Wednesday, October 21, 2020

LWANDAMINA AANZA NA MIDO ‘MKATA UMEME’

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY

KOCHA mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, ameanza kuimarisha kikosi chake kwa kumvuta kiungo mkabaji wa Zesco United, Justice Zulu ambaye anatarajia kutua nchini leo akitokea kwao Zambia kujiunga na miamba hiyo ya Jangwani.

Licha ya Lwandamina kusema kuwa hana mpango wa kumsajili wakati huu wa dirisha dogo kutokana na kujitosheleza kwa kikosi chake, BINGWA lina taarifa kuwa kauli hiyo ya Mzambia huyo ilikuwa kuwatoa kwenye reli wapinzani wake, lakini ukweli ni kuwa Zulu anakuja kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo.

Ujio wa Zulu unatajwa kuja kumaliza tatizo sugu la kiungo mkabaji (namba sita) ambalo limeitesa klabu hiyo ya Jangwani kwa misimu kadhaa tangu alipoondoka Athuman Iddi ‘Chuji’ na Frank Domayo.

BINGWA lina taarifa kuwa Yanga inamleta Zulu, baada ya kushindwa kunasa saini ya kiungo mkabaji mwingine wa Zesco United, Meshack Chaila ambaye ana mkataba wa muda mrefu na miamba hiyo ya Zambia ambayo ilikuwa inataka mkwanja mrefu ili kumwachia.

“Kocha alisema hana mpango wa kusajili ili kuwapoteza wapinzani wetu, si unajua mara nyingi Yanga tunapenda kufanya mambo yetu kwa siri,” alisema mtoa habari wetu (jina tunalihifadhi) na kuongeza: “Kwani hata suala la ujio wa George Lwandamina si unakumbuka viongozi walikanusha hata baada ya kutua Tanzania, lakini mwisho wa siku ndiye aliyekabidhiwa majukumu.

“Mimi ninakuhakikishia Zulu anakuja kesho (leo) kama mipango itakwenda jinsi ilivyopangwa kwa kuwa suala la  tiketi tayari limekamilika, ingawa ujio wake unafanywa kwa siri kubwa na hata kama atawasili, upo uwezekano akenda kufichwa kama ilivyokuwa kwa Lwandamina hadi mipango ikamilike ndipo atatambulishwa.”

Ujio wa Zulu ambaye ni kiungo mkabaji mwenye uwezo na chaguo la Lwandamina, ni wazi utakuwa umemuweka kwenye wakati mgumu kiraka Mbuyu Twite ambaye mara kwa mara imekuwa ikidaiwa kuwa anaweza kufunguliwa milango ya kutokea.

Moja ya sifa zilizomshawishi Lwandamina kumleta Zulu  ambaye ni raia wa Zambia, ni umahiri wake wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji lakini pia uwezo wake wa kupiga mabao ya mbali.

Zulu ana sifa ya kuwa kiungo ‘mkata umeme’ mwenye sifa ya kuusoma mchezo na kuzuia mashambulizi ya timu pinzani na kulinda ukuta wake ipasavyo na pia ana sifa ya kupiga pasi zenye macho, kitu kinachomfanya kuwa mchezaji sahihi ambaye Yanga imekuwa ikimsaka kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, kikosi cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kinatarajia kuanza mazoezi yake leo katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kuanza mazoezi yamekamilika na leo ndiyo wataanza kujiandaa na mzunguko wa pili wa VPL.

“Tunaanza mazoezi kesho (leo) katika Uwanja wa Chuo Cha Polisi Kurasini, kama unavyofahamu huku hakuna mwandishi wala mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia,” alisema Hafidh na kuongeza: “Kwa upande wa wachezaji wote tayari wamepewa taarifa na kwa wale wanaotoka nje ya Tanzania wameshawasili.

“Ni lazima wachezaji wote wafike kwa wakati kwani hivi sasa kikosi kipo chini ya kocha mpya ambaye hamjui mtu na baada ya mazoezi ya kesho (leo), kutakuwa na kikao kizito kati ya wachezaji na kocha Lwandamina.”

Lwandamina amekabidhiwa klabu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba ambao wana pointi 35, hivyo mtihani wake wa kwanza utakuwa kuishusha timu hiyo ya Msimbazi kutoka kileleni.

Lwandamina ambaye anachukua mikoba ya Hans van der Pluijm ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo ya Jangwani, ametua Yanga akiwa ametoka kuifikisha Zesco United ya Zambia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -