Monday, November 30, 2020

LABDA MBINU HIZI ZITAUZIMA MOTO WA CHELSEA EPL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MOTO uliowashwa na Chelsea kwenye mbio za kuwania taji la Ligi Kuu England (EPL), hauonekani kuzimika kirahisi.

Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, Chelsea wameonesha kuwa msimu huu ni wao na wamepania kuupeleka ubingwa Magharibi mwa London yaliko maskani ya klabu hiyo.

Katika mchezo wa wikiendi iliyopita, walipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnley, mchezo ambao wakali hao wa Stamford Bridge walikuwa ugenini.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupachika bao kupitia kwa nyota wao, Pedro lakini Robbie Brady alichomoa.

Hata hivyo, zipo njia ambazo wachambuzi wa soka wanaamini kuwa zinaweza kutumika kuikwamisha kasi waliyonayo Chelsea msimu huu.

Kuwazuia kupata bao la kuongoza

Katika michezo 19 ambayo Chelsea wamepata bao la kuongoza, ni mitatu tu ambayo walifungwa.

Kikosi hicho cha Antonio Conte, kimekuwa kikicharuka na kuwazidi wapinzani wake kila wanapopata bao la kuongoza.

Ni kama Burnley walilishtukia hilo wakiwa wamechelewa lakini walipoamka waliweza kuwakabli vema wapinzani wake hao.

Baada ya bao la kwanza, Burnley hawakuwaruhusu Chelsea kupiga shuti lolote lililolenga lango.

Kuepuka ‘kukopi’ mfumo wao

Timu nyingi zilizokutana na Chelsea hivi karibuni zilijaribu kuiga mfumo wao wa 3-4-3. Ni Tottenham pekee walioweza kufanikiwa katika hilo baada ya kushinda mabao 2-0 pale White Hart Lane. Timu zilizobaki zilishindwa kuendana na ‘mzuka’ wa Blues.

Walichokifanya Burnley ni kupishana nao na kutumia mfumo wa 4-4-2.

Imeonekana kuwa zile zinazowaiga Chelsea katika mfumo wa 3-4-3 huwa hazijauzoea mfumo huo. Kwa maana nyingine, kwa kuwa ndio mfumo rasmi wa Chelsea, huwa wameuzoea zaidi kuliko timu zinazoiga.

Kuzuia wasitumie ‘counter-attack’

Arsenal walipata madhara makubwa kwa kitendo chao cha kuwaruhusu Chelsea kutumia mashambulizi ya kushtukiza ‘counter-attack’. Kwa kiasi kikubwa, Burnley walionekana kuwazuia katika hilo.

Waliwaruhusu Chelsea kuchezea mpira lakini si kutumia counter-attack, mbinu ambayo Chelsea wamekuwa wakiitumia katika michezo mingi msimu huu.

Kuwafunika viungo wake

Siri kubwa ya kuwazuia Chelsea kwa sasa ni kuhakikisha viungo wake hawachezi. Ni hatari zaidi kuwaruhusu N’Golo Kante na Nemanja Matic, kufanya wanavyotaka katika eneo la katikati ya uwanja.

Burnley walilijua hilo mapema na kwa kiasi fulani waliweza kuwamiliki. Burnley iliwatumia Joey Barton na Ashley Westwood, kuhakikisha Chelsea wanakuwa wapole katika eneo la kiungo.

Kuwazidi kasi

Takwimu za mchezo dhidi ya Burnley zinaonesha kuwa Chelsea walifunikwa katika suala la kasi ya uwanjani. Hiyo ilikuwa moja ya sababu ya wakali hao kutulizwa kwa sare.

Wachezaji wa Burnley walikimbia zaidi ya kilomita sita ukilinganisha na wenzao wa Chelsea.

Mchezaji aliyekimbia umbali mrefu alikuwa George Boyd wa Burnley ambaye alitumia kilomita 13.3. Kwa upande wa Chelsea, Marcos Alonso, alikuwa kinara wa kukimbia umbali mrefu kwenye kikosi cha Chelsea ambapo alitumia kilomita 12.5.

Kwa mantiki hiyo, kama timu pinzani zitaweza kuwa na kasi ya kuizidi Chelsea katika michezo iliyobaki, kuna uhakika mkubwa wa kuipunguza kasi.

Katika michezo michache ijayo ya Ligi Kuu England, Chelsea watavaana na Swansea, Watford, West Ham na Stoke City.

Je, timu hizo zitaweza kutumia vema mbinu hizo na kusimamisha kasi waliyonayo Chelsea katika mbio za kulifukuzia taji la Ligi Kuu England msimu huu?

Lakini pia, kuna uwezekano mkubwa wa Chelsea kuja kivingine katika michezo hiyo, hasa kutokana na ujanja wa mkongwe Conte ambaye amewahi kuwanoa mabingwa wa Seria A, Juventus na timu ya Taifa ya Italia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -