Wednesday, October 28, 2020

LWANDAMINA AANZA MAJUKUMU YAKE JANGWANI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR


KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, ameanza kwa mbwembwe majukumu yake ya kukikonoa kikosi cha timu hiyo, akianza kwa kutumia zaidi ya saa moja na nusu kuzungumza na Mkurugenzi wa Ufundi, Hans van der Pluijm, wakati mazoezi yakiendelea kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam, jana asubuhi.

Lwandamina alianza kazi rasmi mnamo saa mbili asubuhi alipowasili uwanjani hapo sambamba na kikosi cha wachezaji 18 cha timu hiyo, wakiwa katika basi lao wakitokea makao makuu yao yaliyopo katika makutano ya Mtaa wa Twiga na Jangwani, jijini.

Mara baada ya kufika uwanjani hapo, Lwandamina akiwa na Pluijm, walianza kwa kujadiliana hili na lile kabla ya kuanza programu yake iliyosimamiwa vizuri na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi.

Mzambia huyo alianza kwa kuwapa mazoezi mepesi mepesi vijana wake, ili kupasha misuli moto kabla ya kuanza kucheza na mpira chini ya Mwambusi, baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa bosi wake huyo mpya.

Japo mazoezi hayo yalionekana ya kawaida, lakini kwa kiasi fulani yalikuwa yaking’ata na kupuliza, kwa maana ya kuwafua vilivyo wachezaji bila kutumia nguvu nyingi.

Wakati mazoezi hayo yakiendelea, Lwandamina na Pluijm walikuwa wakiteta kwa muda mrefu, kitendo kilichotafsiriwa kuwa wawili hao walikuwa wakibadilishana mawazo kama si Mzambia huyo kutaka kuwafahamu vizuri wachezaji kutoka kwa mtangulizi wake huyo.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo mepesi, Lwandamina, Pluijm pamoja na Mwambusi, waligawa vikosi viwili na wachezaji kuanza kucheza mechi, lakini wakiwa katika utulivu wa hali ya juu.

Pamoja na hilo, wachezaji walionekana kuwa na morali ya hali ya juu, huku kila mmoja akionekana kupania vilivyo kumwonyesha vitu adimu kocha wao mpya ambaye amepewa majukumu mazito ya kuhakikisha anaipa mafanikio makubwa timu hiyo kuanzia katika Ligi Kuu Tanzania Bara hadi ile ya kimataifa.

Katika mazoezi hayo, kikosi cha kwanza kiliundwa na Deogratius Munish ‘Dida’, Mwinyi Haji, Andrew Vicent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Amis Tambwe, Deus Kaseke, Juma Mahadh, Thaban Kamusoko na Juma Abdul.

Kikosi cha pili kiliundwa na Ali Mustafa ‘Barthez’, Pato Ngonyani, Geoffrey Mwashiuya, Said Juma Makapu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Oscar Joshua na Matheo Anthony.

Katika mechi hiyo ya mazoezi, Kamusoko, Mahadh na Abdul walionyesha vitu adimu kwa kucheza kwa umahiri wa hali ya juu kumshawishi Mzambia huyo kuwapa nafasi katika kikosi chake cha kwanza.

Kati ya wote hao, Mahadh alipiga shuti kali akiwa umbali wa mita 18, lililogonga mwamba na kumfurahisha vilivyo Lwandamina.

Mara baada ya kumalizika mazoezi hayo, Lwandamina aliwasogelea baadhi ya wachezaji wake na kuwaangalia mara mbili mbili kuonyesha jinsi walivyomkuna.

Akizungumzia mazoezi hayo, Mzambia huyo alisema: “Nimeshuhudia hali ya kujituma, nidhamu ya kumsikiliza mwalimu na uelewa mzuri kutekeleza majukumu waliyopewa, nimpongeze mwalimu kwa mazoezi mazuri ya ‘warm up’ baada ya likizo ndefu.”

Wachezaji waliokosa mazoezi hayo ni Donald Ngoma, Haruna Niyonzima, Hassan Kessy, Vincent Bossou, Beno Kakolanya, Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Yusuf Mhilu, ambao wameelezwa kukabiliwa na sababu mbalimbali.

Lwandamina amekabidhiwa klabu hiyo ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL, pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Simba, ambao wana pointi 35, hivyo mtihani wake wa kwanza utakuwa kuishusha timu hiyo ya Msimbazi kutoka kileleni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -