Saturday, November 28, 2020

LEICESTER CITY KUFUATA NYAYO ZA HAWA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

BAADA ya timu ya Leicester City kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu England, wengi waliamini haitaweza kufika mbali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa  Ulaya, UEFA.

Hata hivyo, tofauti na matarajio ya wengi, mdogo mdogo mabingwa hao wa msimu uliopita wakajikuta wakitinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Ulaya.

Kwa sasa timu hiyo ndiyo pekee kutoka England iliyobaki katika michuano hiyo, baada ya nyingine, Arsenal, Tottenhm na Man City kuishia njiani.

Kwa sasa kilichobaki ni swali moja kama timu ambayo iliweza kupigania isishuke daraja msimu wa 2014/15, lakini ikafanikiwa kutwaa ubingwa, kampeni zilizofuata itaweka rekodi nyingine?

Mbali na swali hilo, jingine ni je, itaweza kufuata nyayo za timu nyingine ambazo hazikutarajiwa na kujikuta zikifika mbali katika michuano hiyo?

Katika Makala haya BINGWA itaangalia timu nyingine ambazo hazikuwahi kupewa nafasi kutokana na uchanga wake katika michuano hiyo, lakini zikafanikiwa kufika mbali.

1.Málaga: 2012/13 robo fainali

Kutokana na uwekezaji mzuri, ndicho kilichoifanya FC Málaga kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne katika michuano ya La Liga msimu wa 2011/12.

Hata hivyo, baada ya bajeti kupunguzwa ikamfanya Manuel Pellegrini kuwakosa nyota wake, Santi Cazorla na Nacho Monreal kabla ya michuano hiyo ya msimu wa 2012/13.

*Ilichokifanya katika mechi hiyo ya robo fainali, baada ya timu hiyo kutoka nyuma na kisha ikaongoza dhidi ya Dortmund zikiwa zimebaki dakika nane ikajikuta ikiruhusu mabao mawili katika muda wa nyongeza na hivyo kutupwa nje kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa kwanza.

*Kilichotokea baadaye

Bada ya hapo, Pellegrini aliamua kuondoka na timu hiyo ikanyang’anywa nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya Europa msimu wa 2013/14 kutokana na tatizo la kifedha na hadi sasa Málaga haijawahi kurejea katika michuano hiyo mikubwa Ulaya.

2.Villarreal: 2005/06  nusu fainali

Mwaka 2004   Pellegrini ndiye alikuwa nyuma ya mafanikio ya Villarreal na aliwawezesha kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na mara tatu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Villarreal walitinga hatua hiyo, baada ya kuitupa nje Inter Milan kwa matokeo ya jumla ya mabao 2-2, wao wakinufaika na la ugenini, lakini wakajikuta wakitupwa nje na Arsenal kwa bao 1-0, walilofungwa wakiwa ugenini na kisha wakishindwa kushinda wakiwa nyumbani.

*Kilichotokea baada ya hapo

Baada ya hapo Villarreal iliendelea kushiriki katika michuano mbalimbali ya Ulaya na vile vile msimu wa 2008/09 ikajikuta tena ikifungwa na Gunners katika hatua ya robo fainali.

Baada ya michuano hiyo, Pellegrini akaondoka  na msimu wa 2011/12  ikashuka daraja kabla ya kupanda tena msimu uliofuata na tangu kipindi hicho imekuwa ikiishia kushika nafasi ya sita bora katika ligi ya nyumbani.

3.Deportivo La Coruña: 2000/01 robo fainali

Deportivo ilijidhihirisha kuwa miamba ya soka nchini Hispania kipindi cha miaka ya 1990 na msimu wa 1999/2000, mabao makali yaliyowekwa kimiani na nyota wao, Roy Makaay yakawafanya Galicians  kutwaa ubingwa wa Liga.

Hata hivyo, baada ya kuvuka milima na mabonde, huku ikipiku vigogo kadhaa, ikiwamo AC Milan na Paris Saint Germains, ikajikuta ikikwama hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Leeds United kwa jumla ya mabao 3-2 kutokana na mchezo wa kwanza kufungwa 3-0 na ikashinda 2-0 ikiwa nyumbani.

*Kilichotokea baadaye

Tangu kipindi hicho Deportivo iliendelea kuwa miongoni mwa tatu bora za La Liga hadi msimu wa 2003/04 wakati ilipofanikiwa kufika nusu fainali ya michuano hiyo ya UEFA.

Hata hivyo, makali ya timu hiyo yalianza kufifia baada ya mwaka 2005  aliyekuwa kocha wao, Javier Irureta, kuondoka  ambapo tangu kipindi hicho imewahi kushiriki mara moja katika michuano hiyo mwaka  2008/09 na huku ikinusurika kushuka daraja mara mbili.

4.Lazio: 1999/2000  robo fainali

Vinara hao wa Ligi ya  Serie A walianza kuchomoza kipindi cha miaka ya 90 na waliweza kupokwa ubingwa siku ya mwisho msimu wa 1998/99  walipofungwa na AC Milan, lakini baadaye wakaja kutwaa ubingwa wa Kombe la Washindi, UEFA.

Msimu uliofuata vijana hao waliokuwa chini  ya Sven-Göran Eriksson waliweza kumaliza kiu yao ya muda mrefu ya kutwaa ubingwa wa kombe hilo la Scudetto kwa mara ya pili baada ya ule wa kwanza wa mwaka  1973/74 na hivyo kuchomoza kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo ya Ulaya.

*Kilichotokea baada ya hapo

Tatizo la kifedha ndilo lililokifanya kikosi hicho kushindwa kutamba katika michuano hiyo na hivyo kuwafanya kulazimika kusubiri hadi msimu wa 2006/07.

5.Bayer Leverkusen: 1997/98 robo fainali

Baada ya kwa mara ya kwanza kushika nafasi ya pili katika kipindi cha miaka minne kati ya 1997 na 2002 katika  michuano ya Bundesliga, Leverkusen walijiimarisha katika michuano hiyo kwa kumteua kocha Christoph Daum.

Kwa kujiimarisha huko walijikuta wakitinga hatua ya robo fainali baada ya kuzifunga timu kadhaa kabla ya kuchapwa na Real  Madrid katika mchezo huo kwa jumla ya mabao 4-1, baada ya kutoka sare ya 1-1 wakiwa nyumbani kabla ya kuambulia kipigo cha mabao 3-0 ugenini.

*Kilichotokea baada ya hapo

Tangu kipindi hicho Leverkusen wamekuwa wakiendelea kuwa washindani katika mbio za kusaka taji hilo na waliweza kufika fainali mwaka 2002.

 6.Auxerre: 1996/97 robo fainali

Baada ya timu ya Auxerre kufanya vyema ikiwa chini ya kocha wao, Guy Roux, ambaye alichukua mikoba mwaka 1964 wakati timu ikiwa daraja la tatu na kuiwezesha mwaka 1995/96  kutwaa ubingwa, ndicho kilichoifanya itinge kwenye michuano hiyo ya UEFA.

Hata hivyo, ndoto za kusonga mbele zilizimwa na wale wale waliokutana nao hatua ya nusu fainali msimu wa 1992/93, Borussia Dortmund, baada ya kufungwa jumla ya mabao 4-1 kutokana na mchezo wa kwanza walifungwa 3-1 wakiwa ugenini, kabla ya kuchapwa 1-0 nyumbani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -