Tuesday, October 27, 2020

Lil Wayne & Birdman Baba na mtoto waliogeuka maadui

Must Read

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa...

LOS ANGELES, Marekani

HAKUNA asiyejua urafiki mkubwa uliokuwepo kati ya Lil Wayne na rapa mwenzake, Bryan Williams ‘Birdman’.

Wakati Birdman alipohojiwa na kituo kimoja cha redio alisema: “Ni mtoto wangu.  Kama ningekuwa naye hapa ningembusu. Nitaua kwa ajili yake, nitahangaika kwa ajili yake, na nitakufa kwa ajili yake.”

Kauli hiyo ya Birdman, anayetajwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 150, iliuthibitishia ulimwengu wa muziki wa hip hop ni jinsi gani marapa hao walivyoshibana.

Wafuatiliaji wa muziki wanafahamu kuwa Birdman ana mchango mkubwa kwenye mafanikio ya Lil Wayne.

Kwa lugha nyepesi, kupitia lebo yake ya Cash Money, Birdman ndiye aliyemfanya Wayne kuwa staa.

Inasemekana kuwa, baada ya baba mzazi wa Wayne kuitelekeza familia, ndipo Birdman alipoanza kuwa karibu naye.

Hata hivyo, mama mzazi wa Wayne, Jacida “Cita” Carter, hakuupenda ukaribu wa mwanawe na Birdman na hiyo ni kutokana na tabia za kihuni alizokuwa nazo mshikaji huyo.

Inadaiwa kuwa, Cita alikuwa akiyajua maisha ya kisela ya Birdman, kwani walisoma wote, hivyo hakutaka mwanawe apotee.

Hatimaye mwanamama huyo aliolewa na jamaa mmoja aitwaye Reginald McDonald “Rabbit” na ndiye anayetajwa kumshawishi mkewe huyo kumruhusu Wayne ajiunge na Cash Money ya Birdman.

Kama alivyokuwa Birdman, Rabbit naye alikuwa msela tu na wawili hao walikuwa wakifahamiana kitambo.

Kipindi hicho, Wayne alikuwa na umri wa miaka 11.

Baadaye Rabbit alipofariki kwa kupigwa risasi, kutokana na ugumu wa maisha, Cita alilazimika kuukubali urafiki wa Birdman na Wayne, ambaye aliacha shule na kujiunga na Cash Money. Hapo ndipo Birdman alipoanza kuwa ‘baba’ wa Wayne katika ulimwengu wa muziki.

“Nilikuwa naye nikimnoa na hata kwenda naye studio. Nilikuwa nikimweka ndani aandike mistari. Nilifanya hivyo kila siku,” aliwahi kusema Birdman.

Hata hivyo, hivi sasa Wayne, mwenye umri wa miaka 33 na Birdman (46) ni chui na paka. Licha ya historia hiyo nzuri ya uhusiano wao, katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiteka sehemu kubwa ya mzungumzo ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutokana na vita yao ya maneno.

Uswahiba wao ulianza kuyumba mwishoni mwa mwaka 2014, baada ya Wayne kukasirishwa na kitendo cha kuchelewa kutoka kwa albamu yake ‘Tha Carter V’.

Katika moja ya ‘posti’ zake katika mitandao ya kijamii, Wayne aliandika hivi: “Nataka kujitoa kwenye lebo (Cash Money) kwa sababu sina cha kufanya na hawa watu.

“Albamu yangu haijatoka na haitatoka kwa sababu Baby (Birdman) na Cash Money wamekataa kuiachia.”

Mbali na hilo, pia Wayne aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi kubwa, lakini Birdman alikuwa akimdhulumu mapato.

Ikumbukwe kuwa, madai kama hayo ya ‘mtonyo’ yaliwahi kutolewa na mastaa Juvenile, B.G. na Turk, ambao nao waliamua kuitema Cash Money.

“Birdman ni mtu hatari sana katika kusaka vipaji, lakini hajawahi kupenda kulipa watu. Unapokea kile anachotaka kukupa,” alisema Juvenile.

Akijibu shutuma hizo, Birdman alisema: “Hapa kuna nyumba ambayo unaweza kuishi, kuna magari unayoweza kuendesha. Ni ngumu kujua mmiliki halali wa mali hizi.

“Nimepata takribani mashitaka 20. Kuna watu wanahisi wana thamani kubwa kuliko wanachoingiza. Ndivyo biashara ilivyo.”

Wengi wamedai kuwa Wayne alikuwa akishindwa kudai stahiki zake kutokana na ukaribu alionao kwa Birdman.

Pia, Birdman aliibuka na kudai kuwa hakutegemea kama Wayne angempasukia hadharani kwa shutuma za uongo.

Katika ngoma yake ya ‘Sorry 4 the Wait 2’, ambayo hakumshirikisha msanii yeyote kutoka Cash Money, Wayne aliifananishya lebo hiyo na ‘bustani yenye nyoka’, akidai kuwa hakufanya kosa kujitoa.

Kwa mujibu wa Wayne, kwa kipindi chote alichokaa Cash Money, hakuwa ‘memba’ bali mfungwa.

Baadaye, Wayne aliifungulia mashitaka Cash Money Records, akiitaka kumlipa Dola za Marekani milioni 51 pamoja na kuvunja mkataba wake.

Aprili mwaka huu, gari alilokuwemo Wayne lilipunyuliwa na risasi, huku mtu aliyedaiwa kufanya uhalifu huo akitajwa kuwa ni rafiki mkubwa wa Birdman, Jimmy Carlton Winfrey.

Birdman alikanusha kuhusika kwenye tukio hilo na Winfrey alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

Mwaka jana, Birdman alimtambulisha Young Thug, ikiwa ni harakati zake za kuliziba pengo la Wayne pale Cash Money.

Lakini, Thug alizomewa na mashabiki wa Wayne katika sherehe ya kuachia albamu mpya.

Katika kile kinachosemekana kuwa ni kuchoshwa na ‘bifu’ za ajabu, ikiwemo vita ya maneno na bosi wake huyo wa zamani, tayari Wayne ameshatangaza kuachana na muziki.

“Kazi yangu ni kuhakikisha nastaafu nitakapofikisha umri wa miaka 35. Nistaafu nikiwa kijana ili niyafaidi maisha,” alisema Wayne.

Wakati Wayne alipokuwa akisherehekea kufikisha umri wa miaka 33, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Birdman aliposti picha iliyokuwa na ujumbe uliosomeka: “Happy BDAY kwa mtoto wangu.”

Katika hatua nyingine, wadadisi wa mambo wamedai kuwa hakuna uhakika kama meseji hiyo ya Birdman kwa Wayne imezika tofauti zao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -