Thursday, December 3, 2020

LUFUNGA AITIA SIMBA MATATANI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA

Simba imeingia matatani baada ya timu ya Polisi Dar kuwasilisha rufaa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupinga kuchezeshwa kwa beki wao, Novat Lufunga, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) akiwa na adhabu ya kadi nyekundu.

Kanuni ya 22 ya michuano hiyo ya FA inayohusu nidhamu na udhibiti wa wachezaji, inasema masuala yote ya nidhamu yatatumia kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kanuni ya nidhamu ya ligi kuu inasema mchezaji akipewa kadi nyekundu kwenye mechi, atatumikia kadi hiyo kwenye mechi ijayo.

Kama kadi hiyo ni katika mechi ya mwisho ya msimu basi ataitumikia kadi hiyo kwenye mechi ya kwanza ya msimu ujao wa michuano ya FA.

Hivyo baada ya Lufunga kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya Aprili 11 mwaka jana dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali na kutolewa kwa kuchapwa mabao 2-1, mchezaji huyo alitakiwa kutumikia adhabu kwenye mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Polisi Dar.

Katika mchezo huo, Lufunga alimchezea rafu Ally Shiboli wa Coastal Union ndani ya 18 na kusababisha penalti ambapo mwamuzi wa mchezo alimtoa kwa kumpa kadi ya pili ya njano.

Lakini Lufunga alikuwamo benchi katika mchezo dhidi ya Polisi Dar, ambao Simba walishinda mabao 2-0.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas, alikiri kupokea barua hiyo na kusema kwamba Kamati ya Mashindano inatarajiwa kukaa leo ili kupitia rufaa hiyo ya Polisi Dar.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -