Friday, December 4, 2020

LIPULI FC MTARAJI KUKUTANA NA HAYA VPL

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAINAB IDDY

LIPULI FC ya mkoani Iringa imekuwa timu ya kwanza kujiwekea nafasi katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania katika msimu ujao wa 2017/18.

Timu hiyo imekata tiketi ya kushiriki ligi kuu msimu ujao baada ya Jumamosi iliyopita kufanikiwa kupata ushindi wa  3-1 dhidi ya Polisi Dar na kufikisha pointi 29, ambazo haziwezi kufikiwa  na timu yoyote ile katika kundi A walilokuwapo.

Katika mchezo huo, mchezaji wa zamani wa Simba, Salumu Machaku, ndiye aliyeing’arisha Lipuli baada kuifungia mabao mawili huku jingine likifungwa na Ramadhan Madege.

Wakati Lipuli ikiwa imeshakata tiketi katika ligi kuu, hivi sasa zinasubiriwa timu za kundi C na B ambapo kutoka B, Polisi Moro, Mji Njombe  na KMC zinaonekana kuchuana vikali huku C ipo vita kati ya Singida United, Rhino Ranges na Alliance Academy.

Kwa upande wa Lipuli, imefanikiwa kupanda ligi kuu ikiwa ni baada ya takribani miaka 19 iliyopita tangu iliposhuka na kuanza kushiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Wadau wengi wa soka wanaimani kuwa kupanda daraja kwa Lipuli ni nafasi nyingine kwa Mkoa wa Iringa kuleta soka la ushindani kwa klabu kongwe za Simba na Yanga, ambazo zinaonekana ndio miamba ya soka la Tanzania.

Kwa kufahamu uzito na ugumu wa ligi kuu, BINGWA linabainisha mambo kadhaa ambayo timu ya Lipuli inapaswa kujiandaa kukutana nayo kwenye ligi hiyo ambayo kila mwaka yamekuwa yakipigiwa kelele na wadau wa soka lakini yameonekana kuwa donda ndugu.

 

Ratiba ngumu inayopanguliwa wakati wowote

Kwenye Ligi Daraja la Kwanza, Lipuli ilipata mteremko pengine kwani ratiba ya ligi hiyo haikukumbwa na panguapangua yoyote. Lakini pia Lipuli ilipata ubwete kwa kupangiwa mechi nne za mwisho kucheza nyumbani.

Kwenye ligi kuu hilo wasilitarajie, utulivu wa ratiba, pangua pangua za tariba zipo sana na hufanyika kutokana na kutokuwa na mipango mikakati ya kuendesha ligi ya Tanzania inayofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

 

Mbeleko ya TFF inaishia hapo hapo

Kumekuwa na malalamiko mengi kwamba Lipuli imebebwa kuingia ligi kuu. Lakini kwa namana yoyote hata kama timu hiyo ya Iringa imepanda kwa nguvu zake, lazima ifahamu kwamba kubebwa bebwa kwa timu za aina yake mwisho ni Ligi Daraja la Kwanza tu.

Kwenye ligi kuu, TFF, Bodi ya Ligi na wadau wengine akili zao ziko kwa Simba na Yanga tu. Hadi sasa Lipuli inatajwa kama ni moja ya matawi ya Simba licha ya kwamba mmoja wa wajumbe wa TFF, Ayoub Nyenzi, kuwa mdau mkubwa wa Lipuli ambaye pia alishawahi kuwa kiongozi wa Yanga.

Kwa hiyo, Lipuli lazima mtakutana nalo hapa na pale inapotokea mmeingia kwenye mgogoro na timu za Simba na Yanga, msitarajie mbeleko ya TFF kabisa.

Si ajabu kuona wakipewa ushindi wa kesi fulani dhidi ya timu nyingine ndogo kwa kuwa tu TFF ina maslahi binafsi ya klabu hizo, lakini pia hata viongozi wake wengi wapo katika kamati mbalimbali ndani ya shirikisho hivyo ni vigumu kutoa hukumu halali pale zinapoonekana kupepesa macho.

Katika hilo, mfano mzuri ni ishu ya Polisi Dar dhidi ya Simba, pale walipomtumia Novatus Lufunga akiwa na kadi nyekundu.

Waamuzi wa VPL si rafiki wa timu ndogo

Lipuli pengine si timu ndogo, lakini haina ukubwa kama Yanga, Simba na Azam kwa sasa. Kama waamuzi walikuwa marafiki wa Lipuli katika Ligi Daraja la Kwanza, msilitegemee hilo katika ligi kuu.

Katika VPL ndiko kwenye uchafu mkubwa zaidi na uhuni wa waamuzi, kwani si ajabu kukuta mwamuzi anapindisha sheria 17 za mchezo kwa maslahi na mapenzi yake kwa timu fulani.

Katika hili Lipuli mjiandae kuona michezo yenu mingi waamuzi kwanza wakibadilisha pengine kabla ya mchezo, au wakiwauma na kuwageuka kama hawawajui licha ya kwanza walikuwa marafiki zenu kwenye Ligi Daraja la Kwanza.

Wachezaji, viongozi wenu kuwa maduka

Si waamuzi na TFF pekee wanaoweza kuwaumiza kwa ratiba au kupindisha sheria za soka, lakini hata hao wachezaji na viongozi wenu ambao wamepambana kufa au kupona na kuwapandisha daraja wanaweza kuwageuka ndani ya dimba na nje ya dimba.

Timu kadhaa zimefukuza wachezaji na wengine kusimamishwa kutokana na kuwatuhumu wachezaji hao kuuza mechi, au kuwaambia wamecheza chini ya kiwango dhidi ya timu fulani hasa hizo kongwe za Kariakoo.

Viongozi wa timu wana itikadi zao na miamba hiyo ya Kariakoo, si ajabu mkawa mmepata msaada kutoka kwa baadhi ya viongozi wa timu hizo hivyo kuwalipa fadhila ni kuwapa pointi tatu wanapozihitaji. Timu kadhaa zimekuwa zikikumbwa na hili na wakati mwingine kujikuta zikiwa kwenye mazingira magumu na nyingine zinashindwa kuhimili mikikimikiki ya VPL na kujikuta zikishuka msimu unaofuata.

Upinzani wa kugombea wachezaji

Kwa sasa Lipuli mnaweza kuwa na wachezaji wenu mnaotaka kuendelea nao lakini mjiandae kwenye mzunguko wa pili kupokonywa wale wote watakaoonyesha kiwango cha ushindani uwanjani.

Mara nyingi kwenye usajili wa dirisha dogo, ndipo zinapofanyika figisu figisu za kuwachukua wachezaji kutoka katika timu zinazoonekana kuwa tishio kwa lengo la kuzidhoofisha katika mzunguko wa pili. Usajili mwingine kufanyika kwa makusudi hata kama timu haina nafasi ya kumpa mchezaji kucheza hilo lipo.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -