Sunday, November 1, 2020

LIGI KUU ‘LIVE’ ILIVYOONGEZA MSISIMKO WA SOKA NCHINI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS


KIPUTE cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea leo na wikiendi hii kwenye viwanja tofauti nchini, huku mabingwa watetezi, Simba, wakiwa wageni wa Mbao FC, jijini Mwanza.

Kwa mara nyingine, Simba watashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kupepetana na wenyeji wao hao bila kocha msaidizi wao, Masoud Djuma, mchezo utakaoonyeshwa ‘live’ na kituo cha televisheni cha Azam TV.

Djuma hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoifuata Ndanda FC mkoani Mtwara na kuambulia suluhu mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Kitendo cha Djuma kutokuwapo mjini Mtwara kimeonekana kuwagawa watu wa Simba, baadhi wakiamini kuwa ndicho kilichochangia timu yao kutopata ushindi kwa madai kuwa Mrundi huyo ndiye anayewajulia wachezaji wake, tofauti na ilivyo kwa bosi wake, Mbelgiji Patrick Aussems.

Baada ya madai hayo, wengi walitarajia Djuma angeungana na kikosi jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa leo, lakini haijawa hivyo.

Imeelezwa kuwa Djuma amebaki Dar es Salaam ili kuendelea na programu aliyopewa na Aussems ya kuwapiga msasa wachezaji ambao hawapo katika kikosi cha kwanza, wakiwamo Haruna Niyonzima na Jjuuko Murushid.

Na sasa mashabiki na wapenzi wa Simba wanajiuliza iwapo kikosi chao kikiwa bila Djuma kinaweza kupata ushindi leo dhidi ya ‘wabishi’ Mbao FC.

Kwa kuwa mchezo huo utaonyeshwa ‘live’ na Azam TV kama ilivyokuwa kwa ule wa Nangwanda Sijaona na mingineyo ya Ligi Kuu Bara, ni wazi itakuwa ni fursa ya kipekee kwa kila shabiki wa soka nchini kujionea kile kitakachotokea CCM Kirumba leo.

Katika mchezo uliopita wa Simba mjini Mtwara, pamoja na madai ya kutokuwapo kwa Djuma kwamba kulichangia timu yake kutoshinda, lakini kila mmoja alijionea ‘live’ kupitia Azam TV jinsi vijana wa Ndanda walivyopambana hadi dakika ya mwisho.

Tofauti na ilivyokuwa katika michezo iliyopita, safari hii wachezaji wa Ndanda walionekana kuwapania vilivyo Simba na mwisho wa siku, kuambulia pointi moja.

Wachezaji wa Ndanda FC walionekana kutotishwa na majina ya wachezaji wa Simba kama Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Cletus Chama, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na wengineo.

Walicheza kwa umakini na nidhamu ya hali ya juu kuhakikisha Simba hawapati bao kwenye uwanja wao na wakafanikiwa katika hilo.

Kwa kila aliyefika uwanjani au kushuhudia mechi ile ‘live’ kupitia Azam TV, alijionea mwenyewe jinsi vijana wa Ndanda wakiongozwa na Kiggi Makasi walivyopambana kuipigania timu yao.

Na iwapo Simba wasingekuwa makini, isingeshangaza kuwaona wakitoka Nangwanda Sijaona bila pointi yoyote kutokana na jinsi walivyobanwa na wenyeji wao wikiendi iliyopita.

Swali ni je, na leo Simba bila Djuma watashindwa kutoka na pointi au kuambulia moja tu kwenye Dimba la CCM Kirumba? Hilo ni suala la kusubiri dakika 90 za mtanange huo wa kukata na shoka ambao nao utakuwa ‘live’ kupitia Azam TV.

Yote kwa yote, kitendo cha Azam TV kuonyesha ‘live’ (moja kwa moja) mechi za Ligi Kuu Bara, kimeongeza msisimko wa hali ya juu katika soka la Tanzania.

Tofauti na ilivyokuwa zamani, kwa sasa visingizio vya timu ngeni kuonewa na waamuzi au kufanyiwa hujuma vimepungua, kwani kila mmoja anaona ‘live’ kinachoendelea viwanjani.

Kabla ya Azam TV kuanza kuonyesha mechi za Ligi Kuu Bara ‘live’, kulikuwa na visingizo lukuki kwa timu zinazopoteza zikidai wenyeji wao kupendelewa.

Visingizio hivyo vilifanywa kwa kuwa hakuna aliyeweza kuona kilichokuwa kikiendelea viwanjani zaidi ya mashabiki wa eneo husika.

Ama kwa hakika, Azam TV kupitia kampuni ya Azam Media, imeleta mapinduzi makubwa ya soka hapa nchini kwa kitendo cha kuonyesha ‘live’ mechi za Ligi Kuu Bara na michuano mingineyo kama Ndondo Cup.

Katika kuonyesha jinsi AzamTV ilivyodhamiria kuwapa burudani Watanzania, juzi ilitangaza kutoa ofa ya tiketi 250 kwa mashabiki ili kushuhudia pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga Septemba 30, mwaka huu.

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, huku matangazo yake yakianza kurushwa na AzamTV kuanzia asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa Masoko wa Azam Media na Uhai Production, Abdul Mohamed, alisema hicho ni kitu kipya kitakachoongeza thamani ya pambano hilo la kukata na shoka.

“Namna pekee ya kupata tiketi hizo kwa wateja wetu kushuhudia mchezo huo ni kulipia miezi mitatu kifurushi cha Play ambacho malipo yake ni Sh 28,000 kwa mwezi,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Vipindi wa Azam Media, Baruan Muhuza, alisisitiza mchezo huo utakaoonyeshwa ‘live’ kupitia Azam TV utakuwa na mwonekano bora zaidi ya mingineyo, kuanzia katika uonyeshwaji wake, uchambuzi, picha na mengineyo.

Mhuza aliahidi kituo chao hicho cha televisheni kuendelea kuwapa uhondo wa aina yake Watanzania wapenda soka na burudani kwa ujumla.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -