Sunday, January 17, 2021

LIGI KUU IKIENDELEA LEO, TUNATAKA SOKA SI KARETI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LIGI Kuu Tanzania Bara, inatarajia kuendelea leo kwa mechi mbili kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.

Katika Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam, Azam wataikaribisha Simba, wakati Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Majimaji kwenye Uwanja wa Sokoine.

Ligi hiyo inaendelea baada ya kusimama kwa muda kupisha mechi za kirafiki za kimataifa na za kufuzu fainali za Kombe la Dunia na zile zilizokuwa katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) zilizochezwa hivi karibuni.

Wakati ligi hiyo ikisimama, tayari tulishashuhudia mechi moja ya ligi ikichezwa kwa kila timu na ile ya Ngao ya Jamii iliyowakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, Agosti 23 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mechi hizo, tulijionea baadhi ya matukio yaliyofanywa na wachezaji ambayo si ya kiuanamichezo, ikiwamo kuchezeana rafu za kijinga na zisizo na ulazima mwisho wa siku wahusika kuzigharimu timu zao na wao wenyewe kwa kupewa kadi.

Kutokana na hali hiyo, BINGWA tunaziomba klabu pamoja na wachezaji, kucheza soka la amani ili kuwapa burudani mashabiki watakaofika viwanjani kuzishuhudia timu zao.

Tunasema hivyo kwani endapo wachezaji watacheza kwa kujituma na uwajibika uwanjani, hapatakuwapo na purukushani zisizo za lazima zaidi ya kila timu kupambana ili kupata matokeo mazuri na yasiyo na lawama.

BINGWA tunasema haya kutokana na ukweli kuwa kwa siku za karibuni, mechi za Ligi Kuu Bara zimekuwa zikichezwa kwa mtindo wa ‘bora liende’ kiasi cha kushindwa kutofautisha na mechi za mchangani.

Tunaamini kama timu zetu zikiamua kucheza soka, basi ligi yetu inaweza kufika mbali zaidi ya mahali ilipo kwa sasa.

Kwa kuwa ligi yetu inaonekana katika mataifa mbalimbali barani Afrika kutokana na kuonyeshwa ‘live’ na runinga, hali hiyo itasaidia kuwavutia mashabiki wengi watakaokuwa wakitamani kuifuatilia kwa karibu ili kujionea burudani na vipaji vilivyosheheni kwa baadhi ya wachezaji wetu badala ya kushuhudia mieleka, kareti na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kwa kuonesha kandanda safi, pia inaweza kuwa njia mbadala kwa wachezaji wetu kuwavutia mawakala wanaosaka vipaji ili kuvinadi katika mataifa mbalimbali, zaidi ikiwa ni barani Ulaya.

Tunaamini ligi yetu ina vijana wengi chipukizi ambao wana kiu ya kufikia mafanikio makubwa kama si kuwapita nyota wengine duniani wanaotamba kwa sasa akiwamo Mtanzania, Mbwana Samatta, anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -