Friday, December 4, 2020

LIPULI, SINGIDA ZITAKOLEZA USHINDANI MSIMU UJAO?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MARY PETER

LIPULI na Singida United zimefanikiwa kurejea msimu ujao wa ligi kuu huku Njombe Mji ikipanda daraja kwa mara ya kwanza zikitokea Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Timu hizo zimepata nafasi ya kushiriki ligi kuu baada ya kuongoza katika makundi yao na sasa zinaungana na nyingine13 ambazo zitajihakikishia kubaki kwenye ligi hiyo.

Lakini wakati timu hizo zikijiandaa kushiriki ligi hiyo, timu tatu zinatarajia kurudi kucheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara ambazo zitashuka daraja katika msimu huu.

Timu kama JKT Ruvu, Majimaji  zinaonekana kupoteza mwelekeo wa kuendelea kubaki kwenye ligi hiyo kutokana na kufanya vibaya mechi zao nyingi.

Kwa timu kama Majimaji ni kawaida kupanda na kushuka kwani tangu ilipopanda daraja katika miaka ya 80, yatari imeshuka zaidi ya mara nne.

Binafsi sitashangaa timu zilizopanda daraja msimu huu wa Ligi Daraja la Kwanza zikacheza msimu mmoja wa ligi kuu kutokana na kushindwa kuhimili mikikimikiki.

Sitaona ajabu kwa timu hizo kurejea Ligi Daraja la Kwanza kutokana na viongozi wake kushindwa kufanya maandalizi yenye tija ambapo wanatumia nguvu kubwa kuzipandisha.

Timu kama JKT Oljoro iliyokuja na ushindani wa hali ya juu ya soka katika miaka mitano iliyopita ya ligi kuu, imepotea na sasa inashiriki Ligi Daraja la Pili baada ya kukumbwa na kashfa ya kupanga matokeo katika mchezo wa Kundi C, msimu uliopita.

Lakini kuna timu ambazo sasa zimebaki jina kama Reli ya Morogoro ‘kiboko ya vigogo’, Ushirika Moshi, Vijana Ilala,  Sigara ya Dar es Salaam, Manyema ‘mkuki wa simu’ haziko tena ligi kuu baada ya kushuka daraja.

Timu nyingine kama African Sports ya Tanga iliyotumia nguvu kubwa kurejea ligi hiyo, msimu wa 2014 wa Ligi Daraja Kwanza iliwashangaza mashabiki baada ya kucheza msimu mmoja wa 2015/16 na kurejea ilikotoka.

Ilishangaza zaidi pale African Sports ilipoungana na wapinzani wao wa jadi Coastal Union na Mgambo Shooting kushuka msimu mmoja kutokana na kushindwa kufanya maandalizi mazuri.

Msimu huu tunatarajia kuziona timu za Lipuli, Singida United na Njombe Mji zinazotumia nguvu nyingi  kurejea ligi hiyo, kufanya vizuri ili ubingwa wa Tanzania usibaki kwa Simba na Yanga.

Tunatarajia kuona ushindani wa kweli kutoka  kwa timu hizo tatu ili msimu ujao wa 2018/19 ziweze kutuwakilisha kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara au michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), ambapo mshindi wake wanapata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Naamini timu hizo zikijipanga vizuri kuanzia usajili wa wachezaji na benchi nzuri la ufundi, uongozi na mshikamano wa mashabiki wao zinaweza kutimiza malengo yao.

Mashabiki wengi wa soka wanataka kuona timu hizo zikikoleza ushindani wa kweli wa soka utakaofanya kuendelea kubaki kwa muda mrefu kwenye ligi hiyo.

Hatutarajii kuona tena timu hizo zikishuka kwa kipindi kifupi kwa kisingizio cha kukosa fedha au mahitaji muhimu kwa wachezaji kwa kuwa zimepanda kwa lengo moja la kuendeleza soka la Tanzania.

Ni wakati wa timu hizo kuanza maandalizi mapema ili kujiweka fiti na misukosuko ya ligi kuu ili ziweze kupata matokeo mazuri.

Utakuwa ni msimu mbaya kwao kama watasubiri hadi dakika za mwisho kufanya maandalizi, kwani uzoefu unaonyesha kuwa timu nyingi zinashindwa kuhimili mikikimikiki kutokana na maandalizi duni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -