Sunday, November 29, 2020

LWANDAMINA AITIKISA ZANACO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

BAADA ya Yanga kufuzu kwa hatua ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo itakutana na Zanaco ya Zambia, wapinzani wao hao wanaonekana kutikiswa na rekodi za kocha George Lwandamina.

Mechi baina ya Yanga na Zanaco inatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 10 hadi 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa na kisha mechi ya marudiano itachezwa nchini Zambia wiki moja baadaye.

Uwoga uliowaingia Zanaco unatokana na kocha wa Yanga wa sasa, Lwandamina kuwafahamu vizuri na kulifahamu soka la Zambia, hivyo wanajua kwamba wana wakati mgumu.

Kwenye mtandao wa mashabiki wa klabu hiyo ya Zambia, waliandika: “Lwandamina Again”, kwa maana ya Lwandamina tena, jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wana hofu na kocha huyo ambaye alikuwa akiifundisha Zesco United ya nchini humo kabla ya kutua Yanga.

Zanaco iliyopata nafasi hiyo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda. Zanaco inanolewa na kocha Mumamba Numba, kiungo wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia.

Kocha huyo ambaye ameanza kukinoa kikosi hicho mwaka 2014, amekuwa hana rekodi nzuri anapokutana na Lwandamina tangu alipokuwa Zesco, hivyo hali hiyo imeonekana kuwatia hofu mashabiki wa timu hiyo.

Hata hivyo, katika mechi nne za mwisho ambazo Lwandamina aliingoza Zesco dhidi ya Zanaco, kocha huyo atakuwa na kumbukumbu ya kipigo kikubwa cha mabao 4-0 oktoba 31, mwaka 2015 wakati yeye alishinda bao 1-0 Julai 12, 2015 na nyingine za mwaka jana timu hizo zilitoka sare.

Zanaco kwa sasa wanaongoza msimamo wa ligi yao kwa kuwa na pointi 38, huku wapinzani wao wa jadi Zesco wakiwa na pointi 36.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -