Wednesday, October 28, 2020

Lulu ni mke mtarajiwa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HABARI ZOTE NA ZAITUNI KIBWANA

MWIGIZAJI wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, juzi aliwaacha mashabiki wake kwenye maswali mengi baada ya kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kumpa hongera kwa kufanikiwa kuvishwa pete ya uchumba.

Lulu, ambaye kwa sasa ameamua kutoweka kitu chochote kwenye ukurasa wake wa Instagram,  inasemekana amevalishwa pete ya uchumba na mchumba wake wa muda mrefu, DJ Majizo.

Mwanamitindo, Martin Kadinda ndiye aliyeanza kutoa pongezi hizo kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika: “Hongera Lulu,” jambo lililoacha maswali mengi kwa mashabiki wake.

Mbali na Kadinda, pia mashabiki wengine kwenye ukurasa huo huo waliendelea na pongezi, huku wengine wakiamua kumpa wosia Lulu wa kumtaka kuwa mke bora.

“Najua kila mtu atakupa hongera, ila mimi nakushauri kama kweli wewe ni mke wa mtu mtarajiwa basi nakupa wosia kuwa lazima ubadilike ili uwe mke bora,” alisema.

Lulu, ambaye kwa siku za karibuni haonekani kwenye mitandao ya kijamii, licha ya pongezi hizo ambazo baadhi alikuwa akizijibu, alishindwa kuthibitisha kama kweli ni mke mtarajiwa au la.

“Mimi kwa sasa napatikana kwenye barua pepe tu, yaani niandikie barua na itafika, lakini huku mimi sipo,” alijibu Lulu kwenye ukurasa huo wa Martin Kadinda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -