Friday, October 30, 2020

Luis apiga ‘hat-trick’ Simba ikiua 6-0 Arusha

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA VICTORIA GODFREY

WINGA hatari wa Simba, Luis Miquissone, amefunga mabao matatu (hat-trick), wakati kikosi cha timu hiyo kilipoichapa Arusha FC mabao 6-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Ihefu katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL2020/21) utakaopigwa Septemba 6, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya,

Kwa upande wao, Arusha FC wapo katika maandalizi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao unatarajiwa kuanza Oktoba mwaka huu.

Katika mchezo wao huo wa jana, Simba ilianza kuliona lango la Arusha FC dakika ya 5 baada ya Meddie Kagere kuifungia bao kwanza kabla ya kiungo Larry Bwalya kufunga bao la pili dakika ya 24.

Dakika ya 34, Kagere aliziona nyavu za AFC kwa kuifunga Simba bao la tatu na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Katika kipindi cha pili, Simba iliendeleza umwamba kwa kujipatia bao la nne kupitia Luis aliyecheka na nyavu dakika ya 76 , kabla ya winga huyo machachari kuongeza la tano dakika ya 80.

Luis alifunga bao lake la tatu dakika ya 88, likiwa ni la sita kwa Simba na kuifanya timu hiyo kutoka uwanjani na ushindi huo mnono wa mabao 6-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha wa timu ya Arusha FC, Abdallah Juma, alisema kuwa lengo lao lilikuwa ni kuwapa fursa wachezaji wake kucheza na timu kubwa kwani hawakuwahi kukutana na Simba.

Alisema kuwa pia alilenga kupata picha ya kikosi chake kuelekea kambi yao watakayoianza rasmi siku chache zijazo.

Kocha huyo alisema kuwa kwa jinsi vijana wake walivyocheza jana, kuna kitu ambacho amekiona akiamini hata vijana wake hao watakuwa wamejifunza mengi kupitia Simba.

“Simba nao kuna kitu wamekipata kutoka kwetu sio kwamba walivyofunga mabao sita kwa urahisi sana,” alisema Juma.

Akizungumzia kuhusu maandalizi yao kwa ujumla, alisema kuwa muda uliobaki unaweza kumsaidia kuinganisha timu kutengeneza  umoja miongoni mwa wachezaji wake.

“Jana (juzi) asubuhi ndio nimekutana na wachezaji, lakini leo (jana) tumecheza, kuna timu zinakaa muda mrefu na zinacheza na Simba,  zinafungwa mabao mengi. Nawapa hongera wachezaji wangu na timu itakuwa nzuri. Wana-Arusha waache kutengana, bali tuungane kupambania timu yetu,” alisema kocha huyo. 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -