Wednesday, November 25, 2020

LIGI YA MABINGWA AFRIKA WANAUME 15 WALIVYOTINGA RAUNDI YA KWANZA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

CAIRO, Misri

KIVUMBI cha Ligi ya Mabingwa Afrika kilianza Februari 10 na kinatarajiwa kumalizika Novemba 5, mwaka huu.

Tayari jumla ya michezo 15 imeshachezwa tangu kuanza kwa mashindano hayo makubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.

Kwa mujibu wa ratiba, wababe hao watapepetana katika mechi za raundi ya kwanza zitakazoanza kuchezwa Machi 10-12 na 17-19.

Miongoni mwa mechi kali zilizovuta hisia za mashabiki wengi ni ile ya mabingwa wa zamani wa Kombe la Shirikisho, AC Leopards dhidi ya UMS De Loum ya Cameroon.

Wababe hao wa soka nchini Kenya walianza kwa kufungwa mabao 2-1 nchini Cameroon, lakini matokeo ya mabao 2-2 katika mchezo wa marudiano yamewawezesha kutinga raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini.

Mtanange mwingine ni ule uliozikutanisha AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) dhidi ya Royal Leopards ya Ligi Kuu nchini Swaziland.

Wababe hao wa DRC ndio waliofanikiwa kusonga mbele baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 katika michezo miwili.

Stade Malien ya Mali nayo imesonga mbele baada ya kuiondosha Barrack Young Controllers ya Liberia.

Mikwaju ya penalti ndiyo iliyoamua Malien kutinga katika hatua inayofuata, ikiwa ni baada ya sare ya bao 1-1.

Timu mbili kutoka Nigeria, Rivers United na Enugu Rangers, nazo zilipata nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo. Rivers United waliizamisha Real Bamako ya Mali kwa jumla ya mabao 4-0. Kwa upande wao, Enugu walihitimisha safari ya JS Saoura ya Algeria.

Kwa upande wao, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga Sports Club, walifanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 6-2.

Lakini pia, Wakali wa soka nchini Ethiopia, Saint George, Al Ahli Tripoli ya Libya na Rail Club de Kadiogo ya Burkina Faso, ziliweza kujihakikishia nafasi ya kupiga hatua katika michuano hiyo.

KCCA kutoka Uganda ilijihakikishia nafasi ya kusonga mbele baada ya kuisambaratisha Primeiro de Agosto ya Angola, huku Ferroviario de Beira ya Msumbiji ikiwafungasha virago Wazanzibari waliokuwa wakiwakilishwa na Zimamoto.

Bingwa wa michuano hiyo inayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), atajinyakulia kitita cha Dola za Marekani milioni 2.5 (zaidi ya Sh bilioni 5 za Tanzania).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -