Sunday, January 17, 2021

Kwanini yanga itamkumbuka Pluijm

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA SALMA MPELI

KAMA kuna uamuzi mgumu ambao Yanga wameufanya katika miaka ya karibuni ni huu wa kumfungulia milango ya kutokea Kocha Hans van der Pluijm na kumleta George Lwandamina kutoka Zesco United.

Kitendo cha Lwandamina kutua nchini kimya kimya na kudaiwa kuwa tayari amesaini mkataba wa miaka mwili na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kimesababisha Pluijm aamue kujiuzulu nafasi yake ya ukocha Jangwani.

Kufuatia uamuzi wa Pluijm kujiuzulu kuifundisha Yanga, umeibuka mjadala miongoni mwa wadau wa soka nchini ambao asilimia kubwa wanaulaumu uongozi wa timu hiyo kwa kitendo cha kumtema kocha huyo, licha ya mafanikio aliyowaletea, huku wengi wakiamini kuwa Wanajangwani hao wamekurupuka kumleta Lwandamina.

Kutokana na hali hiyo, makala haya yamelenga kuonyesha kwanini Yanga itamkumbuka Pluijm, licha ya ujio wa Lwandamina, ambaye aliifikisha Zesco United nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Utawala wa soka la Bongo

Tangu arudi Jangwani kwa mara ya pili Desemba 2014, kurithi mikoba ya Marcio Maximo, Pluijm alifanikiwa kutawala soka la bongo na kutwaa mataji yote ya ndani katika kipindi hiki, akiipoteza vibaya Azam, ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wakati akitua nchini.

Pluijm alifanikiwa kuipa Yanga mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, katika misimu ya 2014/15 na 2015/16, huku pia akitwaa taji la Ngao ya Jamii mwaka 2015.

Mbali na Ligi Kuu, msimu uliopita Pluijm aliipa Yanga Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, hii ni baada ya michuano hiyo kurudi kwa mara ya kwanza baada ya kufutwa kwa miaka kadhaa, mafanikio hayo ni ushahidi tosha kuwa Mholanzi huyo alishafanikiwa kutawala soka la bongo katika kipindi chake Jangwani.

Soka la kushambulia

Pluijm ni muumini wa soka la kushambulia na kumiliki mpira na ndiyo maana alipotua nchini kurithi mikoba ya Maximo alibadilisha mfumo wa uchezaji wa kikosi cha Yanga kutoka kucheza soka la kujilinda hadi timu hiyo kucheza soka safi la kushambulia.

Chini yake, Yanga ilisifika kwa kucheza soka safi na la kushambulia ambalo liliwafanya kuwa hatari na kushinda mabao mengi kwenye mechi zao, kitu ambacho kiliwapa burudani mashabiki wa timu hiyo.

Hivyo kufuatia kuondoka kwake, mashabiki wa Yanga watakosa lile soka la pasi ambalo walilibatiza jina la ‘kampa kampa tena’ na hii ni moja ya sababu kubwa kwa nini timu hiyo itamkumbuka sana Mholanzi huyu.

Mafanikio Afrika

Japokuwa inaaminika kuwa Yanga wenyewe walitaka timu yao angalau ifika nusu fainali ya michuano ya kimataifa na ndiyo maana wamekubali kumuachia kutokana na kushindwa kufanikisha hilo, lakini ukweli ni kuwa chini yake miamba hiyo ya Jangwani imepiga hatua kubwa sana katika michuano ya Afrika.

Kitendo cha kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997 ni ushahidi tosha kuwa Pluijm alikuwa na mafanikio makubwa kwenye michuano ya kimataifa na chini yake Yanga ilifanikiwa kuwa timu tishio na hata kuweza kupambana na timu za Kiarabu na kutolewa kwa tofauti ndogo ya mabao tofauti na ilivyokuwa zamani.

Kumaliza ufalme wa Simba

Mashabiki wa Yanga watamkumbuka Pluijm kutokana na kufanikiwa kumaliza ubabe wa Simba dhidi ya timu yao na kufanikiwa kuwafunga nyumbani na ugenini kwa mara ya kwanza msimu uliopita baada ya miaka kibao.

Mbali na sare ya mwanzo wa msimu huu, Pluijm msimu uliopita alifanikiwa kuifunga Simba nyumbani na ugenini kwa mabao 2-0 katika kila mechi na kumaliza ufalme wa miamba hiyo ya Msimbazi kwa Yanga.

Nidhamu ndani ya kikosi

Pluijm anaondoka Yanga akiwa amefanikiwa kusimamia nidhamu ndani ya kikosi hicho, kutokana na tabia yake ya kupenda wachezaji wake wawe na nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Makocha kadhaa wamekuwa wakifeli kufanikiwa kwenye kikosi cha Yanga kutokana na kushindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji, lakini chini ya Pluijm wachezaji wa timu hiyo walikuwa na nidhamu ya hali ya juu na kuonyesha weledi kwenye kazi yao kiasi cha kusaidia mafanikio ya timu.

akatimkia African Lyon ya vijana.

“Tangu nasoma elimu ya msingi nilikuwa nina ndoto za kuja kuwa mchezaji soka maarufu ndani na nje ya Tanzania, ili kutimiza hili nikakazana kujihusisha na mpira kwenye timu ya Abajalo huku nasoma.

“Baada ya kumaliza elimu ya msingi, wazazi hawakuwa na fedha za kuniendeleza, nikaamu kujikita moja kwa moja katika soka na ndipo nilipojiunga na Sifa United ya Manzese, kabla ya kwenda African Lyon kikosi cha vijana na kushiriki Uhai Cup ambayo umahiri wangu uliweza kuwashawishi viongozi na benchi la ufundi kunipandisha kikosi cha wakubwa na kuanza kucheza ligi kuu.

“Mwadui ilipopanda daraja nilikuwa miongoni mwa wachezaji wake na niliweza kucheza na kikosi hicho msimu wake wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, kabla ya msimu huu kuamua kuondoka na kujiunga na Stand United kwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuona maslahi yangu yamepanda kuanzia mshahara na hata fedha za usajili,” anasema Kelvin Kiduku.

Kwanini mwaka mmoja Stand?

“Yapo mengi yanayotokea kwetu wachezaji ambayo wengi wetu hatupendi kuyaweka wazi kwa kuhofia ipo siku unaweza kujikuta ukirudi katika timu uliyoizungumzia vibaya,” anasema Kelvin Kiduku. “Lakini pia mambo hayo ni sababu kubwa ya wanandinga wengi Tanzania kuamua kuomba wapewe mikataba mifupi.

“Kwangu kikubwa napenda kuishi kwa amani, ninaposaini mwaka mmoja inanipa nafasi ya kufanya mazungumzo sehemu nyingine iwapo nikiona hapa kuna vitu vinakwenda sivyo ndivyo, kuliko nikifungwa kwa zaidi ya kipindi hicho kutokana na ukweli kuwa mpira wetu wa kibongo hauna sheria zinazotulinda wachezaji kwa asilimia 90,” anasema.

Hat-trick yake

Sabato anasema kuwa kwake ni jambo la furaha, kwani tangu aanze kucheza timu zinazoshiriki Ligi Kuu ni mara yake ya kwanza kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja.

“Niliwahi kupiga hat-trick nikiwa na Mwadui ilipokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza, lakini kwa Ligi Kuu hii ni mara ya kwanza na ninachofurahi zaidi nimeweza kuwashinda wale ambao walikuwa wanapewa sifa, hususan wachezaji wa kimataifa.

“Kiukweli sikutarajia kufunga mabao matatu, ni jambo la kumshukuru Mungu na naweza kusema ni bahati ya kipekee kwangu ambayo sitoweza kusahau, kwani kwanza mchezo ulikuwa mgumu, mabeki wa Mtibwa walikuwa wakicheza kwa kukamia na walinichezea rafu za mara kwa mara, lakini nashukuru mchezo ulikwisha salama.

“Bao lile la tatu sikutarajia kama ningefunga, lakini jinsi lilivyopatikana na aina ya kulifunga naamini lingeingia kwenye orodha ya mabao bora ya msimu ambayo mwisho wa siku lingeshindanishwa.

“Lakini halikuweza kuonekana na Watanzania wala kwenye Shirikisho kutokana na ukweli hakukuwa na  kituo chochote kilichorekodi mechi, hivyo si ajabu wafungaji wa mabao bora ya msimu wakatoka kwenye mechi zinapocheza Simba, Yanga na Azam, ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kuonyeshwa,” anasema.

Mipango ya baadaye

Sabato, mwenye miaka 23 na mzaliwa wa Musoma, anasema kuwa moja ya mipango yake ni kuona siku moja anacheza soka la kulipwa nje ya Tanzania, lakini pia anatamani kukipiga kwenye moja ya klabu kati ya Simba au Yanga, ambazo zinatoa maslahi mazuri kwa wachezaji.

“Mpira ndio kazi yangu kubwa ambayo inaendesha maisha ya familia yangu kwa ujumla, hivyo natamani siku moja nizitumikie Simba au Yanga kwa vipindi tofauti, kwani ndizo timu zinazotoa maslahi mazuri kwa wachezaji, ukiitoa Azam iliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni, kwa maana hiyo iwapo kama watanihitaji nipo tayari kuwatumikia, lakini kwa masharti nitakayotoa ambayo naamini hayawezi kunibana kucheza soka la kulipwa,” anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -