Monday, October 26, 2020

‘LAST CHANCE’ NI NAFASI YA MWISHO KWA ARSENAL KUPUNGUZA POINTI ZA CHELSEA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...
LONDON, England

LEO ndio leo ambapo vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, watawakaribisha wapinzani wao wa Jiji la London, Arsenal kwenye dimba la Stamford Bridge katika mchezo wa mapema leo.

Timu hizo zitaingia dimbani na lengo linalofanana la kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka sawa kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Vijana wa Arsene Wenger, Arsenal hawana budi kushinda mchezo wao huu wa leo ikiwa wanahitaji kusalia kwenye mbio za ubingwa, kwani Chelsea kwa sasa iko mbali kulinganisha na timu nyingine tatu zilizo kwenye ‘Top Four’ na mbili zilizo nje ya miamba hiyo minne ya ligi.

‘The Gunners’ hao wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakiachwa na vinara Chelsea kwa tofauti ya pointi tisa.

Arsenal walikuwa na nafasi adimu ya kupunguza pointi za Chelsea wiki hii, lakini waliiacha fursa hiyo iende kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Watford.

Kuelekea mchezo huo wa leo, mkongwe wa zamani wa Arsenal, Robert Pires, alisema hii ni nafasi ya mwisho kwa Arsenal kuiangusha Chelsea leo nyumbani kwake na kuhakikisha matumaini ya ubingwa yanaendelea kuwapo.

Pires ambaye aliwahi kunyakua mataji ya EPL alipokuwa akikitumikia kikosi cha Arsenal na pia akiwa mmoja wa wachezaji waliounda kikosi kilichotwaa ubingwa bila kufungwa mchezo wowote (Invincibles) msimu wa 2003/04, anaamini kuwa wachezaji Alexis Sanchez na Mesut Ozil wataisaidia timu hiyo kubakia kwenye mbio za ubingwa.

“Nadhani hii ni nafasi ya mwisho kwa Arsenal na ndio fainali ya Ligi Kuu England. Kama Chelsea wataifunga Arsenal, nadhani msimu wa hii ligi utakuwa umefika mwisho,” alisema Pires.

“Kwa miezi kadhaa sasa Chelsea imekuwa na kiwango kizuri lakini kama kuna linalowezekana ni Arsenal kuifunga Chelsea pale Stamford Bridge.

“Nawaona Sanchez na Ozil kama watu watakaofanya makubwa pale Stamford Bridge,” aliongeza.

Kwenye mchezo wa kwanza msimu huu uliopigwa kwenye dimba la Emirates, Arsenal iliibomoa Chelsea kwa kuichapa maba 3-0, kipigo kilichopelekea kocha Antonio Conte kubadili mfumo wa Chelsea na kuanza kutumia mfumo wa 3-5-2.

Tangu alipobadili mfumo, Conte na vijana wake wamepoteza mchezo mmoja tu hadi sasa katika michezo yao 17 ya ligi waliyocheza, wakipata ushindi wa mechi 15.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -