Friday, December 4, 2020

Luis azua hofu Simba

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ZAINAB IDDY NA FAUDHIA RAMADHAN

NYOTA wa Simba, Luis Jose Miquissone amezua hofu ndani ya klabu hiyo, kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Winga huyo ndiye aliyebeba ‘roho’ za Wanasimba kwa sasa kutokana na kiwango chake, hasa wanapoifikiria mechi ya Jumapili.

Wekundu wa Msimbazi hao, wanaamini iwpao Luis atakuwa fiti siku hiyo na kucheza katika kiwango chake, Wanajangwani ‘wataita maji mma’ kutokana na kile atakachowafanyia.

Jeuri hiyo ya wapenzi wa Simba inatokana na kile alichokionyesha Luis ndani ya mechi tatu zilizopita za Simba, akiwachachafya mabeki wa timu pinzani, kufunga mabao na manjonjo ya kila aina.

Mathalani, katika mchezo wa juzi dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa Taifa, Luis alijikuta akishangiliwa kama mfalme wakati anatoka dimbani baada ya kufunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa 2-0.

Na sasa wakati mashabiki wa Simba wakisubiri kwa hamu kumuona Luis atakavyowatesa Yanga Jumapili, kuna tukio amelifanya ambalo linahatarisha kumweka nje ya uwanja.

Katika mchezo wa juzi, Luis alishangilia bao lake la pili lililotokana na mpira uliopigwa na Deo Kanda dakika ya 71 kwa kuruka kwa kujipindua (samasoti), kitendo kinachoweza kumfanya kuwa majeruhi.

Mara alipotua juzi, alionekana wazi kuugulia maumivu japo alijikaza na kuendelea kushangilia na wenzake.

Ikumbukwe kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aliwahi kumjia juu mshambuliaji wake, Luis Nani kutokana na staili hiyo ya ushangiliaji.

Nani alifanya hivyo baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya FC Shenzhen kutoka China mwaka 2007, ikiwa mechi ya maandalizi ya msimu mpya.

Ferguson alionekana kuwa mbogo kwa mchezaji wake huyo na kumtaka kuacha kabisa ushangiliaji huo kwani uneweza kumletea madhara siku za usoni.

“Tunafahamu Nani ni mchezaji mzuri, kila mtu anatamani kumuona akifunga mabao mengi, lakini kuhusu hili (ushangiliaji), hapana sijapenda,” alinukuliwa Ferguson.

Kwa upande wake, Daktari wa Simba, Yassin Gembe, alisema kitendo alichokifanya Luis si kibaya, lakini kina madhara makubwa ikitokea amekosea hesabu wakati akirudi chini.

“Kwa wanamichezo, najua inaweza kuwa vigumu kukosea kile alichokifanya kutokana na mazoezi ya mara kwa mara wanayoyafanya tofauti na mtu ambaye hana mazoezi, lakini lazima wajue wanahatarisha afya zao pale anapokosea mahesabu.

“Hatuombei itokee, lakini kama akikosea kutua chini, anaweza kuumia maeneo ya kichwa, uso na hata kutenguka mikono au miguu, lakini pia pale atakapotua, anaweza pia kukutana na vitu hatarishi kiafya, mfano wa mawe, chupa, mitaro hasa maeneo ambayo alifanya lile tendo,” alisema.

Gembe alimshauri Luis na wachezaji wengine wanaopenda kuruka samasoti kutofanya hivyo kwani kunahatarisha afya zao na huenda wakazigharimu timu.

“Nawashauri wachezaji wote wasipende sana kufanya mambo ambayo yataweza kuhatarisha afya zao kwa sababu kama ingetokea amekosea mahesabu ya kurudi ardhini, ni wazi ataumia na kuchukua muda mrefu kupona tatizo ambalo amejisababishia.

“Tunajua katika mpira kuna mambo yanahatarisha maisha ya mchezaji kama kukatana mitama, kupigana viwiko, kugongana vichwa na vingine vingi vinavyotokea uwanjani, lakini visiwe ni vya kujitengenezea mchezaji mwenyewe kwa sababu huchukua muda mrefu kupona na kurejea uwanjani,” alisema Gembe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -