Friday, November 27, 2020

LWANDAMINA AKILI NYINGI, NGUVU KIDOGO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMAR NA SAADA SALIM,

AKILI nyingi nguvu kidogo, hivi ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, kuwapa mazoezi ya kisomi na kitaalamu wachezaji wake, baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo, Yanga walionekana kuupiga mwingi, huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Haruna Niyonzima, akitengeneza pasi zote za mabao matatu, mawili yakifungwa na winga Simon Msuva na moja la kujifunga.

Katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru, benchi la ufundi la timu hiyo, likiongozwa na Lwandamina, lilionekana kuwapa mazoezi mepesi wachezaji wa timu hiyo kwa nia ya kurudisha miili yao katika hali ya kawaida, baada ya kupata uchovu wa mechi.

Lwandamina alionekana kuwapa mazoezi hayo mepesi ya kurukaruka, kunyoosha viungo, kukimbia kidogo, kupigiana mipira pasi katika mtindo wa taratibu pasipo kutumia nguvu wachezaji wake.

Mazoezi hayo yalichukua takribani dakika 45, ambapo BINGWA lilishuhudia kikosi cha timu hiyo kikiwasili uwanjani hapo  majira ya saa 3 na kuanza moja kwa moja programu yao ya siku.

Wakiwa uwanjani hapo, makocha wasaidizi wa Yanga, Juma Pondamali, Juma Mwambusi na Noel Mwandila, muda wote walionekana kufurahia jambo, ikiwa ni pamoja na kuwapa vitu adimu vyepesi vyepesi wachezaji wao.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo mepesi ya viungo, Lwandamina aligawa makundi mbalimbali ya wachezaji na kuanza kuchezea mipira pasipo kutumia nguvu, zoezi ambalo lilionekana kufurahiwa na wachezaji wote wa timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -