Wednesday, October 21, 2020

KWAYA YA TAG KIMARA BONYOKWA YASAKA WAIMBAJI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA GLORY MLAY

LEO katika safu hii ambayo hutoka kila siku ya Jumamosi ikiwa ni maandalizi ya ibada ya Jumapili, ambapo hutembelea kwaya mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na wachungaji ili kupata ujumbe unaoweza kuwaongoza waumini wao kuelekea kwenye ibada ya kesho.

Kwaya iliyopata bahati kuwa kwenye safu hii ya leo ni kwaya ya Kanisa la Tanzania Assemblies (TAG), Kimara Bonyokwa, jijini Dar es Salaam.

BINGWA lilitembelea kwaya hiyo hivi karibuni na kufanya nao mahojiano kupitia mwenyekiti wa kwaya hiyo, Essau Edward, ambapo alisema kwaya hiyo ilianza mwaka 2015 mwishoni ikiwa na wanakwaya watano tu.

Alisema kwaya hiyo bado ni changa na haijapata nafasi ya kurekodi albamu kutokana na kanisa bado ni jipya na waumini wake ni wachache.

Mpaka sasa kwaya hiyo imefanikiwa kupiga hatua kwa kuwa na waimbaji 15 wakiwamo wanawake watano wa wanaume 10.

Edward alisema malengo walionayo kwa sasa ni kutafuta wanakwaya ili waongezeke na kuweza kuanza mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya kurekodi alibamu ya kwanza.

“Ukiangalia kanisa letu bado halijakuwa na kujulikana sana kama yalivyo makanisa mengine, hata ukiangalia jengo bado halijaisha na tunaendelea kujenga, tunawaomba vijana wanaotaka kujiunga nasi katika huduma hii ya uimbaji kwa njia ya kwaya wanakaribishwa,” alisema.

Alisema matarajio yao ni kuwa na mradi wa kwaya utakaowawezesha wao kufanya mambo ya kwaya bila kushirikisha kanisa, wanajipanga ili kuweza kujua nini cha kufanya ili kiweze kuwaletea faida katika kwaya yao.

Edward alisema kuelekea katika ibada ya kesho wamejiaanda vizuri pia wameandaa nyimbo zenye ujumbe kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.

“Waumini wote wa TAG wanatakiwa kuwahi katika ibada hii muhimu katika mwaka mpya, tumewaandalia nyimbo nzuri za kusifu na kuabudu zitakazokukutanisha wewe na Mungu,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -