Wednesday, October 28, 2020

Lwandamina aja na makocha wawili

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA ZAINAB IDDY

KOCHA Mpya wa Yanga,  raia wa Zambia, George Lwandamina,  anatarajiwa kutua nchini  keshokutwa na wasaidizi wake wawili kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo kwenye michuano ya  Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa mwakani.

Lwandamina, aliyeiongoza Zesco ya Zambia kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika  mwaka huu na kuiwezesha kutinga nusu fainali, imeelezwa atakuja na kocha msaidizi na wa viungo.

Ujio wa Lwandamina unatokana na uongozi wa Yanga kuelezwa kukatisha mkataba wa kocha mkuu wa timu hiyo,  Hans van der Pluijm na Msaidizi wake, Juma Mwambusi.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya Yanga zilieleza kwamba, Lwandamina amekubaliwa kuja na wasaidizi, lakini akipendekeza kocha wa makipa, Juma Pondamali kubaki katika safu yake ya benchi la ufundi.

Mtoa habari wetu alisema Lwandamina anahitaji kufanya kazi na watendaji wake aliokuwa nao Zambia,  akiamini watamsaidia majukumu yake kwa ufanisi mkubwa Yanga.

“Katika makubalino yetu ya awali tumemtaka ahakikishe anaiwezesha Yanga angalau katika nusu fainali ya Ligi  Mabingwa Afrika mwakani  na ametuomba aje na watu wake atakaofanya nao kazi.

“Tumempa ruhusa ya kufanya mabadiliko anavyotaka katika usajili na hata benchi la ufundi, kwa kuwa sisi tunataka kuona Yanga inafika mbali kimataifa, hatuna pingamizi na kile anachokitaka,” alisema mtoa habari wetu.

Lwandamina amewahi kufanya kazi kwa karibu zaidi na Chembo Tenant  na Mwinga Chuma, ambaye  ni kocha wa  viungo  akiwa Zesco.

Akizungumzia ujio wake, Lwandamina ameliambia BINGWA kuwa kila kitu kimekamilika baada ya kumalizana na waajiri wake wa zamani, Zesco na keshokutwa atawasili jijini Dare Salaam, tayari kwa kuanza kibarua kipya .

“Hahahaaaa  rafiki yangu mambo yote yapo sawa,  kimsingi nimemalizana na Zesco, nasubiri tu tiketi ya ndege nije Tanzania siku ya Jumatano,” alisema Lwandamina.

Lwandamina aliwataka wana- Yanga kutokuwa na wasiwasi juu ya ujio wake na kusisitiza anakuja Tanzania kufanya kazi ya kuipa mafanikio klabu hiyo.

“Naomba sana ushirikiano wenu, haswa nyinyi waandishi wa habari, nitafanya kazi nanyi kwa karibu zaidi  kuipa mafanikio Yanga,” alisema katika mahojiano yake na BINGWA kwa njia ya simu jana.

Kocha huyo alisema amejipanga kuhakikisha anarudisha heshima ya timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa, baada ya mwaka huu kutolewa katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lwandamina anakuwa kocha wa saba  kuifundisha Yanga kuanzia mwaka 2010,  baada ya Kostadin Papic, Sam Timbe, Tom Saintfiet, Ernie Brandts,  Marcio Maximo na Pluijm.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -