Friday, January 15, 2021

LWANDAMINA AANZA NA MO IBRAHIM

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MWANDISHI WETU,

KOCHA wa Yanga Mzambia, George Lwandamina, amemwangalia kiungo mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo’ na kuridhika na uwezo wake kisha kuamua jambo moja kubwa kwenye kikosi chake.

Katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, kocha huyo alimshuhudia nyota huyo alivyowahangaisha viungo wake hasa Said Juma ‘Makapu’ na Thaaban Kamusoko, lakini badala ya kuwalaumu wachezaji wake aliamua vingine kabisa na maamuzi hayo yanaweza kuiimarisha sana na kuiliza Simba siku zijazo.

Mzambia huyo baada ya kubaini ukali wa Mo Ibrahim, kuna mambo matatu anataka kuyafanya na kuwataka Yanga kuyafanya dhidi ya Simba.

Moja ni kuwaongezea kasi viungo wake wakabaji, pili ni kuwanyumbulisha zaidi na tatu kuwaongezea umiliki ya mpira kwani vitu hivyo vitatu vilionekana kuwa ni tatizo lililosababisha Mo kuwasumbua sana kwenye mchezo huo.

Yanga wanaojiandaa kucheza na Majimaji katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Januari 17 mwaka huu, Lwandamina leo amepania kuanza na makosa ya safu ya kiungo aliyoyaona baada ya kuonyeshwa na Mo.

Lwandamina anaamini kiungo wa Simba,  Mohamed Ibrahim maarufu kwa jina la Mo, alikuwa bora zaidi kutokana na  kucheza vizuri eneo la  katikati, lakini akionekana ni mwiba mchungu kwa viungo na mabeki wake.

Habari zilizopatikana kutoka kwenye benchi la ufundi la Yanga, zilisema kwamba, Lwandamina amebaini udhaifu katika idara ya viungo na atalifanyia kazi haraka kabla ya kuanza mechi za kimataifa.

“Ni kweli kiwango cha Mo kimemfanya kocha kujua aina ya viungo alionao na pia kuona udhaifu wao, Mo aliwasumbua sana naye amesema lazima afanyie kazi suala hilo kabla ya kukutana na Simba tena au kabla ya kuanza michuano ya kimataifa,” alisema mtoa habari wetu.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa timu hiyo wanatarajia kuanza mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Majimaji ambao walipewa mapumziko ya siku mbili baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema wachezaji wao wamejulishwa kuendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwao kushinda ili waweze kutetea taji lao.

“Tulikuwa tumewapa mapumziko baada ya kutoka Zanzibar na leo (jana), naendelea kuwapa taarifa ya kuanza mazoezi,” alisema.

Yanga wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na pointi 40 huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 44.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -