Tuesday, October 27, 2020

LIONEL MESSI AWASHTUA MABEKI BARCELONA

Must Read

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu...

CATALONIA, Hispania

NAHODHA wa timu ya Barcelona, Lionel Messi, ametoa angalizo kwa safu ya ulinzi ya vigogo hao wa La Liga, akiitaka iimarishe kiwango baada ya kushuhudia wakilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Bilbao.

Messi alianzia benchi katika mchezo huo kabla ya kuingia kipindi cha pili na kutengeneza bao la kusawazisha, lakini Barca ilishindwa kuepuka kupoteza pointi muhimu kwa mara ya tatu mfululizo.

Kwa kiasi kikubwa, uamuzi wa kocha wa Barca kutomwanzisha Messi ulionekana kuigharimu timu hiyo, licha ya kwamba alipanga kumpumzisha fowadi wake huyo kwa ajili ya mtanange wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Tottenham, utakaochezwa keshokutwa.

Lakini, Messi alisema kwamba Barca bado ipo vizuri ingawa safu ya ulinzi inatakiwa kuimarishwa zaidi.

“Ndio kwanza tupo mwanzoni mwa msimu. Wengi wetu leo tulitawaliwa na hasira juu ya matokeo ya mechi mbili zilizopita.

“Kwa sasa tunatakiwa kuimarisha safu ya ulinzi ili tusifungwe mabao kila mara,” alisema Messi.

Hadi hivi sasa Barca ina takwimu ya kutofungwa bao katika mechi moja tu kati ya tano zilizopita, ambayo walishinda mabao 4-0 dhidi ya PSV kwenye Ligi ya Mabingwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya...

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina ya mpira unaocheza kwa sasa...

Mtibwa yaitungua Azam Jamhuri, Prisons yazidi kupeta

NA GLORY MLAY TIMU ya Azam FC imepoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana baada...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -