundi.

Kuondolewa kwa Yanga katika Ligi ya Mabingwa si jambo la ajabu na lilitegemewa na wengi, licha ya Wanajangwani wenyewe kuonekana walikuwa na matumaini makubwa, hasa baada ya ujio wa kocha Mzambia, George Lwandamina, aliyeipa mafanikio makubwa Zesco mwaka jana kwenye mashindano hayo.

Zipo sababu nyingi ambazo ni wazi Yanga wasingeweza  kuingia hatua ya makundi katika Kombe la Mabingwa na BINGWA linakuletea baadhi yake, lakini pia kama hawatafanya marekebisho mapema, ni wazi hata Kombe la Shirikisho  walikoangukia huenda wasidumu.

Asili ya soka la bongo

Yanga imeathirika mno na janga hili linalosumbua hata taifa letu, kwani hakuna wachezaji wenye ari ya kutaka kufanya jambo fulani litakalowapa mafanikio wao au timu zao.

Ukimtoa Msuva, ambaye kwenye mechi zote mbili ameonekana kujitoa zaidi ndani ya Yanga, wanandinga wengine wote waliingia uwanjani kukamilisha ratiba pekee na hii ni kutokana na tayari wamejiwekea misingi ya kukosa uchu wa mafanikio katika maisha yao na ndiyo maana huishia kucheza soka la ndani bila kujiongeza ili waweze kwenda nje.

Kujituma kwa wachezaji wa Yanga ilikuwa ni njia bora kwa wao kusonga mbele, ikizingatiwa Zanaco walishajipambanua namna wanavyocheza kwenye mtanange wa awali ambao walipambana na kupata bao moja ugenini.

Kukata tamaa

Hakukuwa na sababu ya msingi ya kukata tamaa kwenye mchezo huo, ambao uliwahitaji Yanga kufunga mabao ugenini na kusonga mbele, na hicho ndicho kilichowaadhibu kwa kuingia mchezoni bila kuwa na morali.

Mgomo baridi

Ingawa uongozi ulikataa juu ya suala hili, lakini ukweli utabaki kuwa, wachezaji wa Yanga walikuwa na mgomo baridi uliochangia kwa kiasi kikubwa kutocheza vizuri.

Inakumbukwa kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba, baadhi ya wachezaji muhimu waligoma kucheza, sababu kubwa ikiwa ni kutolipwa mishahara yao kwa zaidi ya miezi miwili, jambo lililowalazimu uongozi chini ya Makamu Mwenyekiti wao, Clement Sanga, kukaa nao chini na kuwapa ahadi, kitu kilichodhihirisha mgomo ulikuwapo.

Ishu hii ya mgomo ilianza kusikika kutoka kwa mastaa Bossou na Ngoma, lakini kuna wale ambao waliamua kukaa kimya na hilo ni jambo baya, licha ya kwamba waliosema wazi walionekana wabaya, kwao ni heri kuliko waliokaa kimya na kucheza chini ya kiwango.

Je, kwa hali hii wangeweza kufanya nini katika mechi yao dhidi ya Zanaco, wakati walishapoteza morali ya kuitumikia Yanga kwa kutolipwa stahiki zao kwa miezi kadhaa? Na hata kocha wa aina gani angekuja Yanga, katu wachezaji wasingeweza kumwelewa wala kucheza kwa kiwango kilichotegemewa na wengi.

Maandalizi hafifu

Kwa sasa analaumiwa sana Lwandamina na kuonekana Hans van Pljuim anastahili kuendelea kuinoa Yanga, lakini mashabiki wanasahau kikosi cha Wanajangwani hao kilikufa tangu kikiwa na Pluijm.

Na hili tujikumbushe tu matokeo waliyoyapata Yanga katika mechi za hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho mwaka jana, yanaweza kutoa majibu sahihi, kwani ni vigumu kwa kikosi kinachopata kila kitu kikashika mkia.

Kiuhalisia mwaka huu Yanga haikuwa na maandalizi kuelekea mechi za kimataifa na badala yake waliyachukulia poa, tofauti na kipindi cha Pluijm ambapo vitu vingi vilifanyika kuashiria Yanga wapo makini kimataifa.

Sekeseke lililotokea hivi karibuni liliifanya klabu kukosa nguvu ya kuweka kambi ya maana, tofauti na wapinzani wao, Zanaco, timu inayomilikuwa na Benki ya Taifa ya Bishara ya Zambia, ambao kabla ya kukutana na Yanga walicheza mechi za kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Zimbabwe, klabu ya CAPS United, kisha wakakutana na TP Mazembe, mechi zilizomsaidia kocha wa timu hiyo, Mumamba Numba, kutambua udhaifu wa kikosi chake.

Kiungo tatizo

Tangu Yanga ilipoondokewa na viungo wao wakabaji, Salum Telela, Mbuyu Twite na kumleta Zulu, bado eneo hilo linakosa nguvu.

Kamusoko anamwagiwa sifa kutoka kila kona, lakini hajafanikiwa kuziba pengo la Twite, aliyeondoka kwa madai ya kuzeeka, pamoja na Telela ambao wote walikuwa viraka ndani ya kikosi.

Kwa falsafa ya Lwandamina, anahitaji kiungo anayeweza kuwa bize kuwalinda mabeki wake na hana tamaa ya kupanda mbele, ambaye ndani ya Yanga hayupo, kwani Zulu ameonyesha kushindwa kuimudu nafasi hiyo, na sasa wanamtumia Yondani, ambaye akili yake imekuwa kama beki, maana ndiyo nafasi aliyocheza kwa miaka mingi.

Lwandamina amekuwa akimtumia Yondani kama kiungo namba sita, kwa kuwa ameona anafaa kwenye mipango yake na soka la Tanzania lilivyo, huku Zulu akichezeshwa mbele yake.

Lakini licha ya kufanya hivyo, bado hajafanikiwa kumtengeneza Yondani kuwa namba sita na anaonyesha dhahiri si sehemu sahihi kwake, kutokana na kuathirika na ubeki wa kati, ambao ndio asili yake.

Ukiangalia kwenye mechi zote mbili za Yanga na Zanaco, utakumbuka Wanajangwani wanavyokata mawasiliano baada ya kutolewa kwa Kamusoko na kukosekana kwa Niyonzima  mchezo wa kwanza, lakini pia wachezaji wa Zanaco waligundua mapema kuwa, Yondani anacheza nafasi ambayo si yake, hivyo kutumia mbinu za kiakili zaidi kumdhibiti.

Na hili lilijitokeza pia katika mchezo wa marudiano, licha ya uwepo wa Niyonzima, aliyetajwa kuongeza nguvu, lakini bado hakuna kilichosaidia, jambo linalowalazimu Yanga kufanya mchakato wa kumpata kiungo namba sita asili.

Udogo wa kikosi chao

Kwa mwonekano wa nje, Yanga ina kikosi kipana, lakini suala la kutumika kwa wachezaji walewale kikosi cha kwanza linakinzana na dhana ya kuwa na kikosi kipana.

Ukiangalia Yanga wachezaji wake waliowasajili, ni wazi kila nafasi ina watu zaidi ya wawili, lakini mfumo uliowekwa na benchi la ufundi kuanzia lile la Pluijm na hata hili la Lwandamina, kubadilika kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni jambo la nadra.

Hilo linahatarisha viwango vya wachezaji wengine wanaosugua benchi, na ndiyo maana kila wanapopewa nafasi huishia kuonekana hawawezi.

Kwenye mechi zote mbili, tumeshuhudia Yanga ikikosa mabao mengi kizembe, nafasi alizozipata Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya, ni wazi wangekuwapo Ngoma na Tambwe wasingeweza kukosa mabao na hii inaonyesha madhara ya kuwategemea na kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji, huku wengine wakila mishahara ya bure.

Majeruhi

Mwaka huu, licha ya wachezaji kutolipwa fedha zao, lakini wengi wao hawakuwa fiti kwa kiasi kikubwa, kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua pamoja na matatizo ya kifamilia.

Ukimtoa Haruna Niyonzima, aliyekuwa na matatizo ya kifamilia, Amis Tambwe aliyekuwa majeruhi, pia kuna watu kama Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Vicent Bossou nao hawakuwa na utimamu wa mwili, ingawa walilazimika kucheza baada ya kocha kukosa chaguo jingine.

Kwenye mchezo wa marudiano Niyonzima aliweza kupewa nafasi, lakini bado mapengo ya Ngoma na Tambwe yalionekana wazi, kutokana na wale waliopewa nafasi kushindwa kuimudu vema safu ya ushambuliaji.

Kuchoka kwa wachezaji

Hakuna atakayepingana na hili, wachezaji wa Yanga kwa sasa wamechoka na hiyo ni kutokana na kukosa muda wa kupumzika.

Inakumbukwa tangu yalipomalizika mashindano ya Ligi Kuu msimu uliopita, Yanga hawakupata muda wa kuiweka freshi miili yao, kwani walilazimika kwenda kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho na baada ya kutolewa wakarejea kwenye Ligi Kuu Tanzania bara, Mapinduzi Cup, jambo lililosababisha wanandinga hao kupata majeraha ya mara kwa mara ambayo hawapati muda wa kuyatibu vizuri kutokana na kuhitajika kuendelea kuitumikia timu, ukizingatia kikosi chao ni kidogo kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -