Monday, November 30, 2020

LINDELOF KUTUA CHELSEA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Haya ndio mateso waliyoyapata United kutoka kwa Chelsea

LONDON, England

KATIKA maisha ya kawaida vitendo wanavyofanyiwa Manchester United na klabu ya Chelsea vinaweza kufananishwa na ubabe. Ambapo kwa kipindi kirefu sasa, matajiri hao wa London wamekuwa na desturi ya kuvamia dili na kumnyakua mchezaji anayefukuziwa na United kwa muda fulani.

Mapema wikiendi hii kuliibuka taarifa kuwa Chelsea wana mpango wa kumsajili beki wa Benfica, Victor Lindelof, ambaye kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa mwezi huu, vyombo vyote vya habari vilimpamba kuwa ni ‘beki mtarajiwa wa Manchester United’.

Lakini sasa tetesi zinamhusisha na Chelsea, klabu inayomilikiwa na tajiri la Kirusi, Roman Abramovich.

Chelsea walianza kama utani, wakaizoea na kuijenga kuwa tabia yao, kupokonya tonge mdomoni mwa United. Ni kama vile kuna ‘mfukunyuku’ pale Stamford Bridge ambaye ana kazi maalumu ya kunusa madili ya United.

Labda vinara hao wa ligi msimu huu watabadili tabia yao na kuanza kujenga kikosi chao kwa kusajili wachezaji bila kutegemea timu gani inamtaka mchezaji gani.

Lakini kwa vyovyote vile, kama Lindelof ataipiga chini United na kukubali kutua Chelsea, ataungana na orodha ya wachezaji hawa waliowahi ‘kugeuzia gia angani’…

 

Eden Hazard

Kabla ya Mbelgiji huyo kujiunga na Chelsea akitokea Lille mwaka 2012, Hazard alikutana na Sir Alex Ferguson ambaye alikuwa na shauku ya kumpeleka winga huyo pale Old Trafford.

Halafu Roman Abramovich akavamia shughuli ya watu!

“Nilizungumza na Abramovich, ni mtu ‘simpo’ anayependa soka,” alisema Hazard baada ya kujiunga na Chelsea.

“Vitu havikukaa sawa wakati wa mazungumzo baina yangu na hizo timu mbili, Chelsea na United, lakini kwa mawazo yangu Chelsea wana mipango mizuri sana. Tayari nilishaingia kwenye hatua zilizofuata katika mazungumzo, si kwa klabu moja bali ni zote sambamba na makocha wake.”

Duh! Kumbe kila mmoja alitupa ndoano yake, lakini bahati nzuri kwa wale wa darajani, samaki alinasa kwao.

Arjen Robben

Mwaka 2004, winga huyo wa Kidachi alishakubali kuondoka PSV na kutua United. Alibakisha nini zaidi ya kupanda pipa kutoka Uholanzi hadi uwanja wa ndege wa Hearthrow?

Yeye na baba yake walishatembezwa pale Old Trafford pamoja na uwanja wa mazoezi wa Carrington. Tayari walipewa uhakika kuwa Robben angepata nafasi ya kutosha ya kucheza.

Na kilichofuata…

“Nilikutana na Sir Alex Ferguson na mazungumzo yalifanyika vizuri,” anasema Robben na nilikuwa tayari kusaini mkataba. Lakini (Claudio) Ranieri na (Peter) Kenyon (Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Chelsea) walinifuata na kunielezea mengi kuhusu Chelsea, nikavutiwa na klabu yao. Sikuhuzunika kuikosa United kwa sababu kwenye soka mambo hubadilika haraka.”

Inatia hasira kidogo…

Pedro Rodriguez

Ukimuuliza shabiki wa Manchester United kitu chochote kilichowahi kumuudhi kumhusu Ed Woodward, watakwambia ni kwa sababu ya Pedro.

Agosti 2015, mwenyekiti msaidizi huyo alikwea pipa hadi Barcelona kukamilisha dili la uhamisho wa winga huyo wa Kihispania.

Mashabiki wote walifurahi kusikia hivyo na walikaa mkao wa kula kumsubiri mshambuliaji huyo, lakini hakuja tena!

Nani walivuruga dili? Kama kawaida walikuwa ni Chelsea. Wakaivuruga United, wakamvuruga Woodward na mashabiki wote.

Wakala wa Pedro aliibuka na kudai kuwa United ‘iliamua kuvuta shuka’ wakati wa kukamilisha dili lenyewe, huku Pedro naye akizungumzia hilo kwenye mkutano wa kuiaga Barcelona.

“Nilipata ofa kutoka kwenye klabu nyingine za England, Manchester United, City. Lakini Chelsea ndiyo iliyokamilisha dili kwani walionesha dhamira ya kunihitaji.”

Didier Drogba

Huyu ni mchezaji ambaye hadi kesho mashabiki wa United wakimkumbuka wanasikitika sana.

Achana na majina yote hayo hapo juu, iwapo United ingemnasa Drogba, ni wazi straika huyo angeifanyia mambo mazuri katikati ya miaka ya 2000.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Ivory Coast, alitakiwa mno na Sir Alex Ferguson kabla hajajiunga na Chelsea mwaka 2004.

“Tulifunga safari kwenda kumfuatilia alipokuwa Marseille,” Fergie aliandika maneno hayo kwenye moja ya vitabu vyake.

“Lakini timu yake hiyo ilihitaji kiasi cha pauni milioni 25 na Chelsea ikajisogeza, ikaua mchezo kabla hata hatujakaa chini kufikiria nini cha kufanya.”

Hapa United walionewa mno, kwani kwa kipindi hicho Wayne Rooney alikuwa moto wa kuotea mbali angali na umri mdogo tu. Hebu vuta picha, United ingekuwa na safu ya ushambuliaji yenye Drogba na Rooney…

John Obi Mikel

Hakuna asiyefahamu ishu hii ya Chelsea kuipoka United mchezaji ambaye walijua tayari wameshamnasa.

Kama hiyo haitoshi, Chelsea walimchukua mchezaji ambaye hakukubali tu kujiunga na United bali alishasaini na mkataba.

United ilikubali kulipa kiasi cha pauni milioni 4 kumsajili Mikel mwaka 2005, alipoanza kupigiwa upatu wa kuwa kiungo bora wa miaka ya baadaye kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 19.

Hadi dili la Mikel kutua Chelsea, kilipita kipindi cha mzozano baina ya klabu yake ya Lyn Oslo, Chelsea yenyewe na United.

Lakini Chelsea iliamua kumalizana nao kwa kuilipa United pauni milioni 12 pamoja na pauni milioni 4 kama fedha ya uhamisho kwa klabu ya Lyn.

Na sasa mashabiki wa United watakuwa na matumaini makubwa kwamba ishu ya Lindelof haianzi kuwasumbua kichwa baada ya Chelsea kutia maguu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -