Tuesday, November 24, 2020

LIGI YA MABINGWA ULAYA… MADRID, LEICESTER WATASUBIRI KWANZA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid na mabingwa wa Ligi Kuu England, Leicester City wote watapaswa kusubiri kuweza kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo ya Ulaya, baada ya kutoka sare kwenye mechi zao za juzi Jumatano.

Borrusia Dortmund wameungana na klabu nyingine kama Arsenal, Paris Saint-Germain, Atletico Madrid na Bayern Munich kutinga hatua ya 16 bora ya ligi hiyo katika mechi zilizopigwa juzi Jumanne.

Leicester, ambao mwanzoni walipewa nafasi kubwa baada ya kushinda mechi zao tatu za mwanzo, lakini walishindwa kusonga mbele baada ya kutoka sare ya 0-0 na FC Copenhagen.

Pointi hizo zinawafanya Foxes kuwa na pointi tatu zaidi kileleni mwa msimamo wa Kundi G, huku wapinzani wao Porto ambao juzi waliifunga Club Brugge bao 1-0 mjini Ureno kwa bao la Tomas Silva, wakifuatia.

Katika Kundi F, Real Madrid walitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Legia Warsaw pamoja na kuongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na Gareth Bale.

Bale, alimtengenezea bao la pili Karim Benzema, lakini Legia walibadilika kipindi cha pili na kusawazisha kwa mabao ya Vadis Odjidja-Ofoe, Miroslav Radovic na Thibault Moulin kufunga la tatu kabla ya Mateo Kovacic kuwasawazishia mabingwa hao watetezi.

Dortmund, ambao ni mabingwa wa michuano hiyo mwaka 1997, walipata bao la kuongoza kutoka kwa Adrian Ramos na kuipiga Sporting Lisbon bao 1-0 na kujihakikishia nafasi hiyo ya 16 bora, baada ya kukusanya pointi 10 na kuwaaacha Real Madrid kwa pointi mbili.

Sevilla, ambao wamefanikiwa kunyakua taji la Ligi ya Europa misimu mitatu mfululizo, wako vizuri lakini wanaweza kuzidiwa na Lyon.

Klabu hiyo ya Hispania iliipa Dinamo Zagreb kichapo cha mabao 4-0, ambapo wafungaji walikuwa ni Luciano Vietto, Sergio Escudero, Steven N’Zonzi na Wissam Ben Yedder na kukaa kileleni mwa msimamo wa Kundi H wakiwa na pointi 10.

Katika kundi hilo, nao Juventus walikosa nafasi ya kuweza kusonga mbele hatua ya mtoano baada ya bao la kusawazisha la Lyon lililofungwa na Corentin Tolisso na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 mjini Turin na kuwa na pointi mbili nyuma ya Sevilla.

Sare hiyo inaifanya Lyon kuwa mawindoni, ambapo wakifanikiwa kupata pointi nne kwenye mechi mbili zilizobaki watatinga hatua ya mtoano.

Tottenham Hotspur ambao kwa sasa wanatumia Uwanja wa Wembley kutokana na dimba lao la White Hart kuwa kwenye ukarabati, hivyo na kuendelea kupata kipigo kwenye uwanja huo, baada ya kufungwa bao 1-0 na Bayer Leverkusen.

Spurs wameendelea kuwa na bahati mbaya na uwanja huo wa Wembley, baada ya kufungwa kwenye mechi yao ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Monaco.

Safari hii, klabu hiyo ya London ilipokea kichapo kwa bao la mbali la Kevin Kampl katika kipindi cha pili cha mchezo huo wa juzi Jumatano na kuwaacha Spurs pointi mbili chini ya klabu hiyo ya Ujerumani na pointi nne nyuma ya vinara wa Kundi E, Monaco.

Monaco ambao waliichapa Spurs kwenye uwanja huo wa Wembley, juzi Jumatano waliibamiza CSKA Moscow mabao 4-0, huku nyota wa Colombia, Radamel Falcao, aliyeshindwa kung’ara England kwenye klabu za Manchester United na Chelsea akipachika mabao mawili ambayo ndiyo mabao yake ya kwanza kufunga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya miaka sita kupita.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -