Tuesday, October 20, 2020

LIGI DARAJA LA KWANZA IMEKUWA JIPU SUGU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara inaelekea ukingoni na timu tatu zitakazopanda kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara zitajulikana muda si mrefu. Ligi hiyo inayochezwa kwenye makundi matatu, imekuwa na ushindani mkubwa lakini pia ndiyo ligi ambayo imekuwa na malalamiko mengi sana pengine kuliko ligi zote hapa nchini.

Malalamiko kwenye ligi hiyo yanatokana na ukweli kwamba baadhi ya timu zimeonekana kupewa upendeleo maalumu ili zipate matokeo mazuri yatakayoziwezesha kupanda ligi kuu. Matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani yamekuwa yakiripotiwa kwenye baadhi ya mechi ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.

Vurugu hizo ambazo zimejeruhi baadhi ya watu, zimetokana na kile kinachoelezwa wachezaji au mashabiki kupinga uamuzi wa waamuzi ambao unaonekana kuwa na upendeleo kwa baadhi ya timu. Mjini Iringa Uwanja wa Samora umekuwa ni wa machinjioni kwani wenyeji Lipuli FC wamekuwa wakilalamikiwa sana kwa kulazimisha kupata ushindi ili wapande ligi kuu.

Pamoja na Lipuli, lakini pia kuna timu nyingine ambazo zimekuwa zikitajwa kubebwa kwa nguvu zote kuhakikisha zinapanda kucheza Ligi Kuu msimu ujao. Kutokana na hali hiyo, tunaona wazi kwamba ligi hiyo inaendelea kuwa jipu kubwa hasa katika suala zima la upangaji wa matokeo.

Msimu uliopita malalamiko yalikuwa mengi sana hata kabla ya sakata la rushwa kuibuka. BINGWA tunaona ipo haja kwa vyombo vinavyohusika na soka kuamka na kuiangalia kwa makini ligi hii kwani imekuwa na taswira mbaya kabisa kwenye soka la Tanzania.

Tunaamini Shirikisho la Soka nchini (TFF), linaweza kututoa kwenye sintofahamu hii iliyoikumba Ligi Daraja la Kwanza na pia tunaamini kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikihusishwa kwa ukaribu hasa katika mechi hizi za mwishoni mambo yatakwenda sawa na timu za kupanda ligi kuu zitapatikana kwa uhalali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -