Wednesday, January 20, 2021

Liver vs Man Utd… Mourinho kwa Klopp kama mkate na chai

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MERSEYSIDE, England

MCHEZO wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool na Manchester United kwenye Uwanja wa Anfield, Jumatatu ijayo, mtandao wa Sky Sports umeangalia rekodi za kocha Jurgen Klopp na Jose Mourinho.

Makocha hao wawili wamekwishakutana mara tano wakati huo Mourinho akiwa Real Madrid na Klopp akiinoa Borussia Dortmund.

Mchezo huo wa Jumatatu mjini Merseyside, utakuwa ni wa kwanza kwa wawili hao kukutana mmoja akiwa kocha wa Liverpool (Klopp) na mwingine wa United (Mourinho).

Je, nani ni mbabe kati ya makocha hao wawili?

Dortmund 2-1 Real Madrid (Ligi ya Mabingwa Ulaya Kundi D, Oktoba 2012)

Kwa mara ya kwanza Klopp na Mourinho kukutana ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi miaka minne iliyopita wakati Borussia Dortmund na Real Madrid zilivaana.

Klopp alimchapa mpinzani wake huyo katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Westfalenstadion kwa mabao ya mshambuliaji, Robert Lewandowski na beki wa kushoto, Marcel Schmelzer, bao la kufutia machozi la Real lilifungwa na Cristiano Ronaldo.

Baada ya mchezo huo, Klopp alizungumzia mbinu alizotumia kumzidi Mourinho akisema: “Walichezea sana mpira, ila hilo halikuwa baya kwetu.”

Real Madrid 2-2 Borussia Dortmund (Ligi ya Mabingwa Ulaya Kundi D, Novemba 2012)

Haikuchukua muda mrefu makocha hao wawili kukutana tena, wakati Madrid walipoikaribisha Dortmund kwenye mechi ya marudiano ya Kundi D kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Lakini bado ‘Special One’ alishindwa kumfunga Klopp baada ya kutoka sare ya 2-2 mjini Madrid, Hispania, Los Blancos walifanikiwa kupata bao dakika za majeruhi lililofungwa na Mesut Ozil kwa mpira wa adhabu na kuisaidia timu hiyo kupata pointi.

Hivyo Mourinho alipata somo kubwa kwa mechi ambazo anakutana na Klopp, baada ya kocha huyo wa Ujerumani kukiongoza kikosi hicho cha Bundesliga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kabla ya mapumziko.

Wakati wote wamefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano, lakini Klopp ndiye aliibuka kidume baada ya kuwa vinara wa kundi hilo na Real kushika nafasi ya pili.

Borussia Dortmund 4-1 Real Madrid (Ligi ya Mabingwa Ulaya nusu fainali ya kwanza, Aprili 2013)

Miezi mitano baadaye makocha hao maarufu walikutana tena, msimu huo ambao fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja Wembley.

Katika mchezo huo, Dortmund walitakata baada ya mabao manne kutoka kwa mshambuliaji wao Lewandowski, ingawa hadi dakika tano za kipindi cha pili timu hizo zilikuwa hazijafungana.

Mourinho aliweka wazi hisia zake baada ya kipenga cha mwisho, akisema: “Timu yangu imekosa uzoefu mpaka Lewandowski anafunga mabao manne bila hata ya kuchezewa rafu japo mara moja.”

Real Madrid 2-0 Borussia Dortmund (Ligi ya Mabingwa Ulaya nusu fainali ya pili, Aprili 2013)

Wakati wa maandalizi wa mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, mechi hiyo ndiyo ilikuwa ikiamua hatima ya Mourinho kwenye klabu hiyo ya Real, hofu ilionekana kuwa juu kati ya makocha hao wawili.

“Nimezungumzia kidogo kuhusiana na Dortmund na hiyo inatosha. Tangu ratiba ilipopangwa, Klopp amekuwa akichonga sana,” alisema Mourinho kabla ya mechi hiyo.

Kocha wa Dortmund, Klopp alikuwa mtulivu, akisema: “Mourinho anasema nachonga sana? Hivyo ndivyo mmoja wa walimu wangu alivyokuwa akiniambia kila mara. Hivyo sijali, sifikirii hilo kabisa.”

Na alipoulizwa labda hiyo ilikuwa ni sehemu ya mbinu zake kuzungumza sana, Klopp, aliongeza: “Mimi si mtu mwenye akili sana kujua hilo inakuwaje. Lakini hakuna tatizo, sasa nitanyamaza na kila kitu kitakwenda sawa.”

Pamoja na Mourinho kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika mechi zao nne walizokutana, kocha huyo wa Ujerumani alikuwa akitabasamu wakati wote, ambapo pamoja na mabao mawili yaliyofungwa na Karim Benzema na Sergio Ramos, ulikuwa ni uchungu mtamu kwa Klopp, ambaye alitinga fainali kwa kushinda jumla ya mabao 4-3 kwa mechi zote mbili. Klopp alicheza fainali alifungwa kwenye fainali na Bayern Munich na baada ya msimu huo, Mourinho aliondoka Madrid.

Chelsea 1-3 Liverpool (Ligi Kuu England, Oktoba 2015)

Oktoba mwaka jana, Klopp akiwa Liverpool alishinda mechi yake ya tatu kati ya tano walizokutana na Mourinho, ambaye wakati huo alikuwa akiinoa Chelsea.

Wakati huo Chelsea wametoka kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England, lakini walikuwa wakihangaika kujinasua kutoka chini ya msimamo wa ligi hiyo baada ya mechi 10 na Klopp aliongeza matatizo kwa hasimu wake huyo kwa kuiongozea Blues kipigo cha sita kwenye msimu huo.

Ingawa mechi hiyo ilianza vizuri kwa kikosi hicho cha Mourinho kupata bao la kuongoza lililofungwa na Ramires, lakini mambo yaliharibika baada ya Philippe Coutinho kupiga bao dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Nyota huyo wa Brazil, Coutinho aliongeza bao lingine kabla ya Christian Benteke kufunga la tatu.

Baada ya mechi kumalizika, Klopp alionekana kumhurumia mpinzani wake, akisema: “Mambo kama hayo yanatokea.”

“Nilikumbana na hali kama hiyo wakati nikiwa Dortmund. Kitu kizuri ni kwamba hakuna mtu kwenye klabu hiyo aliyekuwa na wasiwasi kuhusiana na hali yangu. Namhurumia sana, ila ndio mambo ya soka.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -