Thursday, October 22, 2020

Leaders Club kuwaka moto leo; Yemi Alade, Chameleone waahidi bonge la shoo

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MICHAEL MAURUS

HATIMAYE kilele cha tamasha la Tigo Fiesta 2016, kinatarajiwa kuwa leo katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam ambapo wasanii wakali wa hapa nchini na wengine kutoka nje ya Tanzania, wanatarajiwa kufanya shoo ya aina yake ili kuhitimisha msimu huu wa tukio hilo kubwa kabisa la burudani ya muziki katika ardhi ya Taifa hili lililoasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tamasha hilo lililoanzia Mwanza, limetembelea mikoa takribani 14 ambayo ni Shinyanga, Tabora, Kagera, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Iringa na kwamba leo litakamilisha mkoa wa 15 jijini Dar es Salaam.

Unajua kwanini mikoa 15? Kwa mujibu wa waratibu wa tamasha hilo, kampuni ya Prime Times Promotion, idadi hiyo imetokana na umri wa tukio hilo kwani mwaka huu limetimiza mwaka wake wa 15 tangu lilipofanyika kwa mara ya kwanza.

Kama ilivyokuwa katika misimu iliyopita, safari hii pia tamasha hilo limeambatana na shughuli na matukio mbalimbali kama vile uchangiaji wa madawati kwa kila mkoa lilikofanyika, lakini pia uvumbuzi wa vipaji vya muziki kupitia program ya Fiesta Super Nyota.

Program hiyo iliyoendeshwa katika kila mkoa, imetoa vijana 16 wenye vipaji vya hali ya juu kupitia michujo ambayo ilikuwa ikifanyika katika maeneo husika na kupata mshindi mmoja kati ya wengi waliojitokeza kujaribu bahati yao ya kuwa nyota wa muziki wa baadaye kupitia tamasha hilo.

Japo ilipangwa kila mkoa kutoa mshindi mmoja wa super nyota, lakini Mwanza ilipewa upendeleo ya kutioa washindi wawili kutokana na mkoa huo kuwa wa kwanza kufanyika kwa tamasha hilo, lakini pia kuwa na washiriki wenye uwezo wa hali ya juu hivyo wandaaji kuamua kuchukua washindi wawili.

Tayari washindi hao 16 wapo jijini Dar es Salaam na kwamba jana usiku ilitarajiwa kufanyika kwa fainali kwenye ukumbi wa New Msasani Club ili kupata washindi wawili ambao wangepata ofa kadha wa kadha zinazolenga kuwaendeleza kimuziki waweze kutimiza ndoto zao za kuwa nyota wa muziki hapa nchini kama ilivyokuwa kwa wengine waliopitia program hiyo miaka iliyopita.

Juu ya tamasha la leo, mbali ya wasanii wanaotamba hapa nchini, kuna wakali kutoka nje ya Tanzania ambao wanatarajiwa kufanya shoo ya aina yake ili kuhitimisha msimu huu wa tamasha hilo kwa kishindo cha ‘Imooooo’ ambayo ndio kauli mbiu ya tukio hilo lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkoanoni ya Tigo Tanzania.

Baadhi ya wasanii wa kigeni ambao wameshatua nchini watakaofanya yao leo ni pamoja na Wanigeria Yemi Alade na Tekno pamoja na Mganda, Jose Chameleone, huku pia kukitarajiwa kuwa na ‘surprise’ ya msanii mwingine kutoka Marekani atakayeungana na wengineo kushambulia jukwaa.

Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini, watakaopanda jukwaani leo ni Ben Pol, Nandy, Christian Bella, Fid-Q, Weusi, Roma, Chegge, Dogo Janja, Billnass, Stamina, Jux, Barnaba, Maua Sama, Darassa, Vanessa Mdee, Sholo Mwamba, Jay Moe, Msami na Juma Nature.

Wengine ni Snura, Baraka Da Prince, Shilole, Manfongo, Belle 9, Lord Eyes, Young Dee, Raymond, Mr. Blue, Hamadai na Ali Kiba.

Baada ya kutimua vumbi katika mikoa 14, kwa sasa wapenzi wa burudani wa Dar es Salaam wamekuwa na shauku ya kuona wasanii hao watafanya nini leo pale Leaders Club.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Yemi Alade, alisema kuwa amejiandaa vilivyo kutoa shoo ya nguvu ili kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki nchini.

“Nimefurahi sana kuja Tanzania, ninawapenda sana Watanzania na ninawaahidi kufanya shoo ya aina yake katika tamasha la Fiesta kesho (leo), hivyo mashabiki wa muziki wafike kwa wingi,” alisema.

Katika tamasha la mwaka huu, wapenzi wa muziki wamejikuta wakipata burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wamefanikiwa kutoa shoo ya aina yake.

Wasanii ambao wamekuwa wakipanda jukwaani katika mikoa yote tamasha hilo lilikofanyika, wameacha gumzo kutokana na burudani ya nguvu waliyoitoa, kuanzia katika uimbaji hadi uchezaji.

Lakini pia kwa mwaka huu wasanii wameonesha uwezo mkubwa wa kuimba muziki wa moja kwa moja wakiwa kwenye majukwaa, tofauti na ilivyokuwa misimu kadhaa iliyopita.

Burudani hiyo kwa mwaka huu imekwenda sambamba na ugawaji wa madawati kutoka kampuni ya Tigo kwa kila mkoa ambao tamasha hilo limefanyika.

Katika tamasha la leo, kivutio zaidi kwa wasanii wa hapa nchini wanatarajiwa kuwa Juma Nature, Ben Pol, Ali Kiba, Jux, Shilole, Mr. Blue, Man Fongo, Roma, Weusi, Bella, Fid-Q, Dogo Janja, Vanessa Mdee na wengineo.

Waandaaji wa Tamasha la Fiesta, Kampuni ya Prime Times Promotion chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Kusaga, wameahidi shoo ‘bab kubwa’ leo ili kufunga kwa kishindo msimu huu.

“Tutaendelea na harakati zetu za kuendeleza vipaji kutoka kwa wasanii wapya na wanaoibukia katika kizazi kipya kupitia matamasha ya Fiesta kama ambavyo tumekuwa tukifanya misimu iliyopita wakati kupitia Dance la Fiesta, Fiesta Super Star, Fiesta Super Diva na Bonanza la Soka la Fiesta.

“Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 15 ya Tamasha la Fiesta nchini, mwaka huu tumeendesha kampeni maalum inayojulikana kama ‘kipepeo’ kwa ajili ya kuwatambua na kuwasaidia wasichana walio na mahitaji maalumu katika mikoa 15 ambako tamasha  hili limefanyika,” anasema.

Kwa upande wake, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Savkat Berdiev, anasema wapenzi wa muziki Dar es Salaam watarajie burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii wa muziki wa ndani na nje ya nchi leo Leaders Club.

“Ikiwa ni kampuni iliyojikita katika kukuza sekta ya muziki wa ndani, tunayo furaha kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hili kubwa la muziki nchini Tanzania. Lengo letu kila mara limekuwa ni kunyanyua wasanii wa ndani kupitia majukwaa ambayo  yatawawezesha kuonesha vipaji vyao, kuwaunganisha na mashabiki ili kuzipaisha kazi zao na kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha,” anasema.

Akielezea zaidi jinsi mashabiki wa muziki nchini na wateja wao wanavyonufaika na tamasha la mwaka huu, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, anasema wamekuwa wakiwapatia vifurushi vinavyowawezesha kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo na ukomo vinavyojumuisha dakika 490 Tigo kwenda Tigo.

“Tamasha la Fiesta linawakaribisha Watanzania wote na pia tukio hili linatoa shuguli za kijamii tukiwa na kauli mbiu yetu Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Imoooo,” anasema Mpinga.

Wapenzi wa muziki na burudani kwa ujumla wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani, wanaweza kupata tiketi za kuingia kwenye tamasha hilo leo kwa njia ya Tigopesa au mitandao mingine na kwa kufanya hivyo, wanapata punguzo la asilimia 10 ya kiingilio cha kawaida cha Sh 20,000.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -