Tuesday, November 24, 2020

LIGI YA KIKAPU IWE CHACHU KUIBUA VIPAJI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LIGI ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, inatarajia kuendelea wikiendi hii katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, ikishirikisha timu 24 za wanaume na wanawake.

Tayari baadhi ya timu zimecheza mchezo mmoja baada ya ligi hiyo kuanza wiki iliyopita, huku kila moja ikitoa upinzani mkali lengo likiwa ni kushinda ili kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu.

Timu za wanaume kama JKT, Savio, Oilers, Pazi na Outsiders zinajulikana zaidi kutokana na ukongwe wao katika ligi hiyo, lakini zikiwa zinaundwa na wachezaji wengi nyota wa kikapu.

Lakini tumeshuhudia timu kama hizo za Vijana, Ukonga Kings, Chui, Jogoo, Prisons, DB Young Stars, Mgulani JKT, Mabibo Bullet, Kurasini Heat na ABC zikionyesha uwezo wa hali ya juu kuhakikisha zinapata matokeo mazuri ambayo yatawaweka katika mazingira bora ya kutwaa ubingwa.

Kilichotuvutia zaidi ni kuona timu za wanawake zikiwa zimejitokeza nyingi kushiriki ligi hiyo ambayo tunaiona ni muhimu kwa kipindi hiki kuibuka vipaji chipukizi.

Timu hizi za wanawake, Don Bosco Lioness, JKT Stars, Jeshi Stars, Vijana Queens, Ukonga Queens, Oilers Princesses, Kurasini Divas na  Tanzania Prisons, zimetupa picha halisi kuwa kuna vipaji vingi katika mpira wa kikapu na sasa kuna haja ya wadhamini kujitokeza kwa lengo la kuboresha ligi ya RBA.

BINGWA tunaunga mkono juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), kuhakikisha ligi inafanyika kila mwaka kwa lengo la kukuza viwango vya wachezaji.

Pamoja na jitihada za BD, wakati umefika kwa Watanzania, kampuni mbalimbali kujitokeza kukipa sapoti chama hicho ili kiweze kutimiza malengo ya kuboresha ligi ya RBA.

Hata hivyo, tunaona ligi ya RBA imekuwa ikiendeshwa katika wakati mgumu kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.

Mfano wiki ya kwanza ya ligi hiyo wakati mabingwa watetezi Savio wakimenyana na JKT, umeme ulikatika na kupelekea mchezo huo kusimama kwa zaidi ya dakika 40.

BINGWA tunaamini kuwa changamoto hiyo ni kubwa, isingekuwapo kama kungekuwa na mwamko wa fursa ya uwekezaji katika mchezo wa kikapu hapa nchini.

Kama ilivyo katika soka, ifike kipindi kampuni na wafanyabiashara wakubwa waone umuhimu wa kujitokeza kufukuzia kuwekeza katika mpira wa kikapu, kitu ambacho kitatoa fursa kwa vipaji vingi kuonekana.

Tunarudia kusema kwamba ligi ya RBA iwe chachu kwa kuibuka vipaji chipukizi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -