Saturday, November 28, 2020

LIONEL MESSI ALICHEZA VIZURI, DYBALA ALIKUWA BORA ZAIDI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TURIN, Italia

MSHINDI mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi, alionesha kiwango safi licha ya klabu yake ya Barcelona kubamizwa mabao 3-0 na Juventus kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa usiku wa kuamkia jana jijini Turin.

Inakumbukwa kuwa, wakati Barca ikipoteza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya 16 bora dhidi ya PSG kwa kufungwa mabao 4-0, ilionekana kama vile nguvu ya ‘mchawi’ huyo wa soka inaanza kupungua, lakini kwa alichokifanya juzi pale Turin kinalifuta taratibu wazo hilo.

Aidha, pindi ambapo Juventus walicheza vizuri huku mbinu za kocha Maxmilliano Allegri zikizalisha matokeo ya kufurahisha kwao, walijiona ni watu wenye bahati kuepukana na madhara ya ufundi wa Messi usiku wa juzi.

Aliwafanya wachezaji wakongwe wa Juve, Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci pamoja na wenzao kutumia akili ya ziada kukabiliana na mienendo yake ya hatari.

Mienendo ya Messi kwa nyakati fulani ilitengeneza nafasi kwa wenzake, hasa kwa shambulizi la Luis Suarez lililookolewa kiustadi na mlinda mlango wa muda mrefu, Gianluigi Buffon.

Lakini licha ya juhudi zake zote za kuisaidia Barca, Juve walikuwa bora hasa Paulo Dybala aliyewazamisha mabingwa hao mara tano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mabao yake mawili dakika ya saba na 22 kipindi cha kwanza.

Huenda watu wakawa na sababu zao za kuanza kumfananisha Dybala na Messi na wengine wakagoma, lakini kwa kiwango cha hali ya juu alichokionesha juzi ni kwamba Dybala sasa amejitangaza mwenyewe kama ni mchezaji mwenye kipaji ambacho ipo siku watu wote watakubaliana kuwa ndiye Messi mpya na kumrithi jumla ndani ya Barca na timu ya Taifa ya Argentina.

“Nilipokuwa mtoto nilikuwa na ndoto za kufanya mambo makubwa kama haya,” alisema Dybala mara baada ya mchezo kumalizika.

“Leo (juzi) nimetimiza kwa vitendo. Kilikuwa ni kiwango bora. Tulitambua jukumu letu ni kupata ushindi bila kufungwa bao lolote na tumetimiza,” alisema.

Uwezo huo aliouonesha straika huyo uliendana na kauli iliyowahi kutoka kwenye kinywa cha mkongwe wa Barca, Xavi, kuwa Dybala mwenye umri wa miaka 23 ni mchezaji sahihi kwao na mwenye kipaji ambacho kipo tayari kutumika Nou Camp ingawa kwa sasa inaonekana kama hakuna nafasi ‘ya kazi’ katika kikosi cha Barcelona, lakini haitadumu kwa muda mrefu.

Kiujumla, Barca ilihitaji umoja wa kila mchezaji katika mchezo wa juzi na si ubora wa Messi pekee.

Watu wengine walio kando yake, Suarez alitakiwa kuwa mshambuliaji kuliko kuchuana na watu kama Chiellini, Neymar pia alitakiwa kuwa makini mchezoni kama ilivyokuwa dhidi ya PSG.

Labda hakuwa sawa kwa sababu ya kuoneshwa kadi nyekundu dhidi ya Malaga na ataukosa mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid Aprili 23, mchezo utakaoamua nani bingwa wa La Liga.

Kuna mazungumzo yanayoendelea pia kwamba umri nao ni tatizo kwa washambuliaji wa Barca. Ni kweli, Messi atafikisha miaka 30 Juni mwaka huu, huku Suarez yeye tayari alishavuka umri huo Januari mwaka huu. Neymar ndiye mdogo wao mwenye miaka 25.

Na kwa kuwa kocha Luis Enrique ataondoka mwishoni mwa msimu huu, ni wazi kocha mpya wa Barca atahitaji kitu kipya kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo, Dybala? Huyo atawafaa.

Wakati huo huo, Juventus watapenda kubaki naye huku pia Dybala mwenyewe akinukuliwa hivi karibuni kuwa ana furaha hapo kwa muda mwingine.

“Nina furaha hapa, nakaribia kusaini mkataba mpya hivi karibuni na nipo tayari kuisaidia timu,” alisema.

Lakini bado kuna kila dalili za kumuona Dybala akiondoka muda wowote ule, kwa sababu historia itawahukumu Juve kuhusu kuuza mastaa, Zinedine Zidane mwaka 2001 na Paul Pogba msimu huu.

Zaidi ya yote, huyo ndiye Dybala aliyesajiliwa akiwa bado kinda kwa dau la euro milioni 32  kutoka Palermo Juni 2015, masaa kadhaa kabla Juve haijaivaa Barca fainali ya UEFA na kufungwa mabao 3-1.

Misimu miwili baadaye, akaiongoza Juve katika hatua ya kwanza ya kulipiza kisasi cha fainali ya Berlin. Akang’ara ndani ya uwepo wa Messi.

Ni mastaa wawili ambao siku yao ya kwanza ya kuanza kusakata kabumbu la kimataifa wakiwa Argentina waliwahi kuoneshwa kadi nyekundu, lakini usiku wa juzi walikuwa watu tofauti kabisa.

Dybala akiibeba Juve mgongoni kwake, Messi akijaribu kulivuta gari la Barca kwa kutumia ‘uchawi’ wake. Dunia ya soka ilitikiswa na jina la Messi, lakini Dybala ameanza kutikisa na ataendelea zaidi.

Lakini, inabidi ikumbukwe kwamba, Messi alipokuwa na miaka 23 tayari alishatambulika kama mchezaji bora duniani, kitazame tena kiwango chake cha juzi utakumbuka zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -