Saturday, November 28, 2020

Lwandamina aanza kuisuka Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

MABADILIKO ya benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga, bila shaka yanaandamana na mabadiliko kadhaa kwenye kikosi cha timu hiyo. Huo ndio ukweli kwani kocha mpya wa mabingwa hao watetezi, George Lwandamina, tayari ameshaanza kupangua na kupanga kikosi chake kipya.

Kocha huyo ambaye anatarajiwa kuja kuinoa Yanga mwanzoni mwa mzunguko wa pili mwezi Januari, ameshaanza kuwavuta nyota wake kutoka kwenye kikosi cha Zesco United na kutua nao Jangwani katika usajili wa dirisha dogo.

Tayari Lwandamina amewalengesha Yanga kwa kiungo mkabaji mahiri wa Zesco aliyewasumbua sana Waarabu na kuacha gumzo katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Misheck Chaila.

BINGWA lilikuwa la kwanza kuripoti juu ya Wanajangwani kufanya mazungumzo na Chaila na sasa linakuletea habari mpya kuwa mambo safi kwani kila kitu kimeeleweka baina ya pande hizo mbili.

Yanga wamefikia uamuzi wa kumleta  kiungo huyo namba sita baada ya muda mrefu kukabiliwa na tatizo hilo kwenye kikosi chao na hivyo kulazimika kumtumia kiraka Mbuyu Twite ambaye kwa sasa anaonekana kuelemewa na majukumu uwanjani.

Mbali na Twite, Yanga imejaribu pia kuwatumia Said Makapu, Thaban Kamusoko pamoja an Salumu Telela kabla ya kumaliza mkataba wake na kujiunga kwenye kikosi cha Ndanda FC, lakini bado tatizo hilo limeshindwa kupata tiba sahihi.

Taarifa ambazo BINGWA limezipata zilizothibitishwa na kiungo huyo mwenyewe kutoka Zambia, zinasema kuwa wamefikia mwafaka wa mazungumzo yake na Yanga na tayari taratibu za kuja nchini kuingia kandarasi ya miaka miwili imeshafanyika.

Alisema hivi sasa uongozi wa Yanga upo katika mazungumzo na Zesco kutokana na kuwa na mkataba wa mwaka mmoja uliobaki kati ya mitatu aliyopewa, lengo likiwa kumnunua ili aje kuanza kazi kwa Wanajangwani katika ligi mzunguko wa pili utakaoanza Desemba 17 mwaka huu.

“Wamefikia mwafaka na meneja wangu na kukubaliana nije Tanzania Novemba 15, kusaini mkataba wa miaka miwili kwani hivi sasa Yanga wapo kwenye mazungumzo na Zesco ili kumalizana juu ya gharama za usajili wangu.

“Kulingana na hali ilivyo hapa Zesco, sina shaka nitaruhusiwa kuondoka kwani hawana kawaida ya kuwazuia wachezaji labda kama Yanga watashindwa kukubaliana gharama za kuninunua kwa kuwa nimebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja,” alisema Chaila.

Chaila ni mmoja wa viungo tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Zesco kilichopo chini ya kocha Lwandamina ambaye naye anadaiwa kukamilisha taratibu za kujiunga na Yanga kuvaa viatu vya Hans van de Pluijm, aliyeamua kujiuzulu.

Moja ya sifa za kiungo ni kutibua mipango ya timu pinzani pindi zinapokuwa kwenye harakati ya kusaka mabao langoni mwao.

Katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika iliyofanyika mwaka huu, Chaila alionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa klabu za Al Ahly wakati ilipovaana na Zesco kuanzia mechi ya kwanza hadi ule waliokuwa ugenini nchini Misri.

Kiungo huyo pia anahusishwa na kutakiwa na timu kadhaa za Afrika Kusini ikiwemo mabingwa wapya wa Afrika, Mamelodi Sundowns, lakini kiungo huyo amesema angependa bado kufanya kazi chini ya Lwandamina, ingawa pia anaangalia masilahi mazuri yaliyopo kwenye soka.

“Meneja wangu amepokea ofa kadhaa zikiwemo za Afrika Kusini, bado natamani kuwa chini ya Lwandamina, lakini kikubwa zaidi timu itakayowahi na kunipa fedha nzuri nitajiunga nayo,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -